Pages

Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

March 07, 2014

BABA KANUMBA: NITAMPELEKA MAMA KANUMBA SEGEREA

http://api.ning.com/files/BrAPCEwtvYDNlrlYwAb0FlxzgXMaaorbIDZlHTjKWPHV0Xvq1g*W6OqvzSs2cy2sJ7XYhr8r1y1mE5svyJwDilEhD38B*TMe/BabaKanumba2.jpg?width=640
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba anaonekana kuendelea kuwewesekea mali za mwanaye baada ya kuibuka na kudai kuwa, atampeleka Segerea (jela) mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kwa madai kuwa amezifuja mali za marehemu.
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kwa njia ya simu, baba Kanumba alisema, ameona taarifa kwenye gazeti kuwa mali nyingi za marehemu Kanumba zimeuzwa huku yeye akiwa hajaambulia chochote.
“Huyu mama Kanumba ana laana yangu, amefuja mali za mwanangu kwa kushirikiana na Seth, mimi sijashirikishwa, nisipopata chochote tutafikishana pabaya,” alisema mzee huyo.
Baba wa marehemu Kanumba, Charles Kanumba.
Kuhusiana na hilo, mama Kanumba huyu hapa: “Kwa mila za Kisukuma Kanumba siyo mwanaye kwa kuwa hajanioa, hivyo kuhusu suala la mali kama anazijua zinazomhusu aonyeshe moja baada ya nyingine hapo itakuwa sawa.”

MAIMARTHA ATIWA MBARONI, KISA....!

http://api.ning.com/files/8zXnpLXRQW*WYyyeVLC26vD-Xfv1PinufUy7VKkdxJF9F0s*uKrs2MFKZLpWvAgLOO4duNZvqQrKDx5curmpIEYKGynnLMGQ/Maimartha.jpg


Mtangazaji maarufu wa Runinga Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiwekwa nyuma ya nondo kwa madai ya kumtapeli dada mmoja aliyetambulika kwa jina la Zai, mkazi wa Zanzibar.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, mtangazaji huyo alilipwa pesa ya kianzio cha shughuli ya u-MC visiwani humo mwezi mmoja uliopita lakini akashindwa kwenda bila sababu za msingi.
“Kifupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya siku ya tukio kupita na Maimartha kuingia mitini, chanzo hicho kilisema Machi 4, mwaka huu, Zai alimfungia safari hadi Dar na kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kumalizana.
Alipotafutwa Maimartha kuzungumzia juu ya sakata hilo, alitiririka: “Imeniuma sana, kiukweli alinipa fedha za kianzio huyo dada (Zai) lakini nilishindwa kwa sababu nilipata dharura, hata hivyo nimeshangaa amekwenda kupandisha dau kule polisi tofauti na fedha ndogo aliyonipa, sitaki kuongelea sana lakini nashukuru yameisha.”

DIAMOND: NAJUTA KUWA STAA

Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Exclusive Interview! Staa anayeuza zaidi kwa sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefungukia skendo ambazo zimekuwa zikimtafuna kila kukicha huku akieleza kuwa, sasa anajuta kuwa staa.


Akizungumza na paparazzi wetu katika mahojiano maalum wiki hii, Diamond alisema kuwa amekuwa akivumilia mengi ambayo yanaelekezwa kwake lakini sasa imefika wakati yanamuumiza kwani naye ni binadamu, ana moyo wa nyama na siyo chuma.
Penny.
Ni kweli unatumia ndumba kutafuta mafanikio?
Diamond: “Baadhi ya watu wanakuwa na imani hizo kuwa mimi natumia mambo ya kishirikina kutafuta mafanikio lakini kwa wasiojua ni kwamba kila nifanyalo namtegemea Mungu na muongozo wa mama yangu mzazi (Sanura Kassim a.k.a Sandra).

“Hao ukijumlisha na jitihada zangu mwenyewe na kujituma sana ndiyo wanaonifanya niwe hapa nilipo leo.
“Si kwa sababu ya mambo ya kishirikina. Kwanza siamini katika ushirikina.”
Wema.
Hili la mama Wema Sepetu kudai umemloga Wema likoje?
“Sijawahi kumsikia mama Wema akisema nimemloga Wema na hata kwenye magazeti sijaona ila siku nikimsikia ndiyo naweza kusema chochote juu ya hilo.”

Unazungumziaje madai ya wizi wa nyimbo za wasanii wenzako?
Diamond: “Kwa hatua niliyofikia mimi si mtu wa kuiba wimbo wa mtu, bali wapo baadhi ya watu wanaopenda kunisukumia skendo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

“Wakati mwingine wanaotuponza ni maprodyuza ambao huenda siku za nyuma walitengeneza biti kali kwa ajili ya msanii fulani, msanii huyo akaingia mitini.
Jokate.
“Siku unakwenda studio kwake anakusikilizisha biti hiyo na ukiiona kali anakuambia uilipie utengeneze ngoma.
“Baadaye ndiyo unasikia msanii mwingine anaibuka na kusema kaibiwa biti au wimbo. Sasa hapo kosa ni la nani?

Kwa nini una msururu wa mademu?
Diamond: “Mimi ni Sukari ya Warembo na ni kweli baadhi nilikuwa nao kwenye uhusiano lakini wengine ni maneno ya watu tu, sijawahi kutoka nao.

“Kuna ambao wanajitafutia umaarufu kupitia kwangu kwa kusema nimetembea nao lakini siyo kweli. Si unajua ukizungukwa na uaridi na wewe unanukia uaridi? Ndivyo hivyo, wapo baadhi wanajitangazia tu ili wapate umaarufu.”
http://api.ning.com/files/lHZphyruYBmuTkGYhwKk0vclpSoZ3gL7eQFFZsz-kesjUnFLWfEkx27*wFJElo8Sv5drP2jqhSZDIYQdZE27ZJX-M3jLNASE/peteyafreemasons.jpg
Baadhi ya warembo ambao tayari ameshaelezwa kutoka nao kimapenzi ni pamoja na Rehema Fabian, Pendo Maisha Plus, Jacqueline Wolper, Natasha, Najma Shaa, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Unazungumziaje U-freemason wako?
Diamond: “Mimi siamini juu ya imani hiyo kabisa na sijui kama ipo. Huenda mavazi wakati mwingine yanafanya watu wanahisi hivyo. Kama ni mafanikio niliyonayo, yanatokana na kazi zangu za muziki ambazo kila mmoja anaona.

“Naweza kusema napata shoo nyingi ambazo nalipwa pesa nyingi na mimi situmii pesa yangu kwa anasa. Nawekeza ili baadaye mali zinisaidie nitakaposhuka kimuziki. Huwezi kuwa juu muda wote hivyo ni lazima niwe na tahadhari.”
Ni kweli unawapa mademu mimba kisha kuwatosa hivyo wanachoropoa?
Diamond: “Mabinti wanaoibuka na kusema nimewapa mimba ni walewale wanaotafuta umaarufu ‘kick’ kupitia mimi. Ndiyo maana kuna yule aliyeibuka na kuandikwa na magazeti lakini baadaye alikanusha mwenyewe.

“Najiheshimu na namjua Mola, najua kufanya hivyo ni sawa na kuua.”
Kwa mujibu wa Diamond, kumekuwa na baadhi ya wasanii wenzake ambao wamekuwa wakimchonganisha na mastaa wenzake, mfano ukiwa ni hivi karibuni ambapo alizushiwa kumkandia Ali Kiba ili waingie kwenye bifu.

MAINDA AKUMBUKA PETE ALIYOVISHWA NA MAX

Ruth Suka ‘Mainda’.
STAA  wa filamu  za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
 
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
“Asante Saidi kwa sababu ulionyesha kuwa una malengo makubwa na mimi mpaka  sasa ningekuwa naitwa Mrs, upendo wako kwangu bado upo sanaa ila hilo ulilolianzisha kwenye kidole changu japo ndoto haikukamilika kupitia wewe litatendeka, asanteni wote mlioshiriki siku ya hili tukio akiwemo Nina na Dotnata,” aliandika  Mainda.

March 06, 2014

SETH: KANUMBA ANANITOKEA

Joseph Shaluwa na Erick Evarist
SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo ya kushangaza, akidai kaka yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.
Marehemu Steven Kanumba.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa Kampuni ya Kanumba The Great Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 07,2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth alisema: “Kiukweli sina amani, hii hali inanitesa sana. Kila mara ananitokea ndotoni na kunieleza mambo yanayofanana.”
MAMBO GANI?
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake aliyoiacha haina mafanikio. Sasa nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia. Analalamika kwa nini filamu hazitolewi, ni jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo wangu,” alisema Seth.
Seth Bosco.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.
AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza ni kwamba, kila anaponitokea, lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa kasi na kutoka jasho jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”
MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema lazima tufanye maombi kuondoa hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha uso wa wasiwasi.

March 05, 2014

LINAH: SIPENDI KUTUMIA KONDOMU SABABU ZINAPUNGUZA LADHA YA MAPENZI

Esterlina Sanga ‘Linah’.
MSANII wa kike anayetesa kwenye Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ ametoa mpya baada ya kuibuka na kueleza wazi kuwa, awapo faragha hapendi kutumia kinga.
 
Linah alisema hayo wakati akizungumza na mwakilishi wa kona hii jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita, ambapo alisisitiza kuwa anachukia sana mipira ya kike na kiume wakati wa tendo kwa vile zinamkata stimu.

“Sema naogopa ukimwi na magonjwa mengine ndiyo maana nalazimika kutumia kwa ajili ya afya yangu lakini kiukweli kabisa, sipendi kabisa kinga,” alisema Linah.
Hivi karibuni, gazeti hili liliripoti habari ya staa huyo wa muziki kudungwa mimba na mdosi kabla ya siku chache baadaye kugundulika kuwa, kiumbe chake kilichoropoka.

WASTARA: HUYU NDIYE MSANII WA BONGO FLEVA NILIYEZAA NAYE KABLA YA SAJUKI

http://3.bp.blogspot.com/-65tYqlfukbk/UnoaxrvK4pI/AAAAAAAAB5o/7ZBljXBmxGE/s1600/WASTARA.jpg

RAY C AMUOMBA MPENZI WAKE WA ZAMANI LORD EYEZ ABADILIKE

Aliyekuwa mpenzi wa rapper Lord Eyez, mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C amezungumzia kuhusu sakata la wizi linalomkabili rapper huyo ambaye ni member wa group la Nako 2 Nako Soldiers.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Ray C amefunguka kama ifuatavyo:

MASKINI JACK HALI MBAYA, AKWAA GONJWA LA HATARI MAHABUSU NCHINI CHINA!



Jacqueline Patrick ‘Jack’.
MODO mwenye mvuto Bongo Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka, safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo.
KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.
“Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi yake,” kilisema chanzo hicho.
MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.
“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.
Jack Patrick akiwa amefunikwa uso baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni nchini China.
WAKILI WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga.
KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum.
WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’
Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.
Habari zinasema kuwa hakuna cheni yoyote kutoka kwa watu ambao wanatafsiriwa kuwa ni waliomtuma kwani wanaosumbuka ni watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu zake.
Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es Salaam.
“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.  
SABABU ZA MOYO KUSHINDWA KUSUKUMA DAMU
Juzi, gazeti hili lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ambapo alisema:
“Moyo kushindwa kusukuma damu kwa mwendo wa kawaida husababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa, mgonjwa kushindwa kudumisha udhibiti wa maji mwilini, chakula au dawa.
“Sababu nyingine ni upungufu wa damu na utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za koromeo ambazo zinaleta maumivu ya ziada kwenye misuli ya moyo, utumiaji mwingi wa vimiminika au ulaji wa chumvi uliopitiliza na utumiaji wa dawa ambazo husababisha uwekaji wa maji mwilini kama vile Hiazolidinedione.”
KUHUSU KUKOSA HAMU YA KULA
Kwa mujibu wa daktari huyo, tatizo hilo humkumba mtu anapokuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na jambo zito linalomkabili, ambalo halina mlango wa kutokea.
TUKUMBUKE
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300.
Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili.

NELLY KIM KUTUMIA MAUTUNDU YA KANUMBA

Stori: Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu za Kibongo, Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’ amesema anajivunia sana kufanya sinema nyingi na marehemu Steven Kanumba na kwamba amejipanga kufuata nyayo zake ili aweze kufanikiwa kwa kutumia kipaji chake.
Marehemu Kanumba.
Akizungumza na Stori Mix, Nelly Kim alisema: “Nafurahi kufanya kazi na marehemu Kanumba. Nimecheza naye zaidi ya sinema 20 pale kwa Mtitu Game.
Nimejifunza kujiongoza na kuamini katika mambo makubwa, ndiyo maana sasa hivi nasimama na kampuni yangu ya Kasinge Production ambayo inatayarisha na kusambaza filamu.
Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’.
“Nimesharekodi filamu ya kwanza inayoitwa The Word of God ambayo nimecheza na Kajala, Ben, Kambi na wengineo.
Unajua wasanii hatujitambui, tunakubali kunyonywa wakati tunaweza kujitutumua na kusimamia kazi zetu wenyewe. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Kanumba ambayo nataka kuitumia ili kufaidika kwenye sanaa.”

March 04, 2014

HUDDAH MONROE NDANI YA SKENDO NZITO YA KUFANYA MAPENZI HADHARANI


 Mwanadada mwenye vituko vyakutosha huddah Monroe maarufu kama lady boss hivi karibuni huenda akatupwa mahakamani baada ya kuvunja sheria na kuweka mamba ya ndani hadharani ambapo ametupia picha kwenye mtandao huku akionekana yupo na njema wanafunja amri ya sita bila hata presha wa wasi, hakiki mdada huyu huenda anamatatizo na sio bure tu :Pichazi wakifanya live zitakujia sio muda endelea kutembelea site hii

March 03, 2014

WEMA AMHARIBIA PASTOR MYAMBA

STAA wa filamu mwenye jina kubwa nchini, Wema Sepetu hivi karibuni alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.
Wema Sepetu.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo aliliambia gazeti hili kuwa, Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa haukuwa wa kweli.
Alisema kutokana na kutofika kwa staa huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi wageni wengine, wakiwemo waandishi wa habari.
Emanuel Myamba 'Pastor Muyamba'.
Mmoja wa watu wa karibu na Wema aliliambia gazeti hili kuwa muigizaji huyo hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi karibuni, kwani mara zote amekuwa akiwaeleza kila linapotokea jambo zito kama hilo.
Mtu huyo alisema katika ratiba ya siku hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja la starehe na halikuwa limebadilika.
juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo alichosema kimemsikitisha kwani walitoa mwaliko kwake kutokana na heshima aliyonayo.
“Nimemshangaa sana, lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu anajitambua na ni professional,” aliema Myamba.

AIBU: PICHA ZA HEMED NA NAJMA DATAN WAKINYONYANA MATE HADHARANI ZAVUJA NA KUSAMBAA KWA KASI MITANDAONI!


Waigizaji wa filamu nchini ambao pia ni wanamuziki wa Bongofleva Hemedy Suleiman na Najma Datan wamezua maswali kwa watu wanaofuatilia habari za mastaa wa Tanzania baada ya picha zao wakiwa kimahaba zaidi kuanza kusambaa.

 Katika picha hizo zinazoonekana hapo juu  na chini wawili hao wanabusiana kimahaba kama wapenzi walioshibana. Haijajulikana kama picha hizo ni za video mpya ya muziki, filamu au ni wapenzi kweli.

Hata hivyo tayari inajulikana kuwa Hemedy kwasasa anatoka na Zuhura Gora ambaye ni model na muigizaji pia, huku Najma akiwa ameshawahi kuwa katika penzi na Mr.Blue, Najma pia hivi karibuni alijitosa Rasmi kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood na filamu ya Fan's Death akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Rammy Galis. 

USAGAJI WAMTESA JACKILIN WOLPER



Msanii Jacqueline Wolper, amesema anaumizwa sana na tetesi zinazozagaa kama moto wa kifuu kitaani kuwa anajihusisha na vitendo vya usagaji.

Akizungumza nasi  kuhusiana na skendo hiyo, mwanadada huyo alisema, akiwa kama mwanamke anayejitambua na kumtukuza vyema Mungu wake jambo hilo limekuwa likimuumiza.
 
“Roho inaniuma sana kuhusiana na hizo taarifa sijui niongee nini ili jamii inielewe kile nitachokizungumza, ni ngumu sana kufanya hicho kitu ambacho najua hakimpendezi Mungu kivyovyote vile,” alisema Wolper.

March 02, 2014

“Mimi ni dalali wa madini”….Fid Q

Kati ya mamia ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu Tanzania, ni mwanamuziki mmoja pekee aliyehudhuria katika Tamasha la Sauti za Busara 2014, lililotajwa na Kituo cha Utangazaji cha CNN kuwa ni tamasha lenye nguvu barani Afrika.
Huyu siyo mwingine bali ni Fareed Kubanda (Fid Q), aliyekuwapo mjini Zanzibar kwa siku mbili kushuhudia tamasha hilo lililokuwa la siku nne, lililofanyika katika wiki ya pili ya Februari mwaka huu, Viwanja vya Ngome Kongwe visiwani humo.
Ikumbukwe kuwa Fid Q alianza shughuli za muziki miaka ya 1990. Alitoa wimbo wake wa kwanza mwaka 2000 ulioitwa; Huyu na Yule, alioimba na Mr Paul. Wimbo huu ulirekodiwa na Prodyuza maarufu nchini,  Master Jay katika Studio za MJ Records na kumpa heshima kubwa msanii huyo.
Starehe ilifanya mahojiano na  Fid Q ambaye pamoja na mambo mengine aliweka wazi sababu za yeye kuwapo katika tamasha hilo, kilichomvutia huku akiweka wazi kuhusu biashara ya madini aliyodaiwa kuanza kuifanya mwishoni mwa mwaka jana.
Swali: Nini kimekuvutia ukaamua kuhudhuria katika tamasha hili?
Fid Q: Mimi ni mtu ninayependa kujifunza zaidi, nimeona hili ni tamasha kubwa na zuri kwangu kujifunza. Kubwa zaidi ni kutaka kujua wenzetu wanafanyaje muziki. Huwezi kukaa tu na kwenda kupiga muziki staili moja kila siku; ili ujue, ni vyema ukajifunza kutoka kwa watu unaowaamini.
Swali: Kupitia wanamuziki wa muziki wa asili kutoka mataifa mbalimbali katika Sauti za Busara, unadhani unaweza kupata uzoefu wa kutosha?
Fid Q: Wasanii wote wa mataifa mbalimbali waliofanikiwa hasa Nigeria, wamekuwa wakichukua vionjo kutoka katika muziki wa asili, kisha wakileta katika muziki wa kizazi kipya, inapatikana ladha ya kipekee, ndiyo maana leo unawaona kina P Square wanatamba, walianza kujifunza na kutumia vionjo kutoka katika muziki wa asili.
Swali: Unadhani nini kinachowafanya wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutohudhuria tamasha hili?
Fid Q: Hawapo tayari kujifunza. Mimi nimewahi kutumbuiza katika tamasha hili, ninajua. Huku hakuna ubabaishaji, msanii unatakiwa uimbe kwa sauti yako jukwaani, walio wengi hili hawaliwezi. Idadi kubwa ya wasanii wamezoea kuimba kwa ‘playback’, (kuweka cd ya ala), ndiyo maana hata waandaaji wanashindwa kuwaalika, muziki tunaofanya sisi ni ule wa wenzetu, lakini tunashindwa kuuwakilisha ipasavyo, tumezoea kuimba kwa ‘playback’.
Swali: Unadhani kuna umuhimu gani kwa wasanii kuimba ‘live’ (kwa sauti zao wenyewe pasipo kutegemea CD)?
Fid Q: Ina faida zake. Kwanza inakutangaza na pia unaonekana wewe ni msanii halisi. Haya ndiyo wanayohitaji kuyaona watu wanaoujua muziki, watu wanaohudhuria matamasha ya kimataifa ni wengi, hawawezi kusikiliza kitu walichokisikia kwao, wanapenda kusikia kitu kipya kitakachowateka.

BONANZA LA MICHEZO DAR LIVE HAKUNAGA

Mhe. Angela Kizigha na Mhe. Faustine Ndugulile wakifanya mazoezi na klabu mwenyeji wa bonanza hilo, Magenge 20.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Mh Angella Kizigha akiongea na wanajogging wa bonanza hilo.
Mhe. Angela Kizigha akipokea zawadi kutoka kwa klabu mwenyeji ya Magenge 20.
Mhe. Faustine Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni akipozi na Mgeni Rasmi, Angela Kizigha baada ya kupewa zawadi ya kikoi.
Timu ya Magenge 20 na Classic kabla ya mtanange kuanza.
Baadhi ya washiriki wa bonanza hilo wakiwa ndani ya Dar Live.
Wanabonanza wakiwa stejini ndani ya Dar Live.
BONANZA la michezo la kila mwezi linalofanyika katika Uwanja vya Burudani wa Dar Live Mbagala Zakhem limefanyika leo ambapo maelfu ya wanamichezo wamejitokeza kushiriki bonanza hilo la aina yake.
Wenyeji wa bonanza hilo walikuwa ni klabu ya Magenge 20 ya Mbagala Kiburugwa jijini Dar, ndiyo walikuwa wakizikaribisha timu zote zilizokuwa zimepewa mwaliko wa kushiriki bonanza hilo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa ni Mheshimiwa Angela Kizigha, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki aliyekuwa ameambatana na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na wanamichezo mbalimbali.
Licha mvua kubwa kunyesha lakini haikuweza kukata kiu ya wanamichezo waliokuwa wamejitokea kwani waliendelea kuserebuka ndani ya mvua bila kujali.
Hata hivyo burudani ya kufa mtu inatarajiwa kuangushwa jioni hii na bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Farasi’ chini ya Ally Choky ‘Mzee wa Ambulance’.
Vilabu  zaidi ya 180 vya mbio za pole ‘Jogging’ vimeshiriki ambapo michezo mbalimbali bado inaendelea kufanyika.
Washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali za michezo katika bonanza hilo la kufuru, aidha Tamasha hilo limedhaminiwa na PSPF, Mpango wa Damu Salama, Global TV Online, Kampuni ya A-One watengenezaji wa maji ya Maisha, Global Publishers Ltd, Dar Live pamoja na Benki ya Akiba Commercial (ACB).

February 28, 2014

“Madawa ya Kulevya na Bangi sasa Basi”….Banza Stone

banza
  Mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
 
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV  mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa kuchanganya na sigara au bangi.
 
“Ujana ulisababisha nikajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa nimeacha kabisa na nawashauri vijana wenzangu kuwa mbali na kilevi hicho kwani kama huna kipato cha kutosha unaweza kugeuka kibaka maana mwili ukizoea ni vigumu kuacha.”
CREDIT: GPL

Jokate Aupiga Chini Ulokole.

jokate mwigelo
Picha za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa analosali kumsema kuwa anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema: “Ninachokumbuka Jokate aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili amtumikie Yesu kisawasawa lakini kwa mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole itakuwa basi tena.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo, alipopatikana alisema: “Nilizipiga kwa ajili ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo ya Kidoti.
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi sana?
Jokate: Huh!
Ijumaa: Huh nini?
Jokate: Nishasema ni za Kidoti, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele zangu.
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena?
Jokate: Kimyaaa.
Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo huyu kwamba, kwa kuwa ameshajijengea heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema akawa makini na mavazi kama haya ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa tofauti.

February 27, 2014

Mimba ya Linah Aliyopewa na Mdosi Yachoropoka…!!

mimba
SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.
mimba
Astelinah Sanga ‘Linah’.

Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.

“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.

Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.

“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.

February 26, 2014

“NASIKITISHWA NA WASANII WANAO PENDA KUTENGENEZA UGOMVI WA KILAZIMA NA MIMI”…DIAMOND

Diamond
Muda si mrefu Diamond Amefunguka haya hapa chini kuhusu wasanii wanasanii wanao tafuta beef za lazima kutoka kwake …Jisomee