Pages

Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

March 06, 2014

Matukio Katika Picha Wakati Bunge Maalumu la Katiba Lilipohairishwa Leo Mjini Dodoma kutokana na Vurugu.


 Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa  kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
bunge2
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima Mdee akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa kwa muda mjini Dodoma leo kufuatia sintofahamu iliyokea
bunge4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd  (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa  muda leo kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa TanzaniaFrederick Werema.
bunge5
Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema.

CHADEMA Kumtangaza Mpinzani wa Ridhiwani Kikwete Jimbo la Chalinze.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mchakato wa kutafuta mgombea wa kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Chalinze, ambapo jana fomu za kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho zilianza kutolewa.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishaanza mchakato wa kutafutia mgombea wa kuwania nafasi hiyo, ambapo Ridhiwani Kikwete, alishinda kura ya maoni ya wanachama wa chama hicho na sasa anasubiri uamuzi ya vikao vya juu vya chama hicho.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Uhusiano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema fomu hizo zinatolewa na kurejeshwa katika ofisi za Kanda ya Pwani ya chama hicho.
“Baada ya kurejesha fomu, walioomba kuwania nafasi hizo watapigiwa kura ya maoni na wanachama wa Chadema wa eneo husika, na baada ya hapo uamuzi wa mwisho utakuwa ni wa vikao vya juu,” alisema Makene.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Uenezi wa Halmashauri ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, alisema bado chama hicho kipo kwenye mchakato wa kuandaa vikao vya juu, vitakavyoyachuja majina ya waliopigiwa kura za maoni na kuteua mgombea wa ubunge kupitia chama hicho.
“Tarehe rasmi ya vikao hivi vya juu bado haijapangwa, ndio tuko kwenye mchakato tukikamilisha tutawajulisha,” alisema Nape.
Juzi Ridhiwani alishinda kura ya maoni ya kumpata mgombea wa CCM katika jimbo hilo baada ya kupata kura 758, akifuatiwa na Shaban Madega aliyepata kura 335, Athuman Maneno kura 206 na Changwa Mkwazu aliyepata kura 12.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo la Chalinze, unatarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu na Machi 12, vyama vya siasa vitawasilisha majina ya wagombea wake kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao.
Kampeni rasmi za uchaguzi huo zitaanza Machi 13, mwaka huu. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo kufariki dunia.

February 27, 2014

NAPE ATUA SHINYANGA KUWATAMBULISHA MADIWANI WALIOTEMA CHADEMA NA KUJIUNGA CCM.

CDM
Kutoka kushoto ni Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masekelo(Chadema) na Kulia ni Sebastian Peter aliyekuwa diwani kata ya Ingokole(Chadema) wakitambulishwa mbele ya umati wa watu na Katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini ambao kwa moyo mmoja wamejiunga na CCM.

February 26, 2014

Slaa adai kuwa Kiongozi anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi …..Asema hata wakibaki watatu, chama HAKITAKUFA

slaa

Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama.
 
Alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMAjimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi huku akisisitiza kuwa   hata  wakibaki  watatu  tu  ndani  ya  chama, Chadema  haitakufa  na  kwamba  wameridhia kujiuzulu kwa madiwani wao wawili mkoani Shinyanga.
slaa
Dk. Slaa
 
Alisema kujiuzulu kwao ni mpango maalumu uliotengenezwa na wapinzani wao kisiasa kwa lengo la kuwadhoofisha na kuwavuruga.

February 25, 2014

Madiwani CHADEMA Wahamia CCM.

chadema
Madiwani wawili wa Chadema kutoka Kata ya Ngokolo, Sebastian Peter na wa Kata ya Masekelo, Zacharia Mfuko zilizopo Shinyanga Mjini wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amekituhumu CCM kwa mchezo mchafu.

Awali CCM inadaiwa kuanza mkakati wa kuwachukua waliokuwa viongozi wa chama hicho waliofukuzwa uanachama hivi karibuni wilayani Kahama kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.

Katika mikakati hiyo, juzi kiongozi wa juu wa Umoja wa Vijana Taifa (jina tunalo), aliingia mjini Kahama kimyakimya na kufanya mkutano wa siri na waliokuwa viongozi hao.
Chanzo cha habari kilidai kuwa kiongozi huyo baada ya kufika mjini Kahama akitokea Dodoma alifikia hoteli mojawapo mjini Kahama kwa siri na kualika baadhi ya makada wachache wa CCM ambao aliwapa masharti ya kutotoa taarifa yoyote juu ya ujio wake Kahama.

Viongozi hao waliofukuzwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Majengo, Bobson Wambura, Mwenyekiti wa Jimbo la Kahama, Israel Barakiel, Katibu wa jimbo hilo, Vicent Kwilukilwa, Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo, Benedicto Shija, Mwenyekiti Bawacha Jimbo, Kasigwa Adram pamoja na Mratibu wa Vijana Wilaya, Vicent Manyambo.

Hata hivyo, Dk Slaa akihutubia mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Chadema, Grace Tendega alisema anatoa ruksa kwa wabunge na madiwani wasiopenda kutumikia wananchi kuondoka Chadema.
CREDIT: MWANANCHI

February 24, 2014

Mugabe Aikosoa Afrika kwa Kukosa Shukrani kwa Nyerere.

 Nyerere

Mugabe

Rais wa ZimbabweRobert Mugabe amesema kushindwa kwa viongozi wa Afrika kumuenzi Rais wa kwanza wa TanzaniaMwalimu Julius Nyerere kwa mchango wake katika ukombozi wa Afrika ni jambo la kufedhehesha.

Mugabe
Rais Robert Mugabe
Kiongozi huyo mwenye miaka 90, alikuwa akiongea kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Jumapilii hii nchini Zimbabwe muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Singaporealikoenda kufanyiwa upasuaji wa macho. Alisema viongozi wa Afrika wanapaswa kufanya zaidi kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere aliyeifanya Tanzania kimbilio la vuguvugu la ukombozi barani. Nyerere alikuwa na mchango mkubwa kwa kukamata madaraka kwa Mugabe.
Mwalimu Nyerere enzi za Uhai wake
Mwalimu Nyerere enzi za Uhai wake
Maelfu wa wananchi wa Zimbabwe walijitokeza kwenye uwanja wa Marondera kwenye sherehe hiyo inayodaiwa kugharimu dola milioni 1 za Kimarekani

Mugabe Aelezea Heshima anayonyimwa Nyerere.

“Nataka kusema, wakati ambapo heshima zimekuwa zikimwagwa kwa mashujaa wa Afrika, mtu anayeonewa ni Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Mugabe. “Hapa tulipo, vuguvugu za ukombozi, kule tulikokuwepo – tulitegemea msaada wa Tanzania. Lakini hakuna kinachosemwa kuhusu mtu huyu na nchi yake kwenye Jumuiya ya Afrika.”
Mugabe ambaye ni makamu mwenyekiti wa AU, alisema bara la Afrika linapaswa kukumbushwa fadhila inazotakiwa kumlipa Mwalimu Nyerere.
“Nataka sisi Wazimbabwe, kusimama kwaajili ya Nyerere. Afrika inatakiwa kukumbushwa wajibu iliomtupia mtu huyu, mzigo wa kuendesha vuguvugu zote za ukombozi,” alisema. “Mwisho wa siku, hakuna hata mmoja anayesema Tanzania ilistahili japo kutajwa tu kwa kufanikisha mission hii, mission ya kuwa nasi kama marafiki, mission ya kutufanya tuendeshe vuguvugu za ukombozi wa Afrika. Wote tulienda kwa njia tofauti, kwa sura tofauti hadi Tanzania kukomboa nchi zetu na hatujaenda tena Tanzania. Well, naenda kuwa mwenyekiti wa AU, ntashughulikia suala hili,” alisema.
“Hakuna aliyetambua kile Nyerere alichokifanya. Sisi wa Wazimbabwe sio wachoyo wa shukrani, ni taifa lenye shukrani na tutamuenzi mtu huyu.”

February 20, 2014

Alichokisema Zitto mara baada ya Wajumbe wa Bunge la Katiba Kudai Nyongeza ya Posho na kudai kuwa Tshs. 300,000/= kwa Siku Haiwatoshi.

Ishu ya posho za bunge la katiba ndiyo inayoongelewa sana hivi sasa ambapo pamoja na headlines zote za Wabunge, haya ni mawazo ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuhusu hii posho.
zito
“Naomba niseme wazi kabisa kwamba, sitapokea nyongeza yeyote ya posho hata ikiongezwa. Inaweza isisaidie kuzuia walafi wengine kupata posho kubwa lakini ni bora kuhesabika kwamba nimesema hapana. Ifikie wakati tuseme hapana kwa excesses zisizo na maana. Ninamwomba Rais asikubali kuongeza posho kama baadhi ya wajumbe wa BM wanavyotaka. Wanachopata kinawatosha sana. Nawasihi wananchi mumwombe na ikibidi kumshinikiza Rais kukataa.”

Screen Shot 2014-02-20 at 11.43.10 AM

February 19, 2014

Dijitali yatawala Bungeni kudhibiti ulopokaji Bunge la Katiba..!

bunge1
BUNGE Maalumu la Katiba, limeanza chini ya mfumo wa kidijitali ambao pamoja na masuala mengine, vipaza sauti vyote viko chini ya udhibiti wa Mwenyekiti hali ambayo haitaruhusu mbunge kuvitumia bila ridhaa ya kiti.
Hayo yalifahamika jana bungeni mjini hapa, wakati Sekretarieti ikitoa maelekezo kwa wajumbe kuhusu ukaaji na jiografia ya ukumbi.
Aidha wajumbe wamehakikishiwa kuwepo usalama wa kutosha huku wakiambiwa wakubaliane na upekuzi wa hali ya juu unaofanyika kutokana na mazingira ya sasa ambayo suala la usalama ni tata.
Chini ya usimamizi wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad, ilielezwa, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu sasa anao uwezo wa kuzima kipazasauti za mjumbe akiwa mezani kwake.
“Sauti ya kaa chini ikisikika, ukitaka kuendelea kuzungumza, sauti haitasikika,” alisema Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari (IT), Didas Wambura.
Kutokana na mfumo huo, kipaza sauti cha kwanza kikishawashwa, kinaonesha rangi nyekundu.
Wengine wakiwasha, wanaoneshwa rangi ya kijani kuashiria kwamba wasubiri. Viashiria hivyo vinakuwa kwenye kiti ambaye anavitumia kuruhusu wazungumzaji.
Mfumo utaweza? Hata hivyo muda mfupi baada ya wataalamu kuwasilisha maelekezo, walipopewa muda wa kuuliza maswali au kupata ufafanuzi, walijitokeza wajumbe wengi waliotaka kuzungumza ambao baadhi, baada ya kudhibitiwa na mfumo, walipaza sauti bila kutumia vipaza sauti wakitaka wapewe nafasi.
Wakati huo huo Wambura alisema kila mjumbe ana kadi inayomwezesha siyo tu kufungulia mlango, bali kutumia katika kuzungumza kupitia vipaza sauti hivyo na pia inamwezesha kupiga kura.
Kaimu Mkuu wa Usalama wa Bunge, Peter Magati alisema wameongeza vituo vya upekuzi na akaomba wajumbe wakubaliane na hali hiyo.
“Mazingira ya sasa hivi ya hali tata ya usalama ndiyo sababu ya upekuzi wa namna hii,” alisema.
Aliendelea kusema, “tumejiandaa kuhakikisha mnakaa kwa amani na utulivu ndani na nje ya Bunge.” Kuhusu wageni, alisema watakuja kwa taarifa na akataka wajumbe kuhakikisha wageni wao wanakuwa katika mavazi ya staha yasiyo na walakini. Masuala mengine waliyohakikishiwa wajumbe, ni umeme kutokatika.
Sanjari na hilo, Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dk Jabir Bakar alisema pia ipo Wavuti ya Bunge Maalumu itakayokuwa ikirusha shughuli zote za Bunge moja kwa moja sanjari na Televisheni ya Taifa (TBC).
Huduma za matibabu zinapatikana katika hospitali iliyoko bungeni na ikitokea matibabu yakashindikana, mjumbe anaruhusiwa kwenda hospitali nyingine ya Serikali au binafsi kwa ushauri wa daktari na gharama za matibabu zitarudishwa.
Aidha wajumbe wamepewa orodha ya hoteli huku wakiaswa kutokwenda maeneo yanayohatarisha maisha yao.
Posho Taarifa ya Mhasibu Mkuu wa Bunge ilieleza kwamba licha ya wajumbe kulipwa posho ya kujikimu kila siku huku posho maalumu ikilipwa kwa wiki, vile vile wenye wasaidizi watalipwa posho ya kujikimu.
Malipo mengine wanayopewa wajumbe ni gharama za usafiri ambazo zitarejeshwa baada ya mhusika kuwasilisha tiketi ya usafiri aliotumia. Pia upo utaratibu wa kurudisha mafuta kwa waliotumia usafiri binafsi.
Wajumbe wenye watoto wachanga wameambiwa wawasiliane na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kwa ajili ya kupewa utaratibu juu ya eneo la kutolea huduma.
Ukaaji ndani ya ukumbi huo wenye viti 676, umezingatia majina, wenye mahitaji maalumu hususani wenye ulemavu na pia wenye mahitaji maalumu ya kiusalama kama vile Waziri Mkuu.
Wajumbe Baada ya maelekezo kutolewa ukumbini, baadhi ya wajumbe walilalamikia masuala mbalimbali, wakiwemo wenye ulemavu waliotaka mazingira rafiki kwao ikiwemo kuwepo wakalimani kwenye televisheni.
Vile vile suala la usawa wa jinsia katika uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake, lilijitokeza kutoka miongoni mwa wajumbe. Mjumbe wa kwanza kusimama alikuwa Tundu Lissu, ambaye alitaka ufafanuzi kutokana na kile alichosema baadhi ya nyaraka muhimu hazimo kwenye makabrasha.
Mwingine, Mussa Ali Kombo, alilalamikia posho akisema wapo waliofika Februari 16 mwaka huu lakini hawakujisajili jambo ambalo limewanyima posho ya kujikimu. Alitaka wafikiriwe kupatiwa posho hiyo.
Ernest Kimaya alitaka kufahamu iwapo wenye ulemavu watapatiwa maandishi makubwa. Kwa upande wake, Amon Mpanju alihoji kama kutakuwepo wakalimani wa lugha za alama ili watu walio kundi hilo wafuatilie yanayojadiliwa kwenye Bunge.
Naye Julius Mtatiro alihoji kuhusu stahiki za wajumbe akitaka posho maalumu wanayopewa, viwango vitajwe waelewe. Kwa upande wake, Kangi Lugora alitaka wagawiwe mapema rasimu ya Kanuni za Bunge hilo.
“Iko tabia ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia…tugawiwe haraka. Lazima tuwe na muda wa kutosha. Mpaka kieleweke mimi sitoki bila kuwa na kanuni,” alisema.
Hata hivyo Katibu wa Bunge, Dk Kashililah alisema suala la kanuni inabidi kusubiri apatikane Mwenyekiti wa Muda ambaye ndiye mwenye jukumu la kuandaa kanuni. Akizungumzia usawa wa kijinsia katika kupata Mwenyekiti na Makamu wake, Kashililah alisema uchaguzi huo ni suala la kisheria.
“Mnatubebesha mzigo tu, naliacha kwa mtaalamu,” aliwaambia wajumbe. Kuhusu maandishi makubwa na wakalimani kwa wenye ulemavu, Katibu wa Bunge alisema huduma hizo zitapatikana mkutano utakapoanza.
Aidha kuhusu hoja ya Lissu, Kashililah alikubaliana naye na akasema nyaraka zinaendelea kuchapishwa na kabla ya kuanza kupitia rasimu ya katiba, zitakuwa zimepatikana. Akijibu aliyelalamikia posho, Kashililah alisema ambao hawakulipwa posho ya kujikimu lakini walifika Dodoma Februari 16 wawasilishe uthibitisho.
Source: Habarileo

February 18, 2014

Mbatia, Mbowe Wageuka Mbogo kuhusu Kauli ya Rais Kikwete..!!

mbatia
Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM, kuondokana na unyonge, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni ya vitisho.

Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala alisema: “Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una kikomo chake.”

Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi huku ikishindana na wagomvi: “…Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya siasa,” alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa.

Alisema amechoshwa na vitendo vya ugomvi huku akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoani Shinyanga ambako kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi na mwingine kumwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete akisema: “Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu kuwa watulivu na kuchukua tahadhari kubwa.”

“Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chadema kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha kwamba hakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga,” alisema.

Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCM kumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga. Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha, hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.

Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, Grace Tengega.

Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi Mkuu ambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake.
mbatia“Anapotoa kauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu, bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayoweza kuamsha hisia,” alisema Mbowe.

Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea chama chake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote, zinawafanya wananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama.

“Rais Kikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa tindikali na mwingine kutolewa macho kwa bisibisi, lakini hazungumzii viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwamba kuna vyombo vya dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo.”

Godbless Lema anusurika kukamatwa na jeshi la Polisi kutokana na WARAKA wake unaomhusu Rais Kikwete aliouposti kwenye mtandao wa kijamii


Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.
 
Akizungumza na gazeti  la  Mwananchi  jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu ya polisi.
 
Lema alisema maafisa hao, ambao walikuwa wanatumia gari dogo, baada ya kufika hotelini hapo, waliomba aitwe na aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi makao makuu ya polisi kwa mahojiano.
 
“Niliwauliza nikaandike maelezo juu ya nini, walijibu kifupi wao ni chombo cha dola na walisema wametumwa na viongozi wa juu wa polisi na hawakuwa tayari kutaja tuhuma zangu,” alisema Lema.
 
Alisema baada ya polisi hao kusisitiza kutaka kumchukua, aliwaomba aende chumbani kujiandaa kabla ya kuwasiliana na viongozi wa chama chake na familia yake.
 
“Niliposhuka chini sikuwakuta na ndipo nikashauriana na viongozi wa chama hicho na kuamua kuondoka jana mchana Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
 

Hata hivyo, alisema Chadema leo wanatarajia kutoa tamko juu ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wanachama wa CCM kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani hasa pale wanapodaiwa kupigwa.

Mwananchi:

February 16, 2014

Kigogo wa CCM Ataja Siri Mpya ya Wauzaji Dawa za Kulevya.

MBUNGE wa Kigamboni, Faustine Ndungulile ameanika siri na aina mpya ya wauzaji wa dawa za kulevya wanayoitumia katika kupanua wigo wa watumiaji wa madawa ya kulevya Duniani kupitia watoto wadogo. Ndungulile aliyasema hayo wakati akifungua Baraza la Vijana la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kupitia wilaya ya Temeke uliofanyika katika ukumbi wa Malaika, ambapo alibainisha bayana wauzaji wa madawa ya kulevya wamekuja na mtindo mpya wa kuwafundisha watoto wadogo kutumia madawa ya kulevya kupitia kwenye vyakula wanavyopewa wakiwa shuleni pamoja na kwenye pipi ambazo watoto hao wanapozilamba taratibu huanza kujifunza kutumia dawa za kulevya na hata siku za usoni inawawia vigumu kuacha matumizi ya dawa hizo.
“Wauzaji wa madawa ya kulevya ni watu hatari sana kwani siku hizi wameanzisha mtindo wa kuwachanganyia watoto wadogo kwenye vyakula pamoja na kuyapaka madawa hayo ya kulevya kwenye pipi ambazo watoto hao wanapozilamba huanza kujifunza matumizi ya madawa ya kulevya tangu wakiwa watoto na ni ngumu kuchomoka katika mtego wa matumizi ya madawa hayo katika maisha yao”, alisema Ndugulile.
Kama haitoshi Ndungulile alianika bayana matatizo makubwa yanayowasibu vijana kwa sasa kuwa ni madawa ya kulevya pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo alibainisha waziwazi kuwa nguvu kazi ya taifa la leo imekuwa rehani kupitia mitego hiyo. Mbunge huyo wa Kigamboni ambaye kitaaluma ni Daktari aliweka waziwazi kuwa licha ya takwimu za kushuka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kushuka kutoka asilimia 7 mpaka asilimia 5.1 bado tatizo ni kubwa kupita maelezo kwa vijana nchini.
sembe
“Kati ya vijana wa kike watatu wanaotumia madawa ya kulevya, wawili kati yao ambao ni asilimia 67 wameathirika na virusi vya ukimwi. Halikadhalika kwa upande wa vijana wa kiume wawili wanaotumia madawa ya kulevya, mmojawao ambaye ni asilimia 50 ana maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hali ni mbaya sana kwa vijana.” Alisema Ndungulile.
Mbunge huyo wa Kigamboni aliwaasa wajumbe hao wa Baraza la UVCCM (W) Temeke na vijana wote nchini kuwa mbali na matumizi ya madawa ya kulevya na badala yake wajibiidishe zaidi katika kufanya mambo yenye faida kwao kupitia shughuli za kiuchumi kwa kuchangamkia fursa zilizopo.
 Mjumbe wa Baraza la UVCCM, Ndugu Emmanuel John akichukua karatasi ya kupigia kura.
Wakati huo huo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya Temeke wamefanya uchaguzi wa majimbo yaliyopo ndani ya Wilaya hiyo na kupata Wenyeviti na Makatibu wapya wa majimbo. Baraza hilo la Vijana ambalo lilifunguliwa na Mgeni rasmi Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndungulile ambaye wakati wa ufunguzi aliwaasa vijana kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya na kujikinga zaidi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani hali iliyopo inatisha sana kwa vijana.
“Kati ya vijana wa kike watatu wanaotumia madawa ya kulevya, wawili kati yao ambao ni asilimia 67 wameathirika na virusi vya ukimwi. Halikadhalika kwa upande wa vijana wa kiume wawili wanaotumia madawa ya kulevya, mmojawao ambaye ni asilimia 50 ana maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hali ni mbaya sana kwa vijana.” Alisema Ndungulile.
Ndugu Ndungulile ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Temeke aliwaasa na kuwatia moyo vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa  na uchaguzi mkuu hapo mwakani naye kwa nguvu zake zote atapambana katika kuwatetea vijana wenye sifa stahiki kwani anaamini vijana ni nguvu kazi ya sasa ya Taifa.
Ndugu Ndugulile aliwaasa na kuwatakia uchaguzi mwema wajumbe wa Baraza hao wachague viongozi wenye sifa wanaowataka kwani yeye kama Ndugulile ameanika wazi kuwa hajashiriki kupanga safu za viongozi badala yake jukumu hilo limeangukia mikononi mwa wajumbe.
Kwenye baraza hilo la Vijana ambalo lilikuwa ni baraza la kazi wamechagua viongozi wa majimbo ya Kigamboni na Temeke yanayopatikana ndani ya Wilaya ya Temeke. Kwa upande wa Temeke waliojitokeza kuomba nafasi ya Uenyekiti ni Arnord Sangawe aliyepata kura 48, Julius Mkada aliyepata kura 24 na Peter Sillo aliyepata kura 4. Mshindi wa nafasi ya Uenyekiti wa Jimbo la Temeke UVCCM ulinyakuliwa na Arnord Sangawe. Waliojitokeza kwenye nafasi ya Ukatibu walikuwa ni Athumani Nyamlani aliyepata kura 6, Juma Ndwangila aliyepata kura 59 pamoja na Laurence Limwata aliyeapata kura 11. Hivyo nafasi ya Ukatibu kuchukuliwa na Juma Ndwangila.
Kwa upande wa jimbo la Kigamboni wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa jimbo walikuwa ni Ally Makwilo aliyepata kura 28, Shaaban Mbegu aliyepata kura 7 na Yasin Kanyama aliyepata kura 43. Hivyo Yasin Kanyama akatangazwa ndiye mshindi wa Uenyekiti wa Jimbo la Kigamboni kupitia UVCCM.
Halikadhalika upande wa makatibu wagombea wa jimbo la Kigamboni walikuwa ni Kambarage Makongoro aliyepata kura 27, Mustaffa Pilla aliyepata kura 32 na Salum mpili aliyepata kura 16 na matokeo hayo yalimpa ushindi Ndugu Mustafa Pilla kuwa ndiye Katibu wa jimbo la Kigamboni kupitia UVCCM.

CHADEMA yatishia kususia bunge la Katiba…!!

WAKATI keshokutwa Bunge Maalum la Katiba linaanza kukutana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema huenda kikasusia Bunge Maalum la Katiba iwapo litaendeshwa kwa kufuata matakwa ya chama cha siasa na siyo ya wananchi.
Mwenyekiti wa chama hicho, FreemanMbowe alisema hayo jana wakati akielezea maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichofanyika jana na kueleza kuwa chama hicho kinaenda katika Bunge hilo kikiwa na hadhari ya hilo.
Alisema wanaenda kwenye kikao hicho wakiwa na masikitiko kutokana na uteuzi wa wajumbe 201 wa bunge hilo waliotangazwa hivi karibuni kuwa karibu asilimia 75 hadi 80 ni wanaCCM.
 mbowe
Akijibu hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema “Tumewazoea, sio mara ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni Katiba isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”.
Naye Mbowe alifafanua “Hatuendi katika bunge hilo kugoma lakini mambo yakienda visivyo kwa kufuata matakwa ya chama cha siasa na siyo mapendekezo ya rasimu ya pili ya Katiba hiyo ambayo ni ya wananchi tutalizira Bunge hilo,” alisema.
Alibainisha kuwa chama hicho hawatasita kurejea kwa wananchi wakati Bunge likiendelea au likiwa limeisha iwapo wingi wa wabunge wa chama tawala utaathiri Bunge hilo.
“Sasa wananchi watatuelewa dhamira yetu ya kutaka wajumbe hao wasiteuliwe na Rais kwani tulibishana sana lakini baadaye tulikubalianajambo ambalo limeonesha kwa kuteuliwa makada wengi kwa manufaa ya chama tawala,” alisema Mbowe.
Alisema ingefaa makundi yenyewe yangeteua wawakilishi wao na siyo kupeleka kwa Rais hivyo Bunge hilo linaloanza keshokutwa wanaenda kwa tahadhari.
Vikao vya Bunge Maalum la Katiba linatarajia kuanza keshokutwa likihusisha wajumbe ambao ni wabunge wote wa Baraza la Wawakilishi ,Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete akishirikiana na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein.
Wajumbe hao 201 wameteuliwa kutoka makundi tofauti yakiwemo ya Taasisi zisizo za kiserikali, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Taasisi za dini, Taasisi za elimu, watu wenye ulemavu, vyama vya wafanyakazi, vyama vinavyowakilisha wakulima, wafugaji, wavuvi na kundi la watu wenye malengo yanayofanana.
Bunge hilo litahusisha wajumbe takriban 650 wanaokwenda kuijadili rasimu ya pili ya Katiba na watatumia siku 70 na iwapo hazitatosha wataongezewa siku 20 ili kukamilisha mjadala huo. Kitakachofuata baada ya Bunge Maalum la Katiba ni wananchi kupiga kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo mpya.
Katiba hiyo mpya itafuta Katiba ya sasa iliyodumu tangu Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 na mabadiliko kadhaa yaliyofuatia baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alipoulizwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema “tumewazoea, sio mara ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni Katiba isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”.
soma zaidi hapa <<bofya hapa>>

February 15, 2014

CHADEMA kanda ya ziwa yawatimua Viongozi wake watano kwa kosa la kumpa ushirikiano Zitto Kabwe

chadema
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki leo kimewavua nyadhifa zao viongozi wake watano wa jimbo la Kahama kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukiuka taratibu za chama hicho. 
Uamuzi huo umetolewa na Mratibu wa Chedema Kanda ya Ziwa Mashariki Renatus Nzemo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya Kanda ya Ziwa Mashariki na kupitia mazimio hayo kabla ya kutoa uamuzi.
 
Viongozi waliovuliwa nyadhfa zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama IsraelBarikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa, Katibu Mwenezi wa jimbo Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na Mwenyekiti Bavicha Benedict Shija.
 
Katika Barua yake aliyoiandika kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka tamko la kamati kuu ya chama lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na aliyekuwa naibu katika mkuu wa chama hiccho Zitto Kabwe.
 
Tuhuma zingine ni kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe kupitia chama cha TADEA, huku viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa wako tayari kumfuata Zitto popote atakapokuwa.
 
Aidha Nzemo amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi chama kingine cha Alliance for change and Transparency (ACT), kinyume cha maadili ya CHADEMA katika katiba yake ya mwaka 2006.

February 13, 2014

Edward Lowasa, Fredrick Sumaye na William Ngeleja wahojiwa na kamati ya maadili CCM Dodoma leo…Wengine Waingia Mitini

Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
 
 Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 
 
 
 Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
 
 
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
 
 
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.
 
***
 
 Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali.
  
Ambao hawakufika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu StephenWassira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba.