Nesi Feki Anaswa
Aibu Kubwa ya Kusikitisha, Kilichomkuta Dada Huyu Ama kwa hakika hawezi Kusahau Maishani Mwake . Nesi Feki Ambaye Alinaswa Akiiba Mtoto Hospitalini Huko Nchini Ghana.
Tukio Hilo Lilitokea Wakati Dada huyo Alipoamua Kuvalia Sare za Hospitali kama Nesi na Kuamua Kuingia Wodi Ambayo Watoto Waliotoka Kuzaliwa Huhifadhiwa Kwa Muda kabla ya Kukabidhiwa kwa Mama zao.
Baada ya Kufaulu Mtihani huo na Kuweza Kujipenyeza hadi kwenye Wodi Hiyo , Nesi Feki Huyo Alimchukua Mmoja Kati ya Watoto Aliyeonekana Kuvtiwa nae na Kumficha Kwenye Begi Lake Akioekana kama Vile Amebeba Nguo.
Balaa Lamkuta
Balaa Lilimkuta Dada Huyo Kipindi Ambacho Alikuwa Akijaribu Kutoka Nje ya Hospitali Hiyo na Kwa Bahati Mbaya Mtoto Aliyekuwa Amemficha Ndani ya Begi Lake Akaanza Kulia Kwa Nguvu.
Mshangao
Walinzi wa Hospitali Ilibidi Kumzuia Kwa Muda Dada Huyo (Nesi Feki) Ili Kuweza Kumkagua na Kuona ni Kitu Gani Kilichopo Ndani ya Begi Alililokuwa Amelishikilia. Ndipo Kwa Mshangao Mkubwa Walinzi Walipomwona Mtoto huyo Mchanga Akiwa Ndani ya Begi Huku Akitapatapa Kutafuta Pumzi.
Atembezwa Mtupu
Wananchi wenye Hasira Kali Walianza Kumvamia kwa Kumpiga Bila Huruma na Kufanikiwa Kumvua Nguo zake na Kuanza Kumtembeza Barabarani. Hii Ni Aibu Kubwa Kuwahi Kuipata dada huyo Ambapo Wengi wamelihusisha Tukuio Hilo na Dhamira ya Kufanya Vitendo vya Kishirikina.