Pages

February 06, 2014

SHERRY MAGALI AUGUA, AKONDA

STAA wa filamu za vichekesho Bongo ambaye ni mtoto wa Mzee Charles Magali, Sherry Charles Magali ana hali mbaya na sasa ukimuona huwezi kumtambua kama ni yeye.


Sherry Charles Magali kabla ya kukonda.
Hali hiyo imekuja kutokana na maelezo kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo kiasi cha kumfanya akonde sana na lile wowowo lake lililokuwa likimtambulisha kwenye usanii kupotea.
“Yaani sina hata la kusema kwani najikuta napata aibu kwa sababu watu wananishangaa sana, moyo unauma, najitahidi kutumia tiba mbalimbali lakini naamini nitapona,” alisema Sherry.