Kumekuwa na ghadhabu nchini Tanzania kufuatia uamuzi wa wabunge kujiongeza maelfu ya dola kama marupurupu.
Marupurupu hayo yatatolewa kwa kila mbunge wa bunge la Tanzania lenye wabunge 357 wakati watakapokamilisha muhula wao wa tano kama wabunge.
Kila mbunge nchini Tanzania, hupokea mshahara wa dola elfu saba kila mwezi.
Wakazi wa Dar es Salaam wakihojiwa na waandishi wetu kuhusu swala hili, wamejibu kuwa wameshtushwa sana na marupurupu hayo hasa baada ya kuambiwa na serikali kuwa hakuna pesa za kutosha kwa matumizi ya huduma za jamii.