Kufuatia kitendo ovu cha wafuasi wa chadema mkoani mbeya kuchonga jeneza na msalaba wenye jina la zitto, mbunge huyo ameeleza ifuatavyo:
"Chuki za kisiasa za kiwango hiki ni hatari sana. Viongozi wakuu kutokukemea mambo kama haya ni ishara ya udhaifu na kukosa busara. Kamwe sitalipa ubaya. Wema kwa ubaya ndio silaha tosha na mungu siku zote yupo na wanyonge. Nimechukizwa. Mola atawasamehe maana hawajui watendalo".