MAMA wa majanga, Snura Antony Mushi kwamara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumzia kauli ya msanii mwenzake wa muziki wa mduara, Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole’ juu yake kuwa ameisha kimuziki ndiyo maana ameamua kukimbilia muziki wa Taarab.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Snura ambaye anawika mitaani kwa ngoma kali kama Majanga na Nimevurugwa, alisema kitendo cha Shilole ‘kuponyokwa’ na maneno hayo ni ishara tosha kuwa anamkubali na kufuatilia kazi zake kwa ukaribu mkubwa.
“Sina tatizo na maneno ya Shilole, hiyo ni ishara kuwa anafuatilia na kuzikubali sana kazi zangu, wala hawezi kunizuia kufanya kazi zangu kwa namna ambavyo nafikiria, yeye afanye yake, nami nishike ‘hamsini zangu’, alisema Snura.