LONDON, England
KOCHA
Manuel Pellegrini amefanikiwa kutwaa taji la kwanza akiwa bosi wa
Manchester City baada ya jana kuifunga Sunderland katika fainali ya
Kombe la Capital kwa mabao 3-1kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.
Kocha
huyo raia wa Chile ambaye yupo katika adhabu ya kukosa mechi tatu za
Ulaya baada ya kufungiwa na Shirisho la Soka la Ulaya (Uefa) kutokana na
kumtolea lugha kali mwamuzi, Jonas Eriksson, alikuwa na furaha jana
kutokana na ushindi huo.
Licha ya Sunderland kuanza kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya
10 kupitia kwa Fabio Borini, ilijikuta ikizidiwa nguvu na kupata kipigo
hicho kipindi cha pili.
Yaya Touré ndiye aliyefunga bao kali kwa
shuti katika dakika ya 55, wapinzani wao hao walijikuta wakipagawa na
kufungwa la pili dakika moja baadaye na Samir Nasri.
March 03, 2014
MAN CITY YATWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE
04:30:00
KIMATAIFA