Pages

February 25, 2014

Daktari FEKI Anaswa tena Muhimbili..!

Daktari Feki

Daktari Feki

Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwadaktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali
Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.
Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza.
Hospitali ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.

CHAMA CHA MADAKTARI

Chama cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa  macho na madaktari wanaojitokeza kutaka kusaidia wagonjwa.
Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni Daktari feki.
Daktari Feki
Daktari Feki

Namna alivyonaswa

Eligaeshi alidai maofisa usalama wa hospitali hiyo walipata taarifa za kuwapo kwa daktari aliyeonekana akiwahudumia wagonjwa na kwenda kumkamata.
Baada ya kutiwa mbaroni, inadaiwa alipekuliwa na kukutwa na kadi tatu za kliniki za wagonjwa wa Muhimbili, kitambulisho cha Peter Daniel mfanyakazi wa hoteli moja Dar esSalaam, vipimo vya kupimia ujauzito, namba nyingi za madaktari wa Muhimbili kwenye simu yake ya mkononi na Sh167,000. Wakati akiwa chini ya ulinzi, mmoja wa wagonjwa wake, aliyefahamika kwa jina la Hassan Madika alimpigia simu na kutakiwa kwenda sehemu aliyokuwa akihojiwa. Mtuhumiwa alikiri kupigiwa simu na Madika.

Daktari Feki Ajitetea

Kitano alisema kuwa alifika hospitalini hapo baada ya Madika kumweleza kuwa alikuwa amefanyiwa operesheni wiki iliyopita na kwamba, hawezi kusimama muda mrefu hivyo alikuwa akihitaji msaada wa mtu wa kumpelekea faili sehemu husika.
Haji alipoulizwa na waandishi wa habari, iwapo anamfahamu Kitano alisema alikiri kutomfahamu na kwamba, hajawahi kumwona.
Alisema alifika hospitalini hapo kumsaidi Madika na kwamba, tuhuma hizo zinalenga kumchafulia jina hazina ukweli.
Hata hivyo, Kitano alisema yeye siyo tapeli daktari na ameshafanya kazi hospitali mbalimbali za Serikali.
Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali ya Muhimbili kwa Daktari Feki Kukamatwa.