Upinzani nchini Afrika Kusini unataka
uchunguzi kufanywa kuhusiana na
madai ya ubadhirifu wa pesa
zilizotengwa na chama hicho kwa
matumizi wakati wa hafla ya mazishi
ya hayati Nelson Mandela.
Matakwa hayo ya upinzani
yametolewa baada ya taarifa za jarida
moja kusema kuwa, sehemu ya dola
elfu miatano zilizotengwa mahsusi kwa
shughuli ya kuwasafirisha
waombolezaji katika mazishi ya Mandela, zilitumiwa kwa shughuli
nyinginezo ikiwemo kushonesha fulana
za chama cha ANC Chama cha ANC ambacho kimezongwa
na kashfa za ufisadi hakijajibu tuhuma
hizo.
Duru kutoka mji wa East London
zimesema takriban dola laki tano
zilitengwa kando kusaidia katika
kuwasafirisha waombolezaji wakati wa
ibada maalum ya Nelson Mandela.
Hata hivyo fedha hizo zilielekewa kwa
kampuni nyingine ambazo hazikua
zikitoa huduma za uchukuzi. Diwani mmoja wa chama cha
Democratic Alliance ameambia BBC
kwamba zilitolewa risiti bandia.
Manispa hio imesema inasubiri ripoti
kamili kuwasilishwa mbele yake
mwishoni mwa mwezi huu.
Utawala
wa Rais Jacob Zuma unakabiliwa na
uchaguzi mgumu mwaka huu wakati
ukikumbwa na sakata nyingi za ufisadi