Pages

June 08, 2014

Papa awapokea Peres na Abbas

 Mahmoud Abbas, Papa na Shimon Peres Vatikani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.
"Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema
Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:

"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.
Na kwa upande wake Bwana Abbas aliombea amani katika mkutano huo," alisema Peres.

Naye kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliomba kwenye hafula hiyo.

"Ee Bwana, tuletee amani ya kudumu na ya haki katika taifa letu na eneo letu, kwa ujumla, ili watu wetu na watu wote wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima ifurahie matunda ya amani, utangamano na kuishi kwa pamoja kwa upendo.
Baada ya sherehe hiyo, iliyoshirikisha maombi ya Kikristo, Kiyahudi na Kiislamu, waliokuwepo walisalimiana kwa mikono na kupanda Mzaituni katika Medani ya Vatican kama ishara ya amani.
Papa ametangaza hadharani kuwa hataki kuingilia moja kwa moja mashauriano ya amani ya Mashariki ya kati, yaliyoporomoka Aprili lakini akasema kuwa anatarajia kwamba mkutano katika Vatican utapunguza uahasama kati ya pande hizo mbili kinzani za Mashariki ya Kati