Pages

January 29, 2014

Viongozi wa waasi S.Kusini matatani


Maelfu waliachwa bila makao kutokana na vita Sudan Kusini
Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa itawafungulia mashitaka wahusika wakuu wa njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir.
Serikali ya Kiir, imesema kuwa njama hiyo ndiyo iliyosababisha mapigano kati ya serikali na waasi waliokuwa wanaongozwa na Riek Machar.
Baadhi wanahofia kuwa hatua hii huenda ikasababisha uhasama zaidi na kutishia mkataba wa amani kati ya waasi na serikali.

Pande zote mbili kwenye mgogoro wa Sudan Kusini zilitia saini mkataba wa kusitisha vita Ijumaa iliyopita, lakini vita vimepungua tu bali havijasitishwa.Baadhi wanahofia kuwa hatua hii huenda ikasababisha uhasama zaidi na kutishia mkataba wa amani kati ya waasi na serikali.

Duru zinasema makabiliano yangali yanaendelea huku zaidi la watu 800,000 wakilazimika kutoroka makwao.
Mkuu wa misaada katika Umoja wa Mataifa,Valerie Amos, anakamilisha ziara yake ya siku tatu nchini humo ambako ameshuhudia vita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Wanaume wanne waliozuiliwa watafikishwa mahakamani na wengine watatu akiwemo Riek Machar, pamoja na mjumbe mmoja wa amani kutoka upande wa waasi,Taban Deng -- aliyetia saini mkataba wa amani watakabiliwa na sheria watakapokamatwa.
Rais Kiir alimtuhumu Machar pamoja na waliokuwa maafisa wa serikali kwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya serikali yake baada ya mapigano kuzuka mjini Juba mwezi Disemba mwaka jana.
Maafisa 11 wa zamani walikamatwa wakati Machar aliyepinga kupanga njama ya mapinduzi akitoroka.
Makabiliano mapya yameripotiwa kutokea katika jimbo la Unity karibu na anakotoka bwana Machar.
Wafanyakazi wa misaada wamesema kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu na kuwa wanahitaji msaada zaidi kuwasaidia waathiriwa wa mapigano hayo.