Pages

March 03, 2014

AL AHLY WASUSA VYAKULA, NI BAADA YA KIPIGO

Mohammed Mdose na Said Ally
KIPIGO cha bao 1-0 walichokipata Al Ahly dhidi ya Yanga, kimeonyesha kuwachanganya vilivyo Waarabu hao, kwani baada ya mchezo walionekana kutupatupa ovyo vyakula walivyokuwa navyo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Waarabu hao walikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, juzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa bao safi lililofungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Championi lilifanikiwa kupenya kwenye chumba walichokuwemo Al Ahly na kushuhudia matunda aina ya apple, ndizi na juisi vikiwa vimezagaa chini katika chumba hicho huku wachezaji hao wakiwa hawana muda navyo, kwani wengi wao walionekana kujadili kipigo hicho.
Championi lilijaribu kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kujua kwa kina chanzo cha mkasa huo, lakini walionekana kuwa na hasira na kugoma kuzungumza chochote.
Hali ilikuwa tofauti katika chumba cha timu ya Yanga ambamo wachezaji wake walikuwa wenye furaha muda wote huku wakipongezana.
Yanga na Al Ahly zinatarajiwa kurudiana mwishoni mwa wiki hii jijini Cairo.