Rais Kikwete muda mchache atatembelea daraja la Dumila kuona hali halisi ya uharibifu uliotokana na mafuriko ya maji na kukatiza mawasiliano ya barabara kwenda na kutoka Dodoma.

Pia Rais baada ya kuona uharibifu huo ataongea na wananchi waathirika wa mafuriko hayo ambao mpaka muda huu hawana makazi yoyote pia wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Pamoja na yote hayo atatembelea kambi ya ujenzi ya Wachina iliyo jirani hapo kwenye barabara ya kwenda Turiani.