Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano Kata ya Kibindu Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani hii leo Jioni kwaajili ya Ufunguzi wa kampeni za Uchaguzi wa Udiwani CCM kwenye kata hiyo hii leo tar.27.01.2014.
Mh;Mwigulu Nchemba akimpatia Kadi ya Uanachama wa CCM mmoja ya Wananchi walioamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa hiari yao hii leo ndani ya kata ya Kibindu Wilayani Bagamoyo.


Sehemu ya Kundi Moja la Wananchi waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi wakila Kiapo cha Utii kwa Mujibu wa katiba ya CCM.Hii leo Mh;Mwigulu Nchemba amekabidhi kadi kwa Wanachama wapya 66 kwenye kata ya Kibindu.



Akiwa njiani Kuelekea Uwanja wa Mkutano,Vijana wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi Kitongozi cha Kwamasanja walimuomba Naibu Katibu Mkuu awafungulie Shina lao kwaajili ya Kuimarisha Umoja wa Vijana na shughuli za Kiuchumi zinazofanyika mtaani hapo na WanaCCM.



Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Siasa Mkoa wa Pwani kwa Chama Cha Mapinduzi Ndugu.Imani Madega akiwasalimia Wananchi waliofurika viwanja vya soko kata ya Kibindu.Madega amewaomba Wanakibindu kufanya maamuzi sahihi katika Maisha yao kwa kumchagua Mgombea wa CCM kwa sababu ndiye mwenye Ilani inayotekelezwa kwenye kata hiyo.



Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Fedha Mh;Adam Malima akisalimiana na Wananchi waliofika kwenye Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Kibindu hii leo.



Mh;Mwigulu Nchemba akiwasalimia Wananchi mara baada ya Kupandwa Jukwaani kwaajili ya kuanza kuhutubia Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Kibindu.



Huu ni Upande wa Mashariki wa Jukwaa,Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mh;Mwigulu Nchemba ambaye sehemu Kubwa ya Hotuba yake amewaomba sana WanaKibindu kufanya kampeni kwa Amani na Utulivu,Kupuuzia Wote wanaodai Miaka 50 CCM haijafanya kitu ndani ya Jimbo la Bagamoyo ili hali Barabara, Maji,Umeme(sola),Shule na Vituo Vya Afya vimejengwa ndani ya Kata ya Kibindu kwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.



Upande wa Kaskazini wa Jukwaa,Mh:Mwigulu Nchemba akiwasisitizia jambo wananchi kuhusu CHADEMA na namna wanavyosababisha mauaji kwenye Mikutano ya hadhara ili tu wapate mtaji wa kisiasa.Mwigulu amesema Watanzania wajiulize kuna vyama vya siasa 21 vyenye usajili wa Kudumu ndani ya Nchi yetu,Lakini kwa muda wa Miaka 3 tu CHADEMA wameshasababisha Vifo zaidi ya 10 kwenye Mikutano yao,Wakati Vyama Vingine vyote hata mkwaruzano tu haujawahi kutokea kwenye mikutano yao.
CCM"Tumesimamisha mgombea Kijana,anakubalika na Wakazi wote wa Kibindu,Mchagueni Ndugu Mkufya Ramadhani kuwa Diwani wenu hapa aendeleze yale yalioachwa na Marehemu Rajabu Almas aliyekuwa Diwani(CCM) wenu hapa.Msijaribu kugeuza Kibindu eneo la majaribio kwa Wapinzani,wameshindwa kujiongoza wao ndani ya chama chao,Wameshindwa kuongoza Halmashauri mbalimbali walizopewa waongoze(Mwanza n.k),Hivyo hawana sifa za kuongoza Jamii yenye kiu ya maendeleo kama hii ya Kibindu,watawapotezea muda na Ipo siki wataleta Maandamano huku ilihali mmekuwa mkiishi kwa Amani na Upendo."

Mh;Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Mkufya Ramadhani kwa Wakazi wa Kibindu waliojitokeza kwa wingi sana kwneye Mkutano huu wa Ufunguzi wa kampeni.'



Mkutano Umeshamalizika,Mh;Mwigulu Nchemba anaagana na Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano huu wa Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani unaoendelea Kata ya Kibindu,Wilaya ya Bagamoyo.