Dodoma.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo
Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya
chama au ya kundi la watu wachache.
Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu
ya watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu wakiingia katika
uchaguzi, wataangushwa na Sitta.
“Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu
binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa
kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa
mazuri mbele yake,” alisema Lissu.Alisema katika kipindi ambacho
aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza
kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.
Akizungumzia tetesi kuwa Mwanasheria Mkuu wa
zamani, Andrew Chenge ameonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo, alisema
hayuko tayari kumuunga mkono.
Lissu alisema Chenge hataweza kuliongoza Bunge hilo na kwamba kama atachaguliwa, litavunjika likiwa mikononi mwake.
Kuhusu Samia Suluhu Hassan anayetajwa kuwania
nafasi ya Makamu Mwenyekiti , alisema hana shaka pia ingawa hajaonyesha
makeke yake mbele ya vikao muhimu kama vya Bunge, lakini ni mzoefu wa
muda mrefu serikalini na katika nafasi mbalimbali.