Mtangazaji maarufu wa Runinga Bongo, Maimartha Jesse amejikuta
akiwekwa nyuma ya nondo kwa madai ya kumtapeli dada mmoja aliyetambulika
kwa jina la Zai, mkazi wa Zanzibar.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, mtangazaji huyo alilipwa pesa
ya kianzio cha shughuli ya u-MC visiwani humo mwezi mmoja uliopita
lakini akashindwa kwenda bila sababu za msingi.
“Kifupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
“Kifupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya siku ya tukio kupita na Maimartha kuingia mitini, chanzo
hicho kilisema Machi 4, mwaka huu, Zai alimfungia safari hadi Dar na
kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kumalizana.
Alipotafutwa Maimartha kuzungumzia juu ya sakata hilo, alitiririka:
“Imeniuma sana, kiukweli alinipa fedha za kianzio huyo dada (Zai) lakini
nilishindwa kwa sababu nilipata dharura, hata hivyo nimeshangaa
amekwenda kupandisha dau kule polisi tofauti na fedha ndogo aliyonipa,
sitaki kuongelea sana lakini nashukuru yameisha.”