Serikali imetangaza kuwajiri walimu wapya 36,071 mwaka huu ambao majina yao yanatarajia kutangazwa katikati ya mwezi huu (Machi) na watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi Aprili mosi mwaka huu.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim
Majaliwa, aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha
Kumepambazuka jana kinachorushwa na Radio One.
Majaliwa alisema walimu hao watapangiwa katika vituo mbalimbali vya kazi
kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu na majina yatatoka katikati ya mwezi
huu.
Alisema kati ya walimu hao watakaoajiriwa, 36,020 wataajiriwa na
halmashauri za wilaya ambao ni walimu wa shule za msingi na sekondari na
51 watakuwa chini Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa
ajili ya vyuo.
Aliongeza kuwa kati yao, walimu wa stashahada ni 17,028 na 5,416 ni wa shahada kwa ajili ya sekondari na 12,677.
Alifafanua kuwa wanaoajiriwa ni wale waliohitimu hivi karibuni katika
vyuo vya ualimu na walimu wa masomo ya sayansi watapewa kipaumbele.
Majaliwa alisema tayari Wizara imewaagiza wakurugenzi wote wa
Halmashauri na maofisa elimu kupitia ikama ya walimu kubaini shule zenye
upungufu wa walimu ili walimu hao wapya wanaoajiriwa wapelekwe huko
hususani katika shule zilizopo vijijini.
Alisema kuajiriwa kwa walimu hao kumepunguza tatizo la upungufu wa
walimu 21,684 baada ya ajira hiyo na kwamba hata hivyo upungufu mkubwa
kwa walimu wa sayansi ni 26,212.
Alisema serikali imeweka mkakati wa kukabiliana na tatizo la punguza wa
walimu wa sayansi kwa kuwachukua wanafunzi waliohiotimu vyuo vikuu ili
wapelekwe kwenye vyuo vya ualimu.
Kuhusu tatizo la baadhi ya walimu kukimbia vituo vya kazi, alisema
kimsingi sheria ipo wakishaajiriwa wanakuwa katika kipindi cha matazamio
cha miaka mitatu na wanafanyiwa ukaguzi na wakaguzi ili kubaini kama
wana uwezo wa dhati.