SOMA YANAYOJIRI SASA KATIKA JAMII
naanza scenario maelezo yatafuata chini;

Scenario No. 1
Kuna baadhi ya familia kuanzia baba hadi watoto kwa ajili ya kuogopa au usumbufu wa kuamka usiku kwenda kujisaidia walikuwa na makopo ndani kwa ajili ya huduma hiyo, basi cha kwanza dada akiamka asb ni kukusanya makopo vyumba vyote na kwenda kumwaga chooni. Is it fair jamani...... too bad aisee.


Scenario No. 2
Kuna baadhi ya familia hurundika chupi za week nzima, ikifika jumamosi Mama anakusanya chu.pi za familia nzima na kumkabidhi dada kwa ajili ya kuzifua. Kwa nini hivi?

Scenario No. 3
Kuna baadhi ya familia ambayo dada wa ndani haruhusuwi kula hadi member wengine wote wa familia wale ndio yeye afuate, ni mwiko kula na pamoja na member wengine wa familia na hata kula yeye anakula jikoni na si dinning kama wengine, na ni mwiko dada kukaa sebuleni. aiseee!

Wadau naomba tudadavue tatizo ni nini kwa nini wanawake walio wengi hushindwa kuishi vema na wadada wa kazi? (akina mama ndio huwa-control wadada hawa)

Kadhia hii ndiyo huweza kusababisha wadada hao kufanya malipizi yasiyofaa kama yale ya wao pia kulipiza kwa kuwatesa watoto na hata kuwadhuru kabisa.

Je ni kweli akina mama/dada walio wengi hawaelewi umuhimu wa wadada hao wa kazi?
Nasema haya kwa kurejea matukio mbalimbali ambayo nimepata kusimuliwa na kuona namna ambavyo akina mama/ dada wengi wanawafanyia wadada hao na hata kusababisha hata watoto wa familia hizo kuwadharau akina dada hao.

Naomba michango yenu wadau walau wengine wajifunze hapa namna bora ya kuishi na wadada hao ambao kwa kweli wanaachiwa dhamana kubwa ya kuwalea watoto wetu ambao hawana hata chembe ya undugu wa damu.

Nawapongeza wale ambao wanaishi na akina dada kama wanafamilia wengine kwa maana ya wanaishi kwa upendo na kuthaminiwa kama member wengine wa familia!