KUNDI la watu waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni mjini Kunming, China!
Mashahidi wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao waliovalia nguo nyeusi, waliwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Polisi walifanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya shambulio hilo.
Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo.