Pages

February 23, 2014

“Maisha yangu ni ya Kula Kulala”…Mzee Gurumo

gurumo

Mzee Gurumo.

MWANAMUZIKI ambaye kwa sasa amestaafu kuimba kwa sasa, Muhiddin Maalim Gurumo(Mzee Gurumo) amesema kuwa, tangu atangaze kuacha rasmi shughuli za muziki maisha yake ya sasa ni kula kulala kwani hana shughuli yoyote anayofanya.

Maisha Yake kwa Sasa.

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, maisha yake ya sasa ni kusubiri giza liingie na jua liwake mkono uende kinywani kwa kuwa hana biashara yoyote anayoiendesha ya kuweza kumpatia ridhiki, mara nyingi huwa anajipumzisha kwenye baa ya Amana akiifariji nafsi yake.Mzee Gurumo
Mzee Gurumo akiwa amepozi Amana Bar.

“Makazi yangu makubwa mimi ni kwenye baa ya Amana hapa sinywi pombe wala sivuti bangi napoteza muda saa ya kula ikifika nakula ya kulala nalala sitaki kujichosha uzeeni, wapo wengi tu wanaonitunza kuhakikisha sipati tabu kifedha,”alisema Mzee Gurumo.
CREDIT: GPL