Huku nchi ikiwa kama imesimama kwa wiki sasa kufuatia Operesheni kubwa na ya kishindo ya M4C OPD hatimaye wananchi kadhaa wameshtushwa na mgogoro mkubwa wa kimadaraka unaondelea ndani ya CCM kufuatia makada wa kambi tofauti kutuhumiana hadharani na kushambuliana bila aibu kama walivyofanya John Guninita na Paul Makonda wa UVCCM huku kila kundi likihami kambi yake.

Huku hayo yakiendelea Chadema imetoa Ratiba ya siku ya leo tarehe 29.1.2014 ya M4C OPD kama ilivyothibitishwa na Afisa Habari Mkuu wa Chama Tumaini Makene.

Timu ya Mkiti Mbowe, Halima Mdee na Suzan Kiwanga: Kilombero (Ifakara), Kilosa (Ludewa), Mvomero (Mtibwa) na Morogoro mjini (Tungi), 

Timu ya Katibu Mkuu Dkt. Slaa, Makamu Mwenyekiti Said Issa Mohamed, John Mnyika: Iselamagazi , Kishapu, Mhunze, Itilima na Bariadi mjini. 

Timu ya Lissu na Heche: Kondoa mjini, Mangungu, Orkesemet na Mwanga.