Pages

January 31, 2014

BIBI ANAYESADIKIKA KUWA NI MCHAWI AMEKUTWA CHUMBANI KWA MTU HUKO BUKOBA

 Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi  amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu  akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya jana  Ijumaa Januari 31,2014
 Bi. Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba. Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake  zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni  mchawi wakati wengine wakisema wasubili taarifa ya Polisi.






 Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na  Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.









Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba.
PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG