Kwa mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye
mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za
Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa
Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia
shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye
shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi
karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema
chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu
walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno,
alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali
walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota
mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi
January 31, 2014
SHILOLE NAYE AOPOA JIBWANA LA KIZUNGU…!!!
17:32:00