KIBAO kimegeuka! Yule Mganga wa Diamond anayejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya yamemkuta mazito.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa jamaa huyo anahenyeshwa na polisi akiwa mahabusu kufuatia madai ya wizi wa gari aina Toyota Rav 4 ‘milango mitatu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, gari hilo liliibwa wiki kadhaa maeneo ya Msimbazi-Kariakoo jijini Dar.
HABARI ZA AWALI
Habari za awali zilidai kuwa gari hilo lilifika mikononi mwa Ustadh(Mganga wa Diamond) kutoka kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mwanahamis ambaye ilisemekana kwamba alikuwa akichukua dawa kwa mganga huyo.
Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo naye alihongwa gari hilo na mume wa mtu huku akiwa hajui kuendesha hivyo aliliweka poni kwa Ustadh ambaye alimpa dawa ambayo aliipeleka Kigoma kuwauzia watu wake.
Hata hivyo, ilizidi kudaiwa kwamba mwanamke huyo alichukua dawa za shilingi milioni 3 lakini akashindwa kurudisha fedha hizo na riba waliyokubaliana namganga wa Diamond.
Ikazidi kudaiwa kuwa, Ustadh alimuongezea dawa nyingine mwanamke huyo hadi kufikia deni la shilingi milioni 6 ndipo akaamua kulichukua gari hilo.
Ikazidi kudaiwa kuwa, Ustadh alimuongezea dawa nyingine mwanamke huyo hadi kufikia deni la shilingi milioni 6 ndipo akaamua kulichukua gari hilo.
NI UZEMBE?
Ukiacha stori hizo za awali ambazo zilikosa ‘balansi’, kuna habari nyingine kuwa gari hilo mali ya Edric Magayane liliibwa baada ya kuachwa eneo la tukio likiwa ‘sailensi’ bila mtu ndani.
Ilielezwa kwamba aliyekuwa na gari hilo aliingia dukani kununua vitu na alipotoka alichanganyikiwa akidhani gari hilo lilikuwa limevutwa na watu wa ‘breki dauni’ waliokuwa wakivuta magari yaliyoegeshwa hovyo katikati ya jiji.
Habari zinasema kuwa mhusika alikwenda kulitafuta katika ‘yadi’ zinakopelekwa magari yaliyovutwa lakini hakuliona.

POLISI
“Alichokifanya ni kwenda kuripoti polisi ambao walianza kulisaka Dar bila mafanikio.
“Wakati polisi wakiendelea kulisaka kuna mtu akasema amemuona Ustadh akitanua nalo.
“Yule mwenye gari (Magayane) alimtafuta Ustadh hakumpata. Akaelekezwa nyumbani kwake, Kigogo Luhanga, Dar au Urambo, Tabora.
“Jamaa alipatafuta nyumbani kwa Ustadh, Kigogo hadi akafika akiwa na polisi waliovalia kiraia lakini hawakumkuta.
ALITAKA KULIRUDISHA?
“Waliambiwa amesafiri Tabora. Pia walihakikishiwa kwamba kweli Ustadh alikuwa na gari hilo. Jamaa akaambulia namba za simu.
“Alipompigia simu Ustadh ambaye ni Mganga wa Diamond alimwambia kama gari limeibwa ana uwezo wa kutumia uganga wake kulirejesha kwa kuwa ni mtaalam wa mambo hayo.
“Ustadh aliomba apewe fedha ili afanye mambo yake gari lirudi. Kweli alitumiwa fedha, lakini akawa anazungusha huku akijiita majina lukuki kama Maimuna na mengine,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

MKOKO WATAFUTIWA MTEJA
Baadaye polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa, gari hilo lilikuwa likitafutiwa mteja mkoani Tabora lakini ilishindikana kutokana na kukosa ‘dokyumenti’ muhimu.
GARI LAKAMATWA
Habari zilizidi kutiririka kwamba, wakati Ustadh akikatiza na gari hilo Tabora mjini ndipo alipokamatwa na polisi kisha kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu kabla ya kusafirishwa jijini Dar kwa hatua zaidi za kisheria.

MASHITAKA MAWILI
Habari za uhakika zilieleza kuwa, Ustadh alipofikishwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central), Dar alifunguliwa mashitaka mawili; wizi wa gari na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
Baada ya kujikusanyia habari hizo, juzi gazeti hili lilishuhudia polisi wakipekuwa nyumbani kwa Ustadh kisha kumrejesha kituoni kwa ‘difenda’ huku amepigwa pingu mikononi.
Baada ya kujikusanyia habari hizo, juzi gazeti hili lilishuhudia polisi wakipekuwa nyumbani kwa Ustadh kisha kumrejesha kituoni kwa ‘difenda’ huku amepigwa pingu mikononi.
MMILIKI ANENA
Akizungumza na gazeti hili juzi, mmiliki wa gari hilo, Magayane alikiri maelezo yote juu ya habari hiyo.
Alipoombwa namba ya jalada la kesi aliitaja kuwa ni MS/RB/827/ 2014-WIZI WA GARI NA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA ISIYO HALALI.
Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Ustadh juu ya msala huo mzito ziligonga mwamba kwa kuwa simu yake ilikuwa haipatikani na bado alikuwa mahabusu huku ikelezwa kwamba soo limemkalia vibaya.

DIAMOND KAINGIA MITINI?
Kwa mujibu wa chanzo kingine, Diamond Platinumz amekuwa akiombwa kumsaidia jamaa lakini akaingia mitini kwa madai kuwa hapendi kuhusishwa na Ustadh ambaye aliahidi msanii huyo kupata majanga makubwa baada ya kumkimbia na kwenda kwa waganga wengine.
Diamond alipotafutwa juzi kwa njia ya simu hakupatikana huku mmoja wa watu wa timu yake akisema yupo Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwa ajili ya kufanya kolabo na D’Banj wa Nigeria. Hii ni Aibu kubwa kwa mganga wa Diamond