BAADA ya mwanamuziki Baby Joseph Madaha kunaswa na mtego wa kujiuza aliotegewa hivi karibuni, bidada huyo anaonekana kubadilika na anadai mgogoro uliojitokeza kati yake na meneja wake, Joe Kairuki kutokana na tukio hilo umekwisha.
“Kweli nimejifunza kutokana na makosa maana kunaswa kwenye ule mtego kumenigharimu sana lakini nashukuru nimesamehewa na mkataba ninaendelea nao, yale yamepita na sasa ni kazi tu,” alisema Baby Madaha a.k.a The Queenof Swaga.