Pages

February 18, 2014

KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) Wamshitaki Rais Kikwete ICC kwa kutoa kauli zenye kuhamasisha Uvunjifu wa amani nchini.

KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.
tcib

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu  yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.