Pages

February 04, 2014

JOKATE AMVULIA KOFIA WEMA ,,,, NI KUHUSU BIFU LAO LA KUGOMBANIA PENZI LA DIAMOND... SOMA HAPA!

WERAWERAA! Staa wa Bongo anayesumbua kwenye mitindo na sinema, Jokate Mwegelo amekubali kushindwa baada ya kumwangukia Wema Sepetu waliyekuwa kwenye bifu la kimyakimya wakigombea penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo la kufungulia mwaka lilijiri wikiendi iliyopita jijiniArusha, katika kiwanja cha kulia bata, Triple A Club ambapo Wema alikuwa akimtambulisha mwanamuziki Miraji Hussein ‘Mirror’ kutoka Lebo ya Endless Fame Production.
BONGE LA SAPRAIZI
Mwandishi wetu ambaye alikuwa katika msafara wa Wema na mashosti zake, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel waliokuwa wakimpa kampani, hakumuona Jokate, hivyo alifika pale kwa kushtukiza.
Jokate akionekana mwenye furaha, alipanda jukwaani na kuomba kuzungumza machache ambapo alimkumbatia Wema kwa furaha huku akionekana hana kinyongo.

AKIRI WEMA NDIYE MKE MKUBWA
“Wema ni rafiki yangu na ninampenda kwa dhati... yaliyopita yamepita. Nipo hapa kwa ajili ya kumpa sapoti kutokana na upendo nilionao juu yake. Nakiri  yeye ni mke mkubwa. Nimeamua kumshtukiza ili aone thamani yake kwangu.”
Maneno hayo ya Jokate yalisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele za shangwe.

AMWAGA MINOTI
Kama vile haitoshi, huku shangwe zikiendelea, bidada huyo alitoa burungutu la fedha na kuanza kumtuza Wema.

Pia aliwatuza Kajala na Aunt ambao wote kwa pamoja walikuwa wamevaa sare kama kinogesho cha shughuli hiyo.
JOKATE ABANWA
Risasi Mchanganyiko halikuishia kufotoa picha na kuweka gazetini pekee, lilimfuata Jokate na kumwuliza sababu ya kufanya tukio hilo ambapo alijibu kifupi: “Ni upendo tu dadangu.”

Alipobanwa zaidi alisema: “Mimi niliona nikifika kumpa kampani mwenzangu itapendeza sana na sikutaka ajue mapema ili ujio wangu umshangaze. Nimefurahi imekuwa hivyo.”
WEMA SASA!
“Yaani nimefurahi sana kuona Jokate anajua kuwa mimi ni mke mkubwa na ndiyo kila kitu,  nimefurahi kuacha kazi zote kuja kuungana nami, kitu ambacho nimekiona tofauti kwani hatukuwahi kukaa hivyo na Jokate tangu tulivyoingia kwenye mgogoro (wa kumgombea Diamond),” alisema Wema.

WEMA / JOKATE
Upinzani wa Wema na Jokate ulianza kitambo kwani mwaka 2006, Wema ndiye aliyeibuka Miss Tanzania akifuatiwa na Jokate aliyeshika namba mbili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Lisa Jensen.