Pages

February 07, 2014

WEMA, AUNT, KAJALA WAFANYA MASHINDANO,,,, WAANZIA KWENYE MIDOMOWAMALIZIA KE=WENYE MAUNO,,, CHEKI HAPA!

 MADIVAS waBongo Movies, Wema Sepetu, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel wamenaswa wakishindana uzuri wao kuanzia kwenye midomo hadi katika uwezo wao wa kukata mauno.
 
...Wakiwa katika picha ya pamoja.
Uwanja wa ‘mashindano’ ulikuwa ni pande za Arushawalipokwenda kwa ajili ya kumtambulisha msanii anayepiga mzigo  kwenye lebo ya Wema, Endless Fame, Miraji Hussein ‘Mirror’.
Weekly Star Exclusive ilishuhudia tukio zima ambapo mastaa hao walianza kufanya vituko hivyo ndani ya Hotel ya Point Zone iliyopo jijini hapo, kamera ya paparazi wetu iliwamulika wakishindana kumpata staa mwenye mdomo mzuri kuliko wenzake.
Waligusanisha vichwa na kisha kujitazama katika kioo kisha kuanza kutambiana huku kila mmoja akidai yeye ndiyo mkali kuliko mwenzake. Hawakuishia hapo, walisimama na kuonesha uhodari wa kukata mauno na kudai  wataumalizia mpambano huo katika Ukumbi wa Tripple A.

 
...Wakicheza na Mirror.
“Mnanionaje? Nataka kujua nani zaidi katika yetu hapa au ngoma droo nataka kujua hilo jamani? Kama hapa droo, kivumbi zaidi ni huko ukumbini,” alisika Wema.

 
Mastaa hao wakiwa stejini ndani ya Triple A.
Mastaa hao walipofika katika Ukumbi wa Triple A, waliendeleza mpambano huo ambapo mashabiki walipagawa na kutoa maksi kwa kupiga kelele za shwangwe kila walipokuwa wakikatika huku wakimwagiwa noti.