Pages

Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

June 08, 2014

CHEKI KIKOSI CHA BARAZILI PAMOJA NA NAMBA ZAO KOMBE LA DUNIA 2014

Full list of Brazil's 23-man Fifa World Cup squad as head coach Luiz Felipe Scolari names his players for Brazil 2014 

Brazil head coach Luis Felipe Scolari names provisional 23-man squad for World Cup finals 

Brazil coach Luiz Felipe Scolari's 23-man squad for the World Cup finals:

Goalkeepers: Julio Cesar (Toronto FC), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro)
Defenders: Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (AS Roma), Maxwell, Thiago Silva (both Paris St Germain), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Henrique (Napoli)
Midfielders: Paulinho (Tottenham Hotspur), Ramires, Willian, Oscar (all Chelsea), Hernanes (Inter Milan), Luiz Gustavo (VfL Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City)
Forwards: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Jo (Atletico Mineiro), Hulk (Zenit St Petersburg)
Full World Cup 2014 squad lists:
Group A - Cameroon / Croatia / Mexico / Brazil
Group B - Chile / Holland / Australia / Spain
Group C - Greece / Ivory Coast / Colombia / Japan
Group D - Italy / Uruguay / Costa Rica / England
Group E - Honduras / France / Ecuador / Switzerland
Group F - Nigeria / Iran / Bosnia-Herzegovina / Argentina
Group G - Ghana / Portugal / USA / Germany
Group H - South Korea / Russia / Belgium / Algeria

 

 

Cameroon sasa wapanda ndege ya Brazil

Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ngapi wameongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

Papa awapokea Peres na Abbas

 Mahmoud Abbas, Papa na Shimon Peres Vatikani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.
"Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema
Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:

"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.
Na kwa upande wake Bwana Abbas aliombea amani katika mkutano huo," alisema Peres.

Naye kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliomba kwenye hafula hiyo.

"Ee Bwana, tuletee amani ya kudumu na ya haki katika taifa letu na eneo letu, kwa ujumla, ili watu wetu na watu wote wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima ifurahie matunda ya amani, utangamano na kuishi kwa pamoja kwa upendo.
Baada ya sherehe hiyo, iliyoshirikisha maombi ya Kikristo, Kiyahudi na Kiislamu, waliokuwepo walisalimiana kwa mikono na kupanda Mzaituni katika Medani ya Vatican kama ishara ya amani.
Papa ametangaza hadharani kuwa hataki kuingilia moja kwa moja mashauriano ya amani ya Mashariki ya kati, yaliyoporomoka Aprili lakini akasema kuwa anatarajia kwamba mkutano katika Vatican utapunguza uahasama kati ya pande hizo mbili kinzani za Mashariki ya Kati

June 07, 2014

Wimbo wa Stevie Wonder ni kitambulisho




 

Wimbo wake Stevie Wonder, Another Star, utakuwa wimbo utakaopeana sauti mrejeo katika maonyesho ya BBC ya kombe la dunia.
Wimbo huo, pamoja na ule wa Kilatino , zitatumika kama nyimbo za kufungua vipindi vyote vya Kombe la Dunia Brazili 2014,


Wonder aliutoa wimbo huo kiasili, katika mwaka wa 1976, kwenye albamu yake iliyoshinda tuzo la Grammy mara nyingi, iitwayo Songs in the Key of Life.
Wimbo huo, kwa mara ya kwanza utachezwa kwenye kituo cha BBC One tarehe 11, Juni, saa ili kukitambulisha kipindi kinachoangazia kipute hicho cha kombe la dunia.
Mtayarishi mkuu wa kitengo cha michezo, BBC, Ian Finch alisema kuwa BBC ilikua yenye bahati kupewa ruhusa ya kutumia wimbo huo.
‘Wimbo huu unaonyesha kwa uzuri hisia za sherehe na furaha ambazo tutawaletea watazamaji wetu katika msimu huu wa kombe la dunia.’ Finch.
BBC Kutumia nyimbo za Stevie Wonder kama kitambulisho
BBC itaonyesha kwa kina Kombe la Dunia.
Itaonyesha michuano ya moja kwa moja katika BBC One, BBC One HD na tovuti ya BBC Sport na BBCSwahili.
Michuano mingine itakua ikiendelea katika BBC Three, BBC Three HD na Red Button.
BBC Two na BBC Two HD zitaonyesha mchuano huo kwa kifupi masaa ya asubuhi, na pia marudio ya mchuano wote .

Rais Jacob Zuma alazwa hospitalini


Rais Zuma anatarajiwa kupumzika kwa muda kabla ya kurejea kazini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.














“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’
Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC kilishinda uchaguzi huo.
Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.

March 11, 2014

MFAHAMU PASTA ANAYEHUBIRI KANISANI HUKU AKIWA NA NYOKA SHINGONI



Pasta anayejulikana kuhubiri akiwa amemweka nyoka shingoni ameaga dunia. Pasta Jamie Coots anayeamini kuwa kinga hutoka kwa mungu aliweza kupoteza maisha yake baada nyoka huyo wa sumu kumuuma akiwa akihubiria mbele ya maumini.
Ilikuwaje hadi pasta huyo kuhubiri na nyoka mgongoni?

Kupitia andiko la Marko 16:15-18, pasta huyo anaamini kuwa Yesu aliweza kuwaambia wakristo wote kuwa wanaweza kushika nyoka na hatawaumiza wala kuwadhuru bora tu uwe umebarikiwa na mungu mwenyewe.

Pasta huyo wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name aliumwa na nyoka huyo mbele ya kanisa lake na ilimbidi kukimbizwa hadi nyumbani kwake bila kupelekwa hospitalini.

Wauguzi walipowasili nyumbani kwake waliweza kufukuzwa huku pasta huyo akiwa na imani kuwa mungu atamtibu ugonjwa wake, jambo ambalo halikufanyika.

March 06, 2014

Baada ya Rais Museveni Kupitisha Sheria kali Dhidi ya Mashoga na Wasagaji, Binti wake Ajitangaza kuwa Msagaji.

Imeelezwa kwamba habari hiyo ilianzia kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani itwao Abril Uno, ambao uliandika habari hiyo wiki iliyopita siku yaJumatano.

Kwenye tarifa yake mtandao huo ulitania kwa kuandika kwamba Diana Kamuntu, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amejitangaza kuwa ni msagaji kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio.

lesbian
Taarifa hiyo ilisema: “Mimi ni msagaji, ninafanya mapenzi ya jinsia moja. Nimelijua hilo toka nilivyokuwa msichana mdogo,” taarifa ilimnukuu Kamuntu.
Kwenye mtandao wa Abril Uno ulimtaja muendesha kipindi wa redio hiyo James Kasirivu, kuwa ndiye aliyekuwa akifanya mahojiano hayo, na kusema kwamba “alipatwa na mshangao na mpaka aliishiwa na maneno ya kuongea toka kinywani mwake.”
Maelezo hayo yalisambaa kwenye mitandao mingi Duniani, huku wengine kuitoa na wengine kuiacha.
Watu wengi waliguswa na taarifa hiyo huku baadhi yao wakiandika kwenye kurasa zao za Twitter katika hali ya kumuunga mkono Kamuntu:
Abril Uno, ni jina lenye maana ya ’1 April’ kwa Kihispania, ambayo ni siku ya wajinga.
Hivyo akili Kichwani Mwako.

March 03, 2014

PICHA: HII NDIO BENDI INAYOTIKISA DUNIANI, HAPA BAIKOKO NI CHA MTOTO!





Hii ni Aibu hawa wanafanya matukio machafu kama haya ili mradi tuu kuvunja rekodi ya dunia Dunia hii inaenda wapi jamanii daah
Dunia inaongozwa na matukio machafu sana kwa sasa matukio haya mengi yanafanyika ili kupata pesa wengine wanadiliki hata kufanya mambo ya aibu katika jamii ilimradi wapate pesa ya kujikimu kimaisha












FACEBOOK, INSTAGRAM NA WHATSAPP KUSITISHA KUTOA HUDUMA NCHINI UGANDA BAADA YA RAIS WA NCHI HIYO YOWERI MUSEVENI KUPANGA SHERIA YA KUZUIA USHOGA


Ikiwi ni siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kusaini muswaada wa sheria ya kupinga ushoga nchini humo, kampuni ya Facebook imetangaza uwezekano wa kusitisha huduma zake nchini Uganda kama njia ya kupinga uamuzi huo ambao wamedai kuwa unakiuka haki za baadhi ya watu.
 
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inasema kuwa, Facebook ilianzishwa kusupport haki za binadamu kwa kuwapa nafasi watu wote ya kujielezea kwa uhuru, hivyo wanasikitishwa kujua kwamba Uganda kama nchi imesaini muswaada wa sheria ya kupinga ushoga.
 
Taarifa hiyo inaendelea kusema Facebook kwa sasa inatazama upya juu ya kujihusisha kwake kutoa huduma nchini Uganda, na kuongeza kuwa kusitisha kutoa huduma zake za Facebook, Instagram na Whatsapp nchini humo kwa muda watakaoona unafaa, ni moja ya hatua wanayofikiria kuchukua kama njia ya kuonesha kutoridhishwa kwao na uamuzi huo.
Isome taarifa hiyo:

STATEMENT FROM FACEBOOK ON ANTI-HOMOS6XU8LITY LAW
 
When we launched Facebook, we thought it as a platform to advance people’s rights and liberties of self expression in all form. We were equally shocked to learn that Uganda as a country had gone ahead to sign the Anti Homos9xu9lity bill into a law.

Facebook is currently reviewing its engagement to Uganda, as we seek to come up with a voice to express our dissatisfaction. And of course, suspending our operations in Uganda is one of the options we are considering. In the event that we suspend operations in Uganda, our platforms of Instagram, Facebook and Whatsapp will be off for a time we shall deem necessary.

We strongly condemn the act of the Ugandan Government to overstep the rights of a minority. All humans are created equal and deserve a right to freedom and happiness.
Signed
Sheryl Kara Sandberg
Chief Operations Officer (COO) At Facebook
 
Mmoja wa wamiliki wenza wa Facebook, Chris Hughes ni shoga na aliolewa na June 30, 2012 na mwanaume mwenzake, Sean Eldridge.
 ******
(Kwa  hisani ya  Bongo5

MAN CITY YATWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE


LONDON, England
KOCHA Manuel Pellegrini amefanikiwa kutwaa taji la kwanza akiwa bosi wa Manchester City baada ya jana kuifunga Sunderland katika fainali ya Kombe la Capital kwa mabao 3-1kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.
Kocha huyo raia wa Chile ambaye yupo katika adhabu ya kukosa mechi tatu za Ulaya baada ya kufungiwa na Shirisho la Soka la Ulaya (Uefa) kutokana na kumtolea lugha kali mwamuzi, Jonas Eriksson, alikuwa na furaha jana kutokana na ushindi huo.
Licha ya Sunderland kuanza kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 10 kupitia kwa Fabio Borini, ilijikuta ikizidiwa nguvu na kupata kipigo hicho kipindi cha pili.
Yaya Touré ndiye aliyefunga bao kali kwa shuti katika dakika ya 55, wapinzani wao hao walijikuta wakipagawa na kufungwa la pili dakika moja baadaye na Samir Nasri.

AL AHLY WASUSA VYAKULA, NI BAADA YA KIPIGO

Mohammed Mdose na Said Ally
KIPIGO cha bao 1-0 walichokipata Al Ahly dhidi ya Yanga, kimeonyesha kuwachanganya vilivyo Waarabu hao, kwani baada ya mchezo walionekana kutupatupa ovyo vyakula walivyokuwa navyo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Waarabu hao walikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, juzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa bao safi lililofungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Championi lilifanikiwa kupenya kwenye chumba walichokuwemo Al Ahly na kushuhudia matunda aina ya apple, ndizi na juisi vikiwa vimezagaa chini katika chumba hicho huku wachezaji hao wakiwa hawana muda navyo, kwani wengi wao walionekana kujadili kipigo hicho.
Championi lilijaribu kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kujua kwa kina chanzo cha mkasa huo, lakini walionekana kuwa na hasira na kugoma kuzungumza chochote.
Hali ilikuwa tofauti katika chumba cha timu ya Yanga ambamo wachezaji wake walikuwa wenye furaha muda wote huku wakipongezana.
Yanga na Al Ahly zinatarajiwa kurudiana mwishoni mwa wiki hii jijini Cairo.

March 02, 2014

WATU 28 WAUAWA CHINA

Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakiwa hospitali.
Miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo.
Baadhi ya mizigo iliyoachwa eneo la tukio.
Ulinzi ukiimarishwa eneo la tukio.
KUNDI la watu waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni mjini Kunming, China!
Mashahidi wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao waliovalia nguo nyeusi, waliwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Polisi walifanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya shambulio hilo.
Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo.

February 17, 2014

VIDEO (18+ ONLY): WANAFUNZI WA CHUO WAKIFUNDISHANA JINSI YA KUNGONOKA,,,,!

 
Kweli vyuo vyetu siku hizi maadili hamna yaani badala ya kusoma wadada hawa wamebuni namna ya kuwafundisha wengine namna ya kumhandle mwanaume....

Inasemekana haka kamtindo kameenea sana baada ya wanachuo wengi hasa wanaotoka vivijin kutofahamu staili mbalimbali hivyo hufurahia sana lesson hiyo.

February 16, 2014

Kutana na Delfina Cedeno, Msichna wa Miaka 19 anayetoka Machozi na Jasho la Damu akiwa na Huzuni..!!

Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.
Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.
Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa  kumsaidia.
Cedeno alisema: ‘Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri – nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.
‘Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.’
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake.



Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.



February 14, 2014

UN kuzuru eneo la mauaji DRC

Maelfu ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita vya waasi ambavyo haviishi
Ndege za umoja zizizokuwa na Rubani Goma
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinatarajiwa kuzuru eneo ambako mauaji ya watu wengi yalifanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Hatua hii inakuja baada ya kikosi cha walinda amani cha Umoja huo nchini humo (Monusco) kugundua vijiji vitatu viliteketezwa.
Kikosi hicho kilisema kuwa zaidi ya watu hao sabini waliuawa mwishoni mwa mwezi uliopita na mapema mwezi huu.
Katika mahojiano na BBC, afisa mmoja wa shirika la Monusco, mjini Goma, Ray Tores, amesema kuwa ndege ya wanajeshi wake, iliyokuwa ikifanya uchunguzi, katika eneo hilo iligundua kuwa vijiji vitatu viliteketezwa na kuharibiwa kabisa.
Amesema kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa watazuru eneo hilo baadaye hii leo ili kufanya uchunguzi zaidi.
Jeshi la kutunza amani la Umoja wa Mataifa limeimarisha juhudi zake katika eneo hilo, hasa tangu lilipolisambaratisha kundi la waasi wa M23, Novemba mwaka uliopita.
Bwana Torres, amesema kuwa zaidi ya makundi arubaini ya waasi yanajulikana kuendesha operesheni zao katika eneo hio la Goma.
Manne kati yao yamekuwa yakifanya mashambulio ya mara kwa mara na hivyo kuwa tishio kubwa la usalama.
Umoja wa Mataifa, umesema kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na makundi ya waasi yaliyojihami katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, ili kuwatia hofu watu wanaoishi katika eneo hilo.
Afisa huyo amesema kuwa wengi wa waliouawa walikuwa na majeraha ya mapanga.

February 13, 2014

MBUNGE WA CCM BAHI AGOMA KUJIUZULU BAADA YA KUANDAMWA NA KASHFA ZA UBADHILIFU WA FEDHA ZA JIMBO.

MBUNGE wa Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Omar Baduel amesema hatajiuzulu kwenye nafasi hiyo, kutokana na kuandamwa na baadhi ya madiwani kwa tuhuma za kutumia vibaya fedha za mfuko wa jimbo. Alitoa kauli hiyo juzi kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya Bahi.
Alisema hayo baada ya kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yake, kutoa taarifa na kuonesha Mbunge huyo alitumia kwa maslahi yake fedha za Mfuko wa Jimbo, ambao hutolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
“Sio kweli hayo yaliyoandikwa kwenye taarifa, niliitwa kwenye tume, niliyosema humo hayamo, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” alisema.
Alisema hiyo si mara ya kwanza kuandamwa na baraza hilo la madiwani, kwani hata alipokuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, ilikuwa hivyo, hali iliyosababisha ajiuzulu nafasi hiyo, lakini alipoamua kugombea Ubunge alipata.
“Hamnitendei haki, nimesikitishwa na taarifa hiyo yenye nia ya kufanya nitoke kwenye ubunge, ila namshukuru Mwenyezi Mungu sina sauti ninaposhambuliwa na kundi la watu,” alisema Mbunge huyo. Alisema hawezi kubadilisha makusudio na nia ya watu, ambao wamekuwa wakimuandama mara kwa mara.
“Safari hii sijiuzulu, kuna watu wanaota Ubunge humu,” alisema.
Akisoma taarifa ya tume hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhakiki Fedha za Mfuko wa Jimbo,Julius Chitojo alisema baraza la madiwani lililoketi Oktoba 31, mwaka jana, lilipokea hoja binafsi kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Mfuko wa Jimbo.
mbuge
Alisema baraza liliazimia kuunda kamati ya watu wanne ili kufuatilia na kubaini ukweli wa hoja, zilizotolewa na Diwani wa Lamaiti, Donald Mejitii kuwa mbunge huyo alifanya ubadhirifu wa fedha zilizotolewa kwa vikundi, ununuzi na usambazaji wa majembe ya kukokotwa na ng’ombe hasa katika kipindi cha kuanzia Agosti mwaka jana.
Pia alisema michango ya fedha za wananchi wa kijiji cha Chibelela kwa ajili ya kusafisha kisima cha maji zilichukuliwa na mbunge huyo, lakini hazikutumika kwa kazi iliyopangwa.
Mwenyekiti huyo alisema kikao cha kamati ya maendeleo ya Mfuko wa Jimbo, kilichofanyika Aprili 30, mwaka jana kiliidhinisha Sh milioni 17 kwa ajili ya ununuzi wa majembe 117 na Sh milioni 3.2 kwa ajili ya usafirishaji wa majembe hadi kwa walengwa.
Hata hivyo, alisema hadi kufikia Oktoba 30, mwaka jana, majembe yaliyosambazwa yalikuwa ni 85 yenye thamani ya Sh milioni 14.5, kati ya hayo majembe 78 yaliuzwa kwa Sh 110,000 kila moja sawa na Sh milioni 8.5.
Taarifa hiyo ilisema fedha nyingine za uuzaji wa majembe hayo, zilikuwa zikikusanywa na Msaidizi wa Mbunge huyo, Saidi Kayumbo ambaye baada ya kuhojiwa na kamati, alisema fedha hizo alikuwa akipeleka kwa mbunge huyo, badala ya fedha hizo kupelekwa halmashauri.
Pia, mbunge huyo alikuwa akivitaka vikundi kutumia akaunti ya Jumuiya ya Akiba na Maendeleo Bahi (BASATA) ili fedha zao za maendeleo ya ziingie humo, licha ya kuwa vikundi husika, vilikuwa na akaunti za benki.
Alisema kutokana na kubaini hayo, baraza lichukue hatua stahiki kwa mbunge huyo pamoja na kurejesha fedha zote alizochukua, ambazo zilitengwa kwa shughuli za maendeleo.
Diwani wa Lamaiti, Donald Mejitii alidai mbunge huyo alikuwa akitumia gari lake kusambaza pembejeo hizo huku akiwadai wananchi fedha za usafiri.

February 09, 2014

HII NDIO VIDEO YA SHAKIRA NA RIHANNA INAYOCHOCHEA USAGAJI

 
Video ya wimbo wa Shakira ‘Cant Remember to Forget You’ aliyompa shavu mwimbaji mwenzake wa Caribbean, Rihanna imekosolewa vikali na mwanasiasa mmoja nchini Colombia anayefahamika kwa jina la Marco Fidel Ramirez, akidai kuwa kinyume cha maadili na hivyo kuwaharibu watoto wadogo.
Marco Fidel, ameiomba serikali ya Colombia kuipiga marufuku video hiyo ama vipande vya video hiyo ambavyo amedai kuwa vinasapoti usagaji, uvutaji sigara na mauaji.  
“Our Shakira with her erotic video is promoting tobacco usage and has become the wost example for our youth.” Alitweet mwanasiasa huyo kutoka Bogota, Colombia.
“Shakira’s new video is a shameless case for lesb**nism and immorality. It is a danger to children. It sends a provocative message to weak people who can be polluted and inducet to practice lesbian**m.” Aliongeza katika tweet nyingine.
Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akijiita mlinzi wa kanuni na thamani, aliwahi pia kuzikosoa baadhi ya video nchini humo kwa madai ya kutofuata maadili.