Watajwa hapo juu ni miongoni mwa wanachama ambao walikuwa wanakesha mtandaoni kukitetea CHADEMA ijapokuwa walikuwa wanazidiwa kwa hoja na vijana wa Lumumba. Watu hao walikuwa wanatumia muda mwingi kuwapotosha watumuaji wa mtandao hasa katika ufafanuzi wao ambao kimsingi uliacha maswali mengi.
Moja ya kituko ambacho sitakisahau ni katika sakata la kuondoa ukomo wa madaraka kinyemela kwenye Katiba ya CHADEMA . wadau hawa walijichanganya sana kiasi cha kuzua maswali mengi mtandaoni na mjadala kuhamia huko uswahilini. Mathalan, wakati Dr Slaa akisema kuwa kipengele hicho hakijawahi kuwepo kwenye katiba yoyote ya CHADEMA, Mnyika alisema kuwa kipengele hicho kilikuwepo kwenye katiba ya 2004 lakini kwenye maboresho ya katiba ya 2006 hakikujadiliwa. Tumaini Makene naye akaja na hekaya yake kuwa kipengele hicho kilijadiliwa na wajumbe walikubaliana kukiondoa. kutokana na mkanganyiko huo, hali hiyo ilitafsiriwa ni kama uropokaji wa wanachama na viongozi hao wa CHADEMA mitandaoni.
Hivi sasa, kuna mijadala mingi inaendelea kwenye mtandao ambayo tulitaraji kuona wanachama na viongozi hawa wakijitokeza kama kawaida yao kutoa ufafanuzi. Moja ya hoja ambayo sasa inabamba ni hii ya CHADEMA kutumia zaidi ya bilioni moja kama gharama za M4C OPERESHENI PAMOJA DAIMA. Katika mjadala huu, sijamuona Tumaini Makene, Mnyika wala Molemo kutoa ufafanuzi. Najua Dr Slaa anaona aibu kuingia humu baada ya kutoa ufafanuzi uliomvua nguo.
Kuna vijana pia wanajiita akina Yeriko Nyerere na Ben Saanane. Hawa kwa kiwango kikubwa ndio waliokuwa wanatetea msimamo wa CC ya CHADEMA katika sakata la ZITTO KABWE. Baada ya suala hilo kufikishwa mahakamani na Kijana Albert Msando kuwagaragaza mawakili mashuhuri wa chama hicho, TUNDU LISSU na PETER KIBATARA, hawa vijana nao wamekimbia jukwaa. Sote kwa pamoja tuna kila sababu ya kuuliza hawa jamaa zetu yamewakumba yepi mpaka hawaonekani? je Wametekwa? tunawaomba waonekane mtandaoni kwa ajili ya mijadala zaidi ya mambo yanayojiri sasa.