Pages

March 02, 2014

TASWIRA ZA SALUM MKAMBALA AKIWA HOSPITALI YA TUMBI BAADA YA AJALI

Mtangazaji wa Channel 10, Salum Mkambala, akipelekwa Theatre katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Msanii wa kundi la Mizengwe, Hemed Maliyaga (wa kwanza kulia) akisaidiana na ndugu pamoja na mke wa Mkambala (wa tatu kushoto) kumpeleka mgonjwa Theatre.
...Mkambala akiingizwa Theatre.
HALI ya Mtangazaji wa Channel 10, Salumu Mkambala aliyepata ajali alfajiri ya leo kwa kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro inaendelea vizuri katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na mwandishi wetu hospitalini hapo, mdogo wa mtangazaji huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea Morogoro na alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri saa 10. 30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni kutokana na barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali iliyosababisha gari la kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.