STAA wa filamu mwenye jina kubwa nchini, Wema Sepetu hivi karibuni
alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa
kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha
sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.
Wema Sepetu.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo aliliambia gazeti hili kuwa,
Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa
simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa
amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa haukuwa wa
kweli.Alisema kutokana na kutofika kwa staa huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi wageni wengine, wakiwemo waandishi wa habari.
Mmoja wa watu wa karibu na Wema aliliambia gazeti hili kuwa muigizaji huyo hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi karibuni, kwani mara zote amekuwa akiwaeleza kila linapotokea jambo zito kama hilo.
Mtu huyo alisema katika ratiba ya siku hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja la starehe na halikuwa limebadilika.
juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo alichosema kimemsikitisha kwani walitoa mwaliko kwake kutokana na heshima aliyonayo.
“Nimemshangaa sana, lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu anajitambua na ni professional,” aliema Myamba.