Mhe. Angela Kizigha na Mhe. Faustine Ndugulile wakifanya mazoezi na klabu mwenyeji wa bonanza hilo, Magenge 20.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Mh Angella Kizigha akiongea na wanajogging wa bonanza hilo.
Mhe. Faustine Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni akipozi na Mgeni Rasmi, Angela Kizigha baada ya kupewa zawadi ya kikoi.
BONANZA la michezo la kila mwezi linalofanyika katika Uwanja vya
Burudani wa Dar Live Mbagala Zakhem limefanyika leo ambapo maelfu ya
wanamichezo wamejitokeza kushiriki bonanza hilo la aina yake.Wenyeji wa bonanza hilo walikuwa ni klabu ya Magenge 20 ya Mbagala Kiburugwa jijini Dar, ndiyo walikuwa wakizikaribisha timu zote zilizokuwa zimepewa mwaliko wa kushiriki bonanza hilo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa ni Mheshimiwa Angela Kizigha, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki aliyekuwa ameambatana na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na wanamichezo mbalimbali.
Licha mvua kubwa kunyesha lakini haikuweza kukata kiu ya wanamichezo waliokuwa wamejitokea kwani waliendelea kuserebuka ndani ya mvua bila kujali.
Hata hivyo burudani ya kufa mtu inatarajiwa kuangushwa jioni hii na bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Farasi’ chini ya Ally Choky ‘Mzee wa Ambulance’.
Vilabu zaidi ya 180 vya mbio za pole ‘Jogging’ vimeshiriki ambapo michezo mbalimbali bado inaendelea kufanyika.
Washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali za michezo katika bonanza hilo la kufuru, aidha Tamasha hilo limedhaminiwa na PSPF, Mpango wa Damu Salama, Global TV Online, Kampuni ya A-One watengenezaji wa maji ya Maisha, Global Publishers Ltd, Dar Live pamoja na Benki ya Akiba Commercial (ACB).