Gari la polisi wilaya ya Kahama likiwa limezungukwa na wananchi eneo la Tukio |
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Nyihogo Amos Sipemba, aliyefika eneo la tukio mara baada ya mauwaji hayo, amesema hadi sasa mmoja wa marehemu ametambulika kwa jina la Joseph Bakuku huku mwingine akiwa bado hajafahamika.
Sipemba amesema huenda kufanyika kwa mauwaji hayo kunatokana na wananchi hao kuwahisi vijana hao kuhusika katika matukio mawili ya uvamizi yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika kata hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.
Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katia chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.