MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama
Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana
kwa jina moja la Nagar.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.