Pages

February 25, 2014

Ajinyonga baada ya Rafiki yake Kuuawa.

Ajinyonga

Ajinyonga baada ya Rafiki yake Kuuawa.

Mtu mmoja amejinyonga mpaka kufa baada ya rafiki yake kipenzi kufariki dunia kwa kile kilichoelezwa kupigwa na walinzi wa Mgodi wa North Mara.
Mwita Nyansinge alifariki dunia usiku wa Februari 23 mwaka huu kwa kujinyonga na kamba baada ya rafiki yake aliyetajwa kwa jina la Chacha Mgima (30), mkazi wa Kijiji cha Kewanja Kata ya Matongo wilayani Tarime kudaiwa kuuawa Februari 19 mwaka huu.
Mgima aliuawa kwa kipigo kutoka walinzi wa mgodi huo akituhumiwa kuingia ndani bila ruhusa.
Kwa mjibu wa chanzo chetu, inadaiwa kuwa baada ya Nyangige kupata taarifa za kifo cha rafiki yake, alihuzunika na kujitenga na watu kabla ya kujinyonga.
Chanzo hicho kilieleza kuwa marehemu Marwa alikamatwa na walinzi wa mgodi huo Februari 19 usiku akitafuta mchanga wa dhahabu na baada ya saa chache siku iliyofuata Februari 20 alipelekwa Kituo cha Afya cha Sungusungu Nyamongo akiwa hajitambui.
Hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa katika Hospitali ya KKKT Shirati, ambako alifariki dunia.
Kutokana utata wa kifo cha marehemu, familia yake inadaiwa kukataa kuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi kwa madai ya kutaka uchunguzi ufanyike kwanza.
Ajinyonga
“Tunahitaji kufahamu kwa kina kilichompata ndugu yetu, alikamatwa akiwa hai lakini baadaye tulipokuja kumuona alikuwa hajitambui kutokana na kipigo,” alisema mmoja kati ya ndugu wa marehemu.
Mpaka tunakwenda mitamboni juhudi za kumpata msemaji wa polisi zilishindikana.