BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba anaonekana kuendelea
kuwewesekea mali za mwanaye baada ya kuibuka na kudai kuwa, atampeleka
Segerea (jela) mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kwa madai kuwa amezifuja
mali za marehemu.
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kwa njia ya simu, baba Kanumba
alisema, ameona taarifa kwenye gazeti kuwa mali nyingi za marehemu
Kanumba zimeuzwa huku yeye akiwa hajaambulia chochote.
“Huyu mama Kanumba ana laana yangu, amefuja mali za mwanangu kwa
kushirikiana na Seth, mimi sijashirikishwa, nisipopata chochote
tutafikishana pabaya,” alisema mzee huyo.
Baba wa marehemu Kanumba, Charles Kanumba.
Kuhusiana na hilo, mama Kanumba huyu hapa: “Kwa mila za Kisukuma
Kanumba siyo mwanaye kwa kuwa hajanioa, hivyo kuhusu suala la mali kama
anazijua zinazomhusu aonyeshe moja baada ya nyingine hapo itakuwa sawa.”
March 07, 2014
BABA KANUMBA: NITAMPELEKA MAMA KANUMBA SEGEREA
00:40:00
WASANII