Huu
ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita katikati ya Hospitali ya
Palestina ambapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu
katika kila kona ya hospitali hiyo.

Kushoto
ni mgonjwa akiwa amelala juu ya benchi ambapo pembeni kuna maji na
matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali
katika makazi ya watu.

Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate kuhudumiwa.

Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa kunyesha.
Huu
ndio mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya
hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya mtaro huo kuziba.
Mapema
mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini
Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi
kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara, nyumba za
watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya
hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014
hadi Tarehe 7.03.2014 zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali
ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na
kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya meza na viti wakikwepa
maji hayo wakati wengine wakikimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si
ya mvua tu lakini yalikuwa ni machafu yaliyochanganyikana na maji
kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
Baada ya mvua hiyo kuisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Baada ya mvua hiyo kuisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea kwa simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.