Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa zamani wa
Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili
asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ngapi wameongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la
Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo
huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata
mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo
wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.