Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.
Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.
Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa kumsaidia.
Cedeno alisema: ‘Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri – nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.
‘Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.’
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake.
Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.