Pages

March 11, 2014

MADEREVA WATWANGANA KWA KUTOELEWANA BARABARANI


Madereva Juma na John wakichapana makonde hadharani.
…Akiokota jiwe kumshushia kipigo John aliyedaiwa kutaka kusababisha ajali.
Juma (kulia) akirusha matusi kwa John.
Dereva Juma akimshusha John kutoka kwenye gari lake.
 Watu wakijaribu kumzuia Juma asimshushie kipondo John.
Vidume hao wakiangaliana baada ya kuzipiga.
Gari  la Kulwa.
Daladala lililokuwa likiendeshwa na Hamis.
DEREVA wa daladala Juma Hamis na John Kulwa aliyekuwa na Toyota Canter wamenaswa na kamera yetu wakichapana makonde hadharani pande za Mwenge jijini Dar, kwa kutoelewana.  Hamis alikuwa akiendesha daladala linalofanya safari zake kati ya Kunduchi na Mwenge lenye namba za usajili T 968 AGP ambapo Kulwa alikuwa na gari aina ya Toyota Canetr namba za usajili T945 AM.

CCM YAPULIZA KIPYENGA CHALINZE

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.

MWANACHUO AUAWA KWA RISASI

Jeneza lenye mwili wa Dorryce Lwena.
MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa marehemu huyo.
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha…
Stori: Makongoro Oging’ na Harun Sanchawa
MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.
Jeneza lenye mwili wa Dorryce Lwena.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa marehemu huyo.
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Singida (DSA), alikuwa akitoka Kariakoo kununua vifaa vya kwenda navyo chuo siku mbili mbele lakini kifo kilimkuta akiwa anakaribia kufika nyumbani.
Mama mzazi wa Dorryce akiwa na simanzi wakati wa mazishi ya mwanaye.
Kama ilivyo ada, baada ya kujulishwa tukio hilo la kikatili, waandishi wa Uwazi walifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na baba wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye baada ya baba mzazi kutengana na mama yake.
Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alikuwa na haya ya kusema:
“Ilikuwa Jumamosi, Machi Mosi, mwaka huu, saa tatu usiku nikiwa karibu na kwangu, mke wangu (mama wa marehemu) alinipigia simu akaniambia kuna risasi zimepigwa karibu na nyumba yetu, nikamwambia haraka sana wafunge milango na mtu asitoke nje hadi itakapojulikana kuwa risasi hizo zilikuwa za nini.
Ndugu na jamaa wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi.
“Muda mfupi baada ya kuongea na mke wangu, dada wa Dorryce alinipigia simu akiniambia nirudi nyumbani haraka kwani Dorryce amepigwa risasi na amefariki dunia.
“Nina gari, niliingia ndani yake haraka tayari kwa safari ya kurejea nyumbani. Nikiwa nakaribia nyumbani niliona kundi la watu, nilisogelea eneo hilo na kukuta mwili wa Dorryce umelala katika dimbwi la damu.
“Nilikuta familia yangu, akiwemo mama wa marehemu wakilia kwa uchungu. Iinibidi nikatoe taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kitunda, nao walinishauri niende Kituo cha Polisi Stakishari.

“Polisi walifika eneo la tukio na kufanya michoro kisha wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Mke wangu ana hali mbaya sana jamani. Tangu tukio hilo amekuwa akizimia mara kwa mara, presha inapanda na kushuka. Naombeni msimhoji,” alisema kwa masikitiko makubwa baba huyo.
Alisema mpaka siku hiyo familia ilikuwa haijui chanzo cha mauaji hayo.
Akasema: “Ninachokumbuka mimi siku hiyo mke wangu alimkataza marehemu asiende Kariakoo lakini alikataa, akasema kwa vile Jumapili atakwenda kanisani na Jumatatu ndiyo safari ya kurudi chuo, afadhali aende siku hiyo.”
“Ila wakati marehemu yupo chuoni alizaa na mwanaume mmoja ambaye tulimtaka amhudumie mtoto kwa vile mama yake bado anasoma lakini alikataa, hivyo marehemu aliamua kumchukua mtoto na kumpa. Hadi hapo tukawa hatuna uhusiano naye mzuri,” alisema mzee huyo.
Waandishi wetu walifanya mahojiano na majirani kutaka kusikia kama wanajua lolote juu ya tukio hilo ambapo baadhi yao walisema mauaji hayo hayajawahi kutokea eneo hilo na kudai kwamba marehemu  ndiye anayejua sababu ya kupigwa risasi.
“Marehemu baada ya kupigwa risasi ya kwanza alilia kwa uchungu na kupiga kelele kuomba msaada. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza.
“Aliongezwa risasi ya pili sauti yake haikutokea tena, wale watu walitimka na pikipiki ndipo wananchi tukajitokeza, nahisi ni mapenzi,” alisema mwanamke mmoja anayefanya biashara karibu na eneo la tukio.
Baba mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Julius Jacob Lwena anayeishi Tabata Tenge, Dar yeye alikuwa na haya ya kusema:
“Kifo cha Dorryce kimeniuma sana, ila napenda kusema kwamba maisha yake kwa undani siyajui sana kwa sababu nilikuwa mbali naye.
“Mara ya kwanza marehemu alipomaliza elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi, alirudishwa kutokana na ujauzito.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka Chuo cha Utumishi Singida, bahati mbaya akapata mimba ya mwanaume mwingine, ikabidi arudi nyumbani.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka chuo cha uhasibu Singida na mauti yamempata alipokuja likizo,” alisema mzee huyo.
Marehemu alizikwa Machi 4, mwaka huu katika Makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

MFAHAMU PASTA ANAYEHUBIRI KANISANI HUKU AKIWA NA NYOKA SHINGONI



Pasta anayejulikana kuhubiri akiwa amemweka nyoka shingoni ameaga dunia. Pasta Jamie Coots anayeamini kuwa kinga hutoka kwa mungu aliweza kupoteza maisha yake baada nyoka huyo wa sumu kumuuma akiwa akihubiria mbele ya maumini.
Ilikuwaje hadi pasta huyo kuhubiri na nyoka mgongoni?

Kupitia andiko la Marko 16:15-18, pasta huyo anaamini kuwa Yesu aliweza kuwaambia wakristo wote kuwa wanaweza kushika nyoka na hatawaumiza wala kuwadhuru bora tu uwe umebarikiwa na mungu mwenyewe.

Pasta huyo wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name aliumwa na nyoka huyo mbele ya kanisa lake na ilimbidi kukimbizwa hadi nyumbani kwake bila kupelekwa hospitalini.

Wauguzi walipowasili nyumbani kwake waliweza kufukuzwa huku pasta huyo akiwa na imani kuwa mungu atamtibu ugonjwa wake, jambo ambalo halikufanyika.

MAHEKALU YA MAASKOFU KUFURU


Stori: Jelard Lucas na Makongoro Oging’
MTU akifanya jambo la kupita kawaida lakini zuri watu husema ‘amekufuru’, yaani amefanya kitu kizuri! Imezoeleka hivyo. Sasa kauli hiyo imekuja baada ya Uwazi kufanya uchunguzi wa kina na kuyabaini mahekalu ya maaskofu wa Bongo kwamba nayo ni kufuru!
Ghorofa analomiliki Mwingira.
Katika uchunguzi huo, Uwazi lilitumia muda wa wiki mbili na kubaini kwamba, watumishi hao wa Mungu wapo vizuri na lile neno wanalolihubiri kwamba, kwa Mungu kuna raha, kwa Mungu kuna maisha mazuri na mtu akiyataka ampokee Bwana!
Nabii Mwingira.
UCHUNGUZI ULIPOANZIA
Uchunguzi ulianzia kwa askofu mkuu au Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Ngurumo ya Upako (N.Y.U) lenye maskani yake jijini Arusha ambapo yeye anadaiwa kuwa na jumba kubwa analoishi na familia yake ndani ya jiji hilo na eneo hilo kupewa jina la ‘Mji wa Daudi’. Huyu amewafunika wenzake kwa ubora wa mjengo na pia utajiri alionao.
Ghorofa la Gwajima.
Habari zinasema mjengo wake huo una mandhari ya kiikulu ukilinganisha na mahekalu ya watumishi wenzake ambao wametajwa kumiliki pia.
Kwa mujibu wa chanzo, mjengo wa nabii huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuwa na mfumo wa kiutawala kama ule wa wanasiasa, unapatikana katika Kitongoji cha Njiro, Arusha.
Mchungaji Gwajima.
“Sijawahi kuona askofu au nabii anamiliki jumba la kifahari kama lile, lile ghorofa la ofisi tu pia ni balaa. Tena basi ameweka ulinzi mkubwa sijawahi kuona. Nilibahatika kupata picha ya sebuleni kwake utadhani ikulu. Pia niliwahi kuiona ofisi yake jamani! Jamani! (chanzo kinashangaa).
OFISI ZAKE ANAZIITA STATE HOUSE
 Chanzo kiliendelea kudai kuwa, ofisi za nabii huyo ni maarufu kwa jina la ‘state house’ (ikulu) ambapo pia hapo analindwa kama enzi za akina Mfalme Daudi ndiyo maana hata sehemu anayoishi panaitwa Mji wa Daudi.
MBALI NA HEKALU
Kwa Nabii Geordavie, mbali na kumiliki utajiri ambao umewahi kuandikwa na gazeti hili siku za nyuma, lakini imebainika kwamba ana kituo cha redio kinachojulikana kwa jina Ngurumo ya Upako FM chenye makao yake jijini Arusha.
MAHEKALU YA WENZAKE
Nyumba za maaskofu wengine ambao walizukiwa na Uwazi ni ile ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry, Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Zakary Kakobe International Ministry (zamani Full Gospel Bible Fellowship ‘F.G.B.F’).
Maaskofu wengine ni Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ wa Kanisa la Maombezi (G.R.C) Ubungo -Kibangu, Mchungaji Kiongozi Getrude Rwakatare wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni ‘B’ na Mchungaji Christopher Mtikila wa Kanisa la Salvation Church, wanatajwa kumiliki mahekalu mazuri nchini.
MCHUNGAJI GWAJIMA  
Mchungaji Gwajima hakamatiki kama Geordavie, kwani anatajwa kuwa na mjengo wenye ghorofa nne maeneo ya Salasala jijini Dar. Gwajima maarufu kwa kurudisha misukule, pia anamiliki magari ya kifahari achilia mbali mabasi yanayotumika kubeba waumini wake kwenda kanisani Kawe jijini Dar.
NABII MWINGIRA
Licha ya kuandamwa na skendo, Nabii Mwingira anamiliki jumba la ghorofa moja Mikocheni B, jijini Dar. Ina ulinzi balaa. Eneo kubwa la jumba hilo ni matumizi ya familia yake.
Pia Mwingira anamiliki Benki ya Efatha iliyopo Mwenge jijini Dar. Anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu mabilionea sanjari na baadhi ya viwanja na mashamba anayomiliki.
MAMA RWAKATARE
Mama Rwakatare, wengi humwita ‘Mbaya’. Ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa kujenga nyumba mbili za kisasa, moja ipo Mikocheni B ikiwa na ghorofa moja na Mbezi, Dar yenye ghorofa moja.
MCHUNGAJI MTIKILA
Mchungaji wa Kanisa la Salvation Church, Christopher Mtikila yeye anatajwa kumiliki hekalu moja maeneo ya Mikocheni B jijini Dar likiwa na ghorofa mbili.
MZEE WA UPAKO
Mzee wa Upako ni Mchungaji wa Kanisa la GRC, ni kama Mwingira tu, yeye anamiliki mjengo wa ghorofa moja uliopo Ubungo Kibangu jirani kabisa na kanisa lake.
Mchungaji huyo anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu walio vizuri kimaisha. Mzee wa Upako aliwahi kula kiapo katika moja ya vyombo vya habari (jina kapuni) kuwa kwenye maisha yake haamini katika umaskini kwani umaskini siyo sifa nzuri.
ASKOFU KAKOBE
Askofu Kakobe (I.M) anatajwa kumiliki nyumba ya kawaida sana pale Mpakani B, Kijitonyama Dar. Nyumba yake haina ghorofa. Aliwahi kuburuzana mahakamani na baadhi ya waumini kwa madai ya hati miliki ya kanisa.
Jumamosi iliyopita waandishi wetu walifika nyumbani kwake na kubahatika kuzungumza na majirani ambao wengi walikuwa na swali moja ni kwa nini Kakobe hateremshi hekalu la kisasa ilihali fedha anayo?
KUWAPATA ISHU
Miongoni mwa watu wagumu kupatikana na kuzungumza na wanahabari ni watumishi hao wa Mungu ambapo wote walipotafutwa kwa njia zote, simu na kufuatwa makanisani mwao hawakupatikana.
Kuna wakati Mchungaji Lusekelo aliwahi kuulizwa ni kwa nini hawapatikani, alisema hata Yesu alikuwa hapatikani kirahisi!!

MARANDO: BABU SEYA ALIBAMBIKIWA KESI

Na Elvan Stambuli
WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.

Mabere Nyaucho Marando akiongea na waandishi wa Global Publishers (hawapo pichani).
Akizungumza na waandishi wa habari wa Global Publishers katika ofisi zao zilizopo Mwenge Bamaga mwishoni mwa wiki iliyopita, Marando alisema alipitia jalada la kesi hiyo lenye kurasa 1,362 na kugundua kuwa hakuna hata sehemu moja inayomhusisha kigogo mmoja wa nchi, lakini kesi walikuwa wamebambikiwa.
Hakutaja waliombambikia. Baadhi ya mahojiano ya Marando na waandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Marando: Kuna rafiki yangu alikuja kuniomba nifanye kazi ile, nilikataa hasa kwa kuwa nami nina watoto wa kike. Baadaye nilikubali kwanza kusoma jalada la kesi lenye kurasa 1,362 nikaona hawakufanya makosa waliyoshitakiwa, walibambikiwa nikaamua kuwatetea katika ngazi ya rufaa, niliwatetea bure kabisa.
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?
Marando: Ndiyo, naamini makosa yale walibambikiwa lakini siyo na kigogo yeyote wa serikali katika nchi hii. Lakini Mahakama ya Rufaa haina makosa, Babu Seya na wanawe walikuwa wamehukumiwa na magazeti. Nyinyi waandishi mlimhukumu kwa hii fabricated case (kesi ya kutunga) na sababu zipo.
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?
Marando: Mimi kama wakili, hapo ndiyo mwisho wangu, nimenyoosha mikono. Nimeshindwa nusu, nimeshinda nusu (Kwa kuwatoa jela Mbangu na mdogo wake Francis Nguza na kubaki jela Nguza na Papii.)
Mwandishi: Umekuwa Chadema na kuna habari kuwa uliondolewa kuwa mwanasheria wa chama akapewa Tundu Lissu,pia kuna habari kuwa umekosana na mwenyekiti wako, Freeman Mbowe, Je,  kuna ukweli wowote juu ya hayo?
Marando: Sijawahi kuwa mwanasheria wa Chadema isipokuwa wanapokuwa na tatizo la kisheria huwa nawapa ushauri wakihitaji. Mheshimiwa Mbowe sijakosana naye isipokuwa katika vikao tunaweza kutofautiana na hivyo ndivyo chama makini kilivyo. Wote hamuwezi kuwa na wazo moja katika hoja, baadaye inapigwa kura, upande unaoshinda na unaoshindwa huwa kitu kimoja. Hakuna ugomvi hapo, mimi ni Makamu  Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu.
Mwandishi: Lipo suala kuwa wewe ni usalama wa taifa na ulihusika na mauaji ya Komandoo Tamim, Je, hilo unaweza kulifafanua?
Marando: Mimi nilijiunga na usalama wa taifa na nilikuwa kitengo cha mambo ya nje hasa kuhusu vyama vya ukombozi enzi hizo. Niliacha kazi hiyo kwa kukabidhi barua kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Dk. Hansy Kitime baada ya kulazimishwa kujiunga na TANU kwani sikuwa mwanachama. Kuhusu Tamim aliuawa mwaka 1983 wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kazi.
Hili la kuua walikuwa wakinipakazia watu wa usalama wa taifa bila shaka kwa sababu niliacha kazi kijeuri nikawa jobless (sina kazi).
Baadaye nikaajiriwa Shirika la Sheria Tanzania kabla ya kuanzisha kampuni yangu ya uwakili mwaka 1984. Nimefafanua hili mara nyingi sana, nadhani leo mmenielewa na Watanzania watanielewa.

March 07, 2014

Ngumi mkononi bungeni


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Magdalena Sakaya (kushoto), akizozana na Magdalena Likwina baada ya Semina ya Kupitia Vifungu vya Rasimu ya Kanuni kuahirishwa kutokana na vurugu zilizotokea bungeni jana. Picha na Silvan Kiwale  

Dodoma.
 Ngumi mkononi ndilo neno jepesi ambalo linafaa kutumika baada ya vurugu kubwa kutokea jana ndani ya Ukumbi wa Bunge Maalumu la Katiba kiasi cha kumlazimisha Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho kuahirisha semina kabla ya wakati wake.
Semina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, imekuwa ikianza saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana kabla ya kuendelea tena kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 3:00 usiku. Jana, katika kipindi cha asubuhi, semina hiyo iliahirishwa saa 6:17 licha ya kuanza saa tano asubuhi kabla ya kurejea tena saa 10 jioni.
Ngumi zilitaka kupigwa baada ya Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakari Hamis Bakari kuhoji uhalali wa Christopher Ole Sendeka na Ummy Mwalimu kuchangia wakati hawakuwamo katika orodha ya wachangiaji jambo ambalo liliibua mjadala mkali na kurushiana maneno kabla ya Mwenyekiti Pandu Ameir Kificho kuahirisha semina hiyo.
Chanzo cha vurugu
Kificho alimpa Ole Sendeka nafasi ya kuchangia Kifungu namba 58 cha rasimu ya kanuni na baada ya kutoa mchango wake, Hamisi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kanuni, alisimama na kumtaka Mwenyekiti Kificho kuacha kuwateua watu ambao hawamo katika orodha ya wachangiaji.
Kificho hakumsikiliza na badala yake, alimpa nafasi mjumbe mwingine wa Bunge hilo Ummy Mwalimu ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuchangia. Hata hivyo kabla hajafanya hivyo, Bakari alisimama tena na kumzuia kuchangia kwa madai kuwa hakuwamo kwenye orodha ya wachangiaji.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaendelea na utaratibu huu suala la kuchangia kanuni linaweza kutupeleka hadi miezi sita bila ya kumaliza. Haya majina hayakuwemo kwenye orodha ya wachangiaji na huyo aliyemaliza sasa Ole Sendeka, naye hakuwamo, naomba tuache mchezo huu,” alisema Bakari.
Aliendelea: “Sekretarieti inakuchomekea majina mwenyekiti na kama hivyo ndivyo, basi tunatakiwa kuwachukulia hatua kali hawa kwani tunataka kujadili hoja ambazo hazimo.”
Bakari alisema wajumbe waliotakiwa kuchangia ni wale ambao walipeleka majina kwa makatibu wa Bunge hilo pamoja na michango yao kwa maandishi ili wapewe nafasi ya kuzungumza, lakini Kificho alikuwa akiwateua wajumbe ambao hawamo katika orodha hiyo.
Kificho ajibu
“Mimi sina tatizo na jambo hilo, mkisema tuendelee basi sawa, lakini mkitaka tufanye mambo kwa uzuri inawezekana pia, jambo la muhimu ni kuwa tupo hapa kutengeneza Katiba ya wananchi siyo ya vyama.”
Kelele zilianza kusikika huku wajumbe wakiimba kuwa mwenyekiti anayumba… na kumtaka mwenyekiti atoke nje na kukiacha kiti, kwani anafanya upendeleo.

Kelele hizo ziliambatana na wajumbe hao kuwasha vipaza sauti bila utaratibu. Mjumbe Sadifa Juma Khamis ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasha kipaza sauti chake na kusimama wakati wote akisema anataka kuchangia, huku akiungwa mkono na wajumbe wengine kadhaa.
Kutokana na tukio hilo, Kificho alilazimika kumwita Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Profesa Costa Mahalu ambaye alikiri kuwa yako majina ambayo hayakuwamo kwenye orodha, lakini kwa mwenyekiti yalionekana.
Moto zaidi uliwaka baada ya Ole Sendeka kusimama hata bila ya kupewa nafasi na kusema anazijua kanuni vizuri na kwamba asingeweza kuzivunja.
“Nilijua hayo yote na mimi siyo dhaifu wa kanuni kwani najua kila kitu na tulikwenda tangu mwanzo; mimi, Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Peter Serukamba, ndiyo maana majina yetu yamo humo ila kama mapigo yetu yanawakwaza wengine waseme, siyo jukumu la mimi kupeleka mapendekezo yangu kwa Bakari, labda kama wewe una msimamo wako na chama chako,” alisema Ole Sendeka.
Kauli hiyo ilizusha kelele za wajumbe ndani ya ukumbi, huku Kificho akiwatuliza na kusema Ole Sendeka aliteleza ulimi na kumtaka aombe radhi kama anataka, lakini mjumbe huyo aligoma kwa kuonyesha ishara ya mikono, jambo ambalo lilimfanya Bakari kusimama tena.
Bakari alisimama na kueleza uzoefu wake wa miaka 34 kwenye Bunge akijisifu kuwa yeye ni zaidi ya Ole Sendeka.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sihitaji kuombwa msamaha na Ole Sendeka, nimekuwa kwenye mabunge haya tangu mwaka 1980, leo hii mtu kutoka Simanjiro miaka 10 iliyopita hawezi kunitisha,” alisema Bakari.
Wengine nusura wapigane
Kauli hiyo iliwafanya wajumbe wengi bungeni kusimama, huku wengine wakitaka kupigana ngumi baadhi wakisema: “Twende nje tukapigane, twende nje tukapigane…”
Waliokuwa wakibishana zaidi ni Abdalla Sharia ambaye alitaka kupigana na Khatibu Haji kabla ya kuzuiwa na wenzao, huku Tauhida Nyimbo akitaka kuzikunja na Seleman Bungara (Bwege).
Wakati Bunge likiwa limechafuka na kukiwa na kelele nyingi, mwandishi wa habari hizi alimuona, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda akimuonyesha kwa ishara ya mikono Kificho kuahirisha semina.
“Naahirisha semina hii mpaka saa kumi jioni,” alisema Kificho na kuwafanya wajumbe kupiga kelele huku wengine wakishangilia na baadhi wakiguna.
Nje ya ukumbi
Wakiwa nje ya ukumbi, Ole Sendeka alisema hoja zake ni nzito na haziwezi kuzimwa na Bakari ambaye anaonekana kuwa na masilahi binafsi.
Alisema yeye pamoja na wenzake (Ummy na Serukamba), bado wanatarajia kuwasha moto kwa kila kifungu ili mambo yaweze kukaa vizuri na kuwa kilichotokea kwake ni burudani.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema tatizo kubwa lililosababisha mambo hayo ni misimamo ya mwenyekiti kuyumba wakati wote.
Hata hivyo, alilaani kitendo cha wajumbe wengine kuwa na hoja alizoziita za kitoto kwa kuzomeazomea akisema hata kama kiti kinayumba, bado walipaswa kuwa watulivu na kuangalia kilichowapeleka Dodoma.
Mjumbe mwingine, Charles Tzeba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, alitetea kauli ya Sendeka na kusema hata kama hakuwa kwenye orodha alipaswa kuchangia kwani hiyo ilikuwa ni semina ambayo kila mtu anayo haki ya kuchangia wakati wowote.
Bunge liliporejea jioni, wajumbe wawili-James Mbatia na Profesa Mark Mwandosya walisimama na kutoa nasaha za kutuliza jazba pale wajumbe wanapokwaruzana, huku Mwenyekiti Kificho akisema kilichotokea asubuhi kilitokana na yeye kutokujua kwamba baadhi ya wajumbe hawakuwa katika orodha.

BABA KANUMBA: NITAMPELEKA MAMA KANUMBA SEGEREA

http://api.ning.com/files/BrAPCEwtvYDNlrlYwAb0FlxzgXMaaorbIDZlHTjKWPHV0Xvq1g*W6OqvzSs2cy2sJ7XYhr8r1y1mE5svyJwDilEhD38B*TMe/BabaKanumba2.jpg?width=640
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba anaonekana kuendelea kuwewesekea mali za mwanaye baada ya kuibuka na kudai kuwa, atampeleka Segerea (jela) mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kwa madai kuwa amezifuja mali za marehemu.
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kwa njia ya simu, baba Kanumba alisema, ameona taarifa kwenye gazeti kuwa mali nyingi za marehemu Kanumba zimeuzwa huku yeye akiwa hajaambulia chochote.
“Huyu mama Kanumba ana laana yangu, amefuja mali za mwanangu kwa kushirikiana na Seth, mimi sijashirikishwa, nisipopata chochote tutafikishana pabaya,” alisema mzee huyo.
Baba wa marehemu Kanumba, Charles Kanumba.
Kuhusiana na hilo, mama Kanumba huyu hapa: “Kwa mila za Kisukuma Kanumba siyo mwanaye kwa kuwa hajanioa, hivyo kuhusu suala la mali kama anazijua zinazomhusu aonyeshe moja baada ya nyingine hapo itakuwa sawa.”

MAIMARTHA ATIWA MBARONI, KISA....!

http://api.ning.com/files/8zXnpLXRQW*WYyyeVLC26vD-Xfv1PinufUy7VKkdxJF9F0s*uKrs2MFKZLpWvAgLOO4duNZvqQrKDx5curmpIEYKGynnLMGQ/Maimartha.jpg


Mtangazaji maarufu wa Runinga Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiwekwa nyuma ya nondo kwa madai ya kumtapeli dada mmoja aliyetambulika kwa jina la Zai, mkazi wa Zanzibar.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, mtangazaji huyo alilipwa pesa ya kianzio cha shughuli ya u-MC visiwani humo mwezi mmoja uliopita lakini akashindwa kwenda bila sababu za msingi.
“Kifupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya siku ya tukio kupita na Maimartha kuingia mitini, chanzo hicho kilisema Machi 4, mwaka huu, Zai alimfungia safari hadi Dar na kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kumalizana.
Alipotafutwa Maimartha kuzungumzia juu ya sakata hilo, alitiririka: “Imeniuma sana, kiukweli alinipa fedha za kianzio huyo dada (Zai) lakini nilishindwa kwa sababu nilipata dharura, hata hivyo nimeshangaa amekwenda kupandisha dau kule polisi tofauti na fedha ndogo aliyonipa, sitaki kuongelea sana lakini nashukuru yameisha.”

DIAMOND: NAJUTA KUWA STAA

Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Exclusive Interview! Staa anayeuza zaidi kwa sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefungukia skendo ambazo zimekuwa zikimtafuna kila kukicha huku akieleza kuwa, sasa anajuta kuwa staa.


Akizungumza na paparazzi wetu katika mahojiano maalum wiki hii, Diamond alisema kuwa amekuwa akivumilia mengi ambayo yanaelekezwa kwake lakini sasa imefika wakati yanamuumiza kwani naye ni binadamu, ana moyo wa nyama na siyo chuma.
Penny.
Ni kweli unatumia ndumba kutafuta mafanikio?
Diamond: “Baadhi ya watu wanakuwa na imani hizo kuwa mimi natumia mambo ya kishirikina kutafuta mafanikio lakini kwa wasiojua ni kwamba kila nifanyalo namtegemea Mungu na muongozo wa mama yangu mzazi (Sanura Kassim a.k.a Sandra).

“Hao ukijumlisha na jitihada zangu mwenyewe na kujituma sana ndiyo wanaonifanya niwe hapa nilipo leo.
“Si kwa sababu ya mambo ya kishirikina. Kwanza siamini katika ushirikina.”
Wema.
Hili la mama Wema Sepetu kudai umemloga Wema likoje?
“Sijawahi kumsikia mama Wema akisema nimemloga Wema na hata kwenye magazeti sijaona ila siku nikimsikia ndiyo naweza kusema chochote juu ya hilo.”

Unazungumziaje madai ya wizi wa nyimbo za wasanii wenzako?
Diamond: “Kwa hatua niliyofikia mimi si mtu wa kuiba wimbo wa mtu, bali wapo baadhi ya watu wanaopenda kunisukumia skendo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

“Wakati mwingine wanaotuponza ni maprodyuza ambao huenda siku za nyuma walitengeneza biti kali kwa ajili ya msanii fulani, msanii huyo akaingia mitini.
Jokate.
“Siku unakwenda studio kwake anakusikilizisha biti hiyo na ukiiona kali anakuambia uilipie utengeneze ngoma.
“Baadaye ndiyo unasikia msanii mwingine anaibuka na kusema kaibiwa biti au wimbo. Sasa hapo kosa ni la nani?

Kwa nini una msururu wa mademu?
Diamond: “Mimi ni Sukari ya Warembo na ni kweli baadhi nilikuwa nao kwenye uhusiano lakini wengine ni maneno ya watu tu, sijawahi kutoka nao.

“Kuna ambao wanajitafutia umaarufu kupitia kwangu kwa kusema nimetembea nao lakini siyo kweli. Si unajua ukizungukwa na uaridi na wewe unanukia uaridi? Ndivyo hivyo, wapo baadhi wanajitangazia tu ili wapate umaarufu.”
http://api.ning.com/files/lHZphyruYBmuTkGYhwKk0vclpSoZ3gL7eQFFZsz-kesjUnFLWfEkx27*wFJElo8Sv5drP2jqhSZDIYQdZE27ZJX-M3jLNASE/peteyafreemasons.jpg
Baadhi ya warembo ambao tayari ameshaelezwa kutoka nao kimapenzi ni pamoja na Rehema Fabian, Pendo Maisha Plus, Jacqueline Wolper, Natasha, Najma Shaa, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Unazungumziaje U-freemason wako?
Diamond: “Mimi siamini juu ya imani hiyo kabisa na sijui kama ipo. Huenda mavazi wakati mwingine yanafanya watu wanahisi hivyo. Kama ni mafanikio niliyonayo, yanatokana na kazi zangu za muziki ambazo kila mmoja anaona.

“Naweza kusema napata shoo nyingi ambazo nalipwa pesa nyingi na mimi situmii pesa yangu kwa anasa. Nawekeza ili baadaye mali zinisaidie nitakaposhuka kimuziki. Huwezi kuwa juu muda wote hivyo ni lazima niwe na tahadhari.”
Ni kweli unawapa mademu mimba kisha kuwatosa hivyo wanachoropoa?
Diamond: “Mabinti wanaoibuka na kusema nimewapa mimba ni walewale wanaotafuta umaarufu ‘kick’ kupitia mimi. Ndiyo maana kuna yule aliyeibuka na kuandikwa na magazeti lakini baadaye alikanusha mwenyewe.

“Najiheshimu na namjua Mola, najua kufanya hivyo ni sawa na kuua.”
Kwa mujibu wa Diamond, kumekuwa na baadhi ya wasanii wenzake ambao wamekuwa wakimchonganisha na mastaa wenzake, mfano ukiwa ni hivi karibuni ambapo alizushiwa kumkandia Ali Kiba ili waingie kwenye bifu.

MAINDA AKUMBUKA PETE ALIYOVISHWA NA MAX

Ruth Suka ‘Mainda’.
STAA  wa filamu  za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
 
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
“Asante Saidi kwa sababu ulionyesha kuwa una malengo makubwa na mimi mpaka  sasa ningekuwa naitwa Mrs, upendo wako kwangu bado upo sanaa ila hilo ulilolianzisha kwenye kidole changu japo ndoto haikukamilika kupitia wewe litatendeka, asanteni wote mlioshiriki siku ya hili tukio akiwemo Nina na Dotnata,” aliandika  Mainda.

March 06, 2014

Baada ya Rais Museveni Kupitisha Sheria kali Dhidi ya Mashoga na Wasagaji, Binti wake Ajitangaza kuwa Msagaji.

Imeelezwa kwamba habari hiyo ilianzia kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani itwao Abril Uno, ambao uliandika habari hiyo wiki iliyopita siku yaJumatano.

Kwenye tarifa yake mtandao huo ulitania kwa kuandika kwamba Diana Kamuntu, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amejitangaza kuwa ni msagaji kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio.

lesbian
Taarifa hiyo ilisema: “Mimi ni msagaji, ninafanya mapenzi ya jinsia moja. Nimelijua hilo toka nilivyokuwa msichana mdogo,” taarifa ilimnukuu Kamuntu.
Kwenye mtandao wa Abril Uno ulimtaja muendesha kipindi wa redio hiyo James Kasirivu, kuwa ndiye aliyekuwa akifanya mahojiano hayo, na kusema kwamba “alipatwa na mshangao na mpaka aliishiwa na maneno ya kuongea toka kinywani mwake.”
Maelezo hayo yalisambaa kwenye mitandao mingi Duniani, huku wengine kuitoa na wengine kuiacha.
Watu wengi waliguswa na taarifa hiyo huku baadhi yao wakiandika kwenye kurasa zao za Twitter katika hali ya kumuunga mkono Kamuntu:
Abril Uno, ni jina lenye maana ya ’1 April’ kwa Kihispania, ambayo ni siku ya wajinga.
Hivyo akili Kichwani Mwako.

Matukio Katika Picha Wakati Bunge Maalumu la Katiba Lilipohairishwa Leo Mjini Dodoma kutokana na Vurugu.


 Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa  kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
bunge2
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima Mdee akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa kwa muda mjini Dodoma leo kufuatia sintofahamu iliyokea
bunge4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd  (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa  muda leo kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa TanzaniaFrederick Werema.
bunge5
Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema.

CHADEMA Kumtangaza Mpinzani wa Ridhiwani Kikwete Jimbo la Chalinze.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mchakato wa kutafuta mgombea wa kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Chalinze, ambapo jana fomu za kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho zilianza kutolewa.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishaanza mchakato wa kutafutia mgombea wa kuwania nafasi hiyo, ambapo Ridhiwani Kikwete, alishinda kura ya maoni ya wanachama wa chama hicho na sasa anasubiri uamuzi ya vikao vya juu vya chama hicho.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Uhusiano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema fomu hizo zinatolewa na kurejeshwa katika ofisi za Kanda ya Pwani ya chama hicho.
“Baada ya kurejesha fomu, walioomba kuwania nafasi hizo watapigiwa kura ya maoni na wanachama wa Chadema wa eneo husika, na baada ya hapo uamuzi wa mwisho utakuwa ni wa vikao vya juu,” alisema Makene.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Uenezi wa Halmashauri ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, alisema bado chama hicho kipo kwenye mchakato wa kuandaa vikao vya juu, vitakavyoyachuja majina ya waliopigiwa kura za maoni na kuteua mgombea wa ubunge kupitia chama hicho.
“Tarehe rasmi ya vikao hivi vya juu bado haijapangwa, ndio tuko kwenye mchakato tukikamilisha tutawajulisha,” alisema Nape.
Juzi Ridhiwani alishinda kura ya maoni ya kumpata mgombea wa CCM katika jimbo hilo baada ya kupata kura 758, akifuatiwa na Shaban Madega aliyepata kura 335, Athuman Maneno kura 206 na Changwa Mkwazu aliyepata kura 12.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo la Chalinze, unatarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu na Machi 12, vyama vya siasa vitawasilisha majina ya wagombea wake kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao.
Kampeni rasmi za uchaguzi huo zitaanza Machi 13, mwaka huu. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo kufariki dunia.

SETH: KANUMBA ANANITOKEA

Joseph Shaluwa na Erick Evarist
SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo ya kushangaza, akidai kaka yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.
Marehemu Steven Kanumba.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa Kampuni ya Kanumba The Great Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 07,2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth alisema: “Kiukweli sina amani, hii hali inanitesa sana. Kila mara ananitokea ndotoni na kunieleza mambo yanayofanana.”
MAMBO GANI?
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake aliyoiacha haina mafanikio. Sasa nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia. Analalamika kwa nini filamu hazitolewi, ni jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo wangu,” alisema Seth.
Seth Bosco.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.
AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza ni kwamba, kila anaponitokea, lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa kasi na kutoka jasho jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”
MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema lazima tufanye maombi kuondoa hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha uso wa wasiwasi.