Pages

February 28, 2014

Ajali: Basi la Bunda Express lagongana na Treni Manyoni mkoani Singida…38 Wajeruhiwa Vibaya, Mmoja Afariki

ajali
Mtu  mmoja  amefariki  dunia  na  wengine  38  wamejeruhiwa  vibaya  kufuatia  ajali  ya  basi  la  Bunda  Express  walilokuwa  wakisafirikia   kutoka  Dodoma  kwenda  Mwanza  kugongana  na  Treni  eneo  la  Manyoni  Mkoani  Singida.
AJALI2AJALI1

Majeruhi   wa  ajali  hiyo  wamepelekwa katika   Hospitali ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Aibu! Njemba Anaswa na Mke wa Rafiki yake Gesti…!!

NJEMBA1
MAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’! Ni kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz.
Mke wa mtu sumu: Anton John Mwaweje baada ya kunaswa akiwa na mke wa rafiki yake gesti.
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni- Malapa jijini Dar es Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Mshangao: Anton John akishangaa baada ya kuba
Habari zikazidi kudai kwamba, ilifika mahali katika kumtaka shemejiye huyo ambaye alikuwa akimkatalia katakata, Mwaweje alitumia gia nyingine ikiwemo ya kumuahidi mambo manono kama angekubali kuivunja amri ya 6 ya Muumba na yeye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa,  ‘Mungu si Athuman wa Lucas’ siku isiyo na jina jamaa alimtumia ujumbe (SMS) mke wa mwenzake kwa kutumia maneno ya kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo bwana simu alikuwa nayo mwenye mke.
Misosi na mitungi: Baadhi ya misosi na vinywaji vilivyokutwa chumbani humo.
Chalz alimwita mkewe na kumuuliza ni nani aliyemtumia ujumbe huo? Ndipo mke akaanika ukweli akisema:
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume:  “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”
Za mwizi 40: Bwana Anton John akiwa na pingu mkononi baada ya kunaswa na kamanda wa OFM pamoja na wanausalama.
Pia, mwanamke huyo alimwonesha mumewe meseji kibao ambazo jamaa huyo amekuwa akimtumia na zile ambazo yeye amekuwa akimkatalia.
“Sasa sikia, mkubalie,” mwanaume huyo alimwambia mke wake huku midomo ikimcheza kwa hasira.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.
Baada ya kupanga mipango ya kukutana, mume huyo alipiga simu Global Publisherskwenye kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kuomba msaada wa fumanizi ambapo alibahatika kukuta kuna kamera mpya zimewasi tayari kwa kazi kama hizo.
Baada ya kupata maelezo ya Chalz, OFM ilishirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni –Kwamnyamani jijini Dar na kuandaa mtego ambapo Jumatatu iliyopita, saa nane na ushee mchana, Anton ambaye naye inasemekana ana mke aliuingia mtego na kunasa kwenye chumba namba 5 akiwa na mke mwema huyo.
Ndani ya chumba hicho, Anton alikutwa na boksa  tayari kwa mlo wa wizi ambao alibakia kuendelea kusikia njaa. Mezani, kulikuwa na chipsi kuku na pombe ambazo zingewapa stimu kabla ya mchezo.
Kitendo cha Chalz kumnasa jamaa huyo na mkewe kitandani kilimpandisha munkari ambapo nusura afanye ndivyo sivyo lakini alitulizwa na polisi waliokuwa eneo hilo kwa ajili kulinda usalama.
Kilichofuata baada ya hapo, mgoni huyo akiwa na pingu mkononi alipelekwa kwenye kituo hicho cha polisi ambapo awali, Chalz alitoa ripoti ya malalamiko baada ya kugundua  jamaa huyo anataka kumtumbukiza mkewe kwenye mstari wa usaliti.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo, taratibu za kisheria kuhusiana na kesi hiyo zilikuwa zikiendelea huku mgoni huyo akiwa chini ya ulinzi mkali.
Credit: Global TV Online

Uamsho Wapata dhamana baada ya Kusota Rumande kwa Mwaka Mmoja.

RUMANDE
Baada ya kusota rumande kwa takribani mwaka mmoja na miezi minne, viongozi 10 wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho) jana waliachiwa kwa dhamana yenye masharti nafuu na kujumuika na familia zao.
Awali, viongozi hao walishindwa kutimiza masharti waliyopewa na mahakama ambayo yaliwataka kutoa fedha taslim Sh. milioni 25, kuwa na wadhamini watatu wakiwa ni watumishi wa serikali wenye mali isiyo hamishika ya Sh. milioni 25 pamoja na kutosafari nje ya kisiwa cha Unguja.
Hata hivyo, baada ya kilio cha washtakiwa hao wakiongozawa na mawakili wao Juma Abdallah na Salum Taufik, Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar,  Fatma Hamid Mahmoud, jana alipunguza masharti ya dhamana baada ya washtakiwa hao ambao wamekuwa wakishikiliwa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minne kuanzia Oktoba 17, mwaka 2012, kulalamika kwamba masharti ya dhamana ni magumu.
Jaji huyo alikubali kila mshtakiwa kujidhamini kwa Sh. milioni 25 kwa maandishi sambamba na kuwa na wadhamini wawili badala ya watatu huku mmoja kati ya hao awe mtumishi serikali.
Kadhalika, Jaji Fatma aliwaruhusu washtakiwa hao kusafiri kwenda Pemba, lakini masharti ya kutosafiri nje ya Zanzibar pamoja na kutofanya mihadhara miskitini na nje ya misikiti yanaendelea hadi kesi ya msingi itakapoanzwa kusikilizwa.
Washtakiwa hao ni Majaliwa Fikirini Majaliwa, Faridi Hadi Ahmed, Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Mussa, Azani Khalid Hamdani, Suleiman Juma Suleiman,  Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakari Suleiman, Gharib Ahmed Juma na Abdallah Said.
Washitakiwa hao walishtakiwa kwa makosa ya kufanya uchochezi, ushawishi, kuhamasisha fujo na kula njama ya kufanya kosa kulikosababisha uvunjifu wa amani na usalama wa taifa Oktoba, 2011.

Jaji Fatma alisema watuhumiwa hao wameshakaa rumande kwa muda mrefu, hivyo mahakama imetafakari na kuona kuwa dhamana ni haki ya kila mshtakiwa ambaye kosa lake linastahiki kupewa dhamana.

“Endapo mshtakiwa atakaa rumande kwa muda wa miezi minne bila ya kesi kutokuwa na ushahidi, mahakama ina uwezo wa kuifuta kesi na siyo halali kumuadhibu mtu kwa kumuweka rumande bila ya ushahidi,” alisema Jaji Fatma.
Aliwataka washtakiwa hao kuhakikisha wanalinda amani na usalama wa nchi na kwamba ikiwa watakiuka masharti hayo, mahakama itafuta dhamana waliyopewa.

 Jaji Fatma aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 27, mwaka huu.

“Madawa ya Kulevya na Bangi sasa Basi”….Banza Stone

banza
  Mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
 
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV  mwanzoni mwa wiki hii, Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa kuchanganya na sigara au bangi.
 
“Ujana ulisababisha nikajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa nimeacha kabisa na nawashauri vijana wenzangu kuwa mbali na kilevi hicho kwani kama huna kipato cha kutosha unaweza kugeuka kibaka maana mwili ukizoea ni vigumu kuacha.”
CREDIT: GPL

Jokate Aupiga Chini Ulokole.

jokate mwigelo
Picha za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa analosali kumsema kuwa anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema: “Ninachokumbuka Jokate aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili amtumikie Yesu kisawasawa lakini kwa mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole itakuwa basi tena.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo, alipopatikana alisema: “Nilizipiga kwa ajili ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo ya Kidoti.
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi sana?
Jokate: Huh!
Ijumaa: Huh nini?
Jokate: Nishasema ni za Kidoti, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele zangu.
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena?
Jokate: Kimyaaa.
Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo huyu kwamba, kwa kuwa ameshajijengea heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema akawa makini na mavazi kama haya ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa tofauti.

February 27, 2014

Laana! Mfanyabiashara Anaswa Gesti Akitaka Kumlawiti Modo Maarufu wa Kiume Jijini DAR..!!

kibo
EEH Mungu! Unaweza kukataa lakini ni ukweli kwamba dunia imekwisha! Mambo yanayotendeka kila kukicha juu ya ardhi yanathibitisha hilo.
kibo
OFM walivyomnasa mfanyabiashara wa magari (kushoto) chumbani akitaka kumlawiti modo maarufu.

Mfanyabiashara maarufu wa magari jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Juvenali amekumbwa na aibu ya mwaka baada ya kunaswa mtupu chumbani na mmoja wa wabunifu wa mavazi ‘modo’ maarufu Bongo (jina tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili).

…amefungwa pingu.

Tukio hilo la aibu lilimkuta mfanyabiashara huyo nyumbani kwake, Mbezi ya Tangi-Bovu jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo wawili hao walinaswa chumbani wakiwa watupu katika mtego maalum.
KISA KILIPOANZIA
Chanzo cha kufichuka kwa taarifa hizo ni modo huyo kumwonesha kaka yake (naye jina tunalo) meseji ‘tamutamu’ kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwenda kwake akimshawishi kumlawiti.
KAKA MTU ACHARUKA
Ilidaiwa kuwa kaka mtu alikasirika, aliamini kitendo cha mfanyabiashara huyo kutaka kumlawiti mdogo wake ni kuidhalilisha familia.
“Kaka akamwambia mdogo wake kwamba ni lazima wamtege jamaa huyo ili kumshikisha adabu na ache tabia hiyo,” kilisema chanzo.
                                                                      …Akitatiwa na Polisi.

KAKA ACHUKUA GAZETI, APIGA SIMU OFM
Baada ya kukubaliana na mdogo wake, kaka huyo alitafuta Gazeti la Amani na kukutana na namba za Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kuzipiga.
Kaka: Jamani poleni na kazi, hapo ni OFM?

OFM: Tumepoa ndugu, ndiyo sisi, tena unaongea na mimi kamanda mwenyewe. Niambie ndugu yangu, bila shaka unataka kutupatia kazi, tupo tayari.

Kaka: Ni kweli, kuna jamaa mmoja ni mfanyabiashara wa magari, anamtumia meseji mdogo wangu akimshawishi amlawiti. Tukio hili limenikera sana. Naomba tukutane ili tupange jinsi ya kumnasa ili kukomesha tabia hii.

Nimeshazungumza na mdogo wangu na yupo tayari kwa jambo hilo ili tumtege, tukamilishe hiyo kazi kukomesha huu upuuzi.

OFM: Sawa kabisa, inawezekana.
Kilichoendelea hapo ilikuwa ni OFM kumpa baadhi ya maelekezo kaka mtu, wakakubaliana kila kitu namna mchezo ambavyo ungekamilika kwa mbinu za kitaalam za makachero wa OFM.
                                             …Mfanyabiashara  huyo akichukuliwa na polisi.

OFM YAPOKEA KAZI, YARIPOTI POLISI
Baada ya kukutana na kaka wa modo huyo na kupanga kila kitu, OFM iliwasiliana na Jeshi la Polisi Kituo cha Mbezi – Makonde, Dar ambapo taarifa za uovu huo zilikuwa na dalili ya kufanyika karibu na maeneo hayo.
Mkuu wa kituo hicho alitoa ‘vijana’ wake wawili, shupavu waliojitambulisha kwa majina ya Afande Nassoro na Afande Sele. Wakakamavu kabisa.
                                             …Safari ya kuelekea kituo cha polisi cha Kawe.
KATIKA ENEO LA TUKIO
Fasta, OFM na askari hao walielekea Mbezi Tangi – Bovu, kituo cha daladala eneo la mtego ambapo mfanyabiashara huyo alimuahidi kijana huyo akamchukulie hapo kwenda naye kwenye nyumba ya kumfanyia usodoma.
MFANYABIASHARA AFIKA NA GARI
Wakiwa mita kadhaa, OFM na polisi, walimuona mfanyabiashara huyo akiwasili na gari aina ya GX 100 (namba za usajili tunazo). Alifunga breki miguuni kwa kijana huyo, akamfungulia mlango, naye akazama ndani.
Safari ilianza kuelekea upande wa Bagamoyo lakini mita chache gari hilo lilikata kulia. OFM na maafande walikuwa wakifuatilia kwa nyuma bila kujulikana.
                                                                    …Akiwa kituo cha polisi.
GARI LAFIKA NYUMBA YA TUKIO
Baada ya mwendo wa kama kilometa mbili, gari hilo lilifika kwenye nyumba  moja na kupiga honi kisha geti  likafunguliwa, gari likaingia na geti likafungwa.
MODO NDANI YA CHUMBA CHA TUKIO
OFM, maafande wakiwa nje, wawili hao tayari walikuwa chumbani ambapo dogo huyo aliwasiliana na ‘makachero’ wa nje na kuwaambia kwamba mfanyabiashara huyo alishasaula nguo na yupo kama alivyozaliwa, alikuwa katika hatua za awali za kutaka kukamilisha ufirauni wake. Hapo sasa OFM na polisi wakajipanga kuchoma ndani kuzuia unyambisi huo.
KIZINGITI
Hata hivyo, OFM na askari hao walishindwa kuingia baada ya geti kufungwa kwa ndani na aliyefunga kutoka nje kwa kutumia mlango mwingine.
Hata hivyo, askari walitumika ukomandoo, ‘timu’ ikafanikiwa kuzama ndani moja kwa moja na kwenda kugonga katika chumba husika (wale askari hatari sana aiseee!).
AFUNGUA MLANGO BILA WASIWASI
Bila kujua kuwa OFM na polisi ndiyo waliogonga mlango,  jamaa huyo alifungua mlango na kukutwa akiwa mtupu sanjari na modo huyo.
SHETANI ATUPIWA ZIGO
Maafande walimuuliza ‘biznesmani’ huyo ni kwa nini wamekutwa uchi tena wanaume watupu chumbani, alijibu kuwa walikuwa wanahisi joto ndiyo maana waliamua kuvua nguo zote.
Lakini akaongeza: “Jamani niacheni. Hii ni aibu, nitawapeni chochote kile mnachotaka, shetani ndiye alinipitia jamani.”
SAFARI KUELEKEA LUPANGO
Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na askari hao hadi polisi lakini baadaye akahamishiwa Kituo cha Kawe ambako shauri hilo liliandikishwa na kupewa jalada la kesi namba KW/RB/1747/2014.
Baada ya kuchukuliwa maelezo, mfanyabiashara huyo aliswekwa lupango akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

CREDIT: GPL

Mimba ya Linah Aliyopewa na Mdosi Yachoropoka…!!

mimba
SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.
mimba
Astelinah Sanga ‘Linah’.

Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.

“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.

Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.

“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.

NAPE ATUA SHINYANGA KUWATAMBULISHA MADIWANI WALIOTEMA CHADEMA NA KUJIUNGA CCM.

CDM
Kutoka kushoto ni Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masekelo(Chadema) na Kulia ni Sebastian Peter aliyekuwa diwani kata ya Ingokole(Chadema) wakitambulishwa mbele ya umati wa watu na Katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini ambao kwa moyo mmoja wamejiunga na CCM.

February 26, 2014

Slaa adai kuwa Kiongozi anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi …..Asema hata wakibaki watatu, chama HAKITAKUFA

slaa

Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama.
 
Alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMAjimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi huku akisisitiza kuwa   hata  wakibaki  watatu  tu  ndani  ya  chama, Chadema  haitakufa  na  kwamba  wameridhia kujiuzulu kwa madiwani wao wawili mkoani Shinyanga.
slaa
Dk. Slaa
 
Alisema kujiuzulu kwao ni mpango maalumu uliotengenezwa na wapinzani wao kisiasa kwa lengo la kuwadhoofisha na kuwavuruga.

“NASIKITISHWA NA WASANII WANAO PENDA KUTENGENEZA UGOMVI WA KILAZIMA NA MIMI”…DIAMOND

Diamond
Muda si mrefu Diamond Amefunguka haya hapa chini kuhusu wasanii wanasanii wanao tafuta beef za lazima kutoka kwake …Jisomee

Makongoro Nyerere: Msiponiachia Najiua.

makongoron

Makongoro Nyerere

MSHITAKIWA Makongoro Nyerere anayekabiliwa na kesi ya mauaji ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imuachie huru akaishi na watoto wake au ajiue.
Makongoro alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Liwa, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Inspekta Jackson Chidunda kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Makongoro, ambaye ameshitakiwa pamoja na mfanyabiashara maarufu Abubakar Marijan (50), ‘Papaa Msoffe’ aliomba mahakama imuachie huru kwa kuwa hana kesi, alikuwa anafanya kazi halali lakini ameambiwa ameua, kisa Sh milioni nane.

Makongoro Afunguka

“Tarehe nyingine kesi itakapotajwa naomba niachiwe nikakae na watoto wangu niende nikakae polisi, huko watajua pa kunipeleka kama kujiua nijiue,” aliomba Makongoro.
Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 11, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Aliutaka upande wa Jamhuri kuharakisha upelelezi. Jana Papaa Msoffe hakufika mahakamani hapo kwa madai kuwa anaumwa.
Makongoro
Makongoro Nyerere
Washitakiwa wanadaiwa Oktoba 11, mwaka 2011 katika eneo la Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam kwa makusudi walimuua Onesphory Kituli.
Hawakujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na wataendelea kusota rumande kwa kuwa mashitaka yao hayana dhamana.

Wananchi wataka Posho ya wabunge wa Bunge la Katiba ipunguzwe kutoka 300,000 hadi 170,000

Bunge la Katiba
WAKAZI wa wilaya za Tarime na Rorya mkoani Mara, wameshauri kupunguzwa kwa posho za wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba kutoka Sh 300,000 hadi Sh 170,000 ambazo walisema ni za kawaida kwa vikao vya Bunge.
Wamewaomba pia wajumbe hao ambao wamekwenda kuwawakilisha wenzao kuweka maslahi ya Taifa mbele na kuacha tamaa za kujipatia fedha nyingi ambazo ni kodi za wananchi.
Waliotoa ushauri huo ni Sigirya Mwita ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Pemba,Peter Mwera ambaye ni Diwani wa CCM wa Kata ya Mriba na Nyangoko Paulo ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji Sirari kupitia Chama cha Chadema.
Wengine ni wananchi wa kawaida Otieno Igogo, Matiko Majani, Elizabeth Mseti, Ores Lameck, Kansela Sereria, Maria Bhoke na Gimase Marwa.
Viongozi na wananchi hao walisema hawakubaliani na maombi ya wabunge hao ya kuomba serikali kuwaongezea posho na badala yake wapunguziwe kutoka Sh 300,000 za sasa hadi Sh 170, 000 ambazo ndizo zinazokubalika kisheria kwa vikao.
“Katiba hii wanayoijadili ni ya Watanzania wote hata wao wamo na familia zao. Hawakupendekezwa kwenda kujitafutia mitaji na kutaka kuhujumu uchumi wa nchi. Kuna baadhi yao humo hawapati au kuzalisha hata Sh 100,000 kwa siku kwao.
“Kisingizio kuwa ni wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba hakina mashiko.Tunaomba Serikali kutowaongeza posho hizo badala yake zipunguzwe kwani fedha hizo ni za wananchi ambazo zingine hupelekwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, barabara, kuchimba visima vya maji na kuwasomesha wanafunzi waliokwama kuendelea na masomo,” walisema kwa nyakati tofauti.
Credit: Habari Leo

February 25, 2014

ASKOFU BILIONEA ATIKISA BONGO

Askofu bilionea

Askofu Bilionea

ASKOFU Bilionea na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.
Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie(Askofu Bilionea) ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.

Alindwa na Jeshi la Polisi

Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Askofu Bilionea alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.
Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.

Waumini wabaki na Mshangao.

“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

Ugumu wa Kumwona

Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka  kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” alisema Fred Mushi.
Askofu bilionea
Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.