Pages

March 03, 2014

ABIRIA AJICHINJA NDANI YA BASI

AMA kweli duniani kuna mambo kwani dereva na abiria wa basi la Manchester ambalo namba yake haikujulikana mara moja, lililokua likitoka Lindi kwenda jijini Dar es Salaam walijikuta wakiangua vilio baada ya kumuona mwenzao akijichinja hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo.
Ujumbe kabla ya kifo: Kijana aliyejichinja ndani ya basi akiandika ujumbe kabla ya kukata roho.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri, Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo lilipofika katika hoteli moja ya Nangulukulu kwa ajili ya kupatia chakula.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa  mara walipofika katika hoteli hiyo, kila mmoja alitawanyika kwa lengo la kujipatia chakula na baadhi yao walienda maliwatoni akiwemo marehemu huyo.
Msaada:...Kijana huyo akitolewa kwenye basi baada ya kujichinja kwa sime.
Walisema kwamba  marehemu huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, wakati wa kushuka hakuonekana na kisu aina ya sime lakini baadaye abiria wachache waliotangulia kwenye gari, walimshuhudia akiwa ameshika sime hiyo mkono pasipokujua aliipata wapi.
“Hata sisi tulishangaa kumuona akiwa karibu  na usukani wa dereva huku akizamisha sime tumboni kisha kuichomoa  na kujichinja shingoni  hadi pale alipokuwa akivuta koromeo na kuning’inia.
Damu kila mahali: ...Akiingizwa katika gari lingine huku damu zikiwa zimetapakaa.
“Tulichanaganyikiwa kwani ni kitu ambacho hatukukitarajia na wala hatujawahi kushuhudia tukio kama hilo la mtu kujichinja hadharani, tulibakia kutokwa machozi huku akina mama wakipiga yowe, hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea kumuokoa kwani kila mmoja alimuogopa.
“Tulishindwa kupanda basi hilo kwani ni tukio la ajabu pia ndani kwa mbele kulikuwa kumetapakaa damu, ghafla alidondoka chini ndani ya gari, aliomba kalamu na karatasi ili kuandika ujumbe.
Silaha: Polisi akiwa na sime aliyotumia kujichinja kijana huyo.
“Dereva alichukua kalamu na kipande cha karatasi na kumpa, alianza kuandika  huku damu ikimbubujika tumboni na shingoni, hatukujua alichokiandika, aliishiwa nguvu taratibu akadondoka.
“Abiria walimsogelea na kumuinua na walimueleza kuwa atubu kwa Mungu kosa alilolifanya kabla hajafa, alipiga magoti na kuomba,  ghafla alidondoka tena.
Imani: Kijana akisali kabla ya kukata roho.
“Kaka yake ambaye alikuwa akisafiri naye kuelekea Dar es Salaam alichanganyikiwa kwani hakutegemea kuwa mdogo wake angejiua, kwani alisema hana historia ya kuugua ugonjwa wa akili. Polisi walipigiwa simu na walifika kumchukua lakini baada ya muda mfupi akawa amefariki dunia.
“Sisi abiria wengine tuliendelea na safari kuelekea Dar es Salaam  ambapo marehemu na kaka yake walibakia huko  mkoani Lindi.
Kifo:...Kijana huyo baada ya kukata roho.
“Mara tulipofika Dar es Salaam dereva alitusihi tukae kimya kwa dakika moja na kuomba kutokana na tukio lililotupata, tulifanya hivyo baadaye kila mmoja alitawanyika na kuelekea kwake,” kilisema chanzo kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alipoulizwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea.
“Ni kweli tukio hilo lilitokea lakini kwa sasa sina data kwani nipo njiani nikitokea Nairobi, Kenya kikazi kuelekea Lindi, mara nitakapofika huko ofisini ndipo nitapata tukio zima lilivyokuwa,” alisema Kamanda Mzinga.

FREEMASON WATUA KANISA LA GWAJIMA

WATU wanaodaiwa kuwa ni wa imani ya Freemason wametua ndani ya ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Baadhi ya vitu vilivyokutwa kanisani kwa Gwajima.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Freemason hao wawili waliingia kwenye ibada hiyo iliyofanyika Februari 23, mwaka huu ndani ya kanisa hilo lenye makao makuu yake katika Viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe jijini Dar wakiwa na mfuko wa rambo wenye vitu mbalimbali vikiwa na alama zao.
GWAJIMA MADHABAHUNI
Habari zilidai kwamba wakati neno likiendelea kunenwa na Mchungaji Gwajima, watu hao walifunua mfuko huo ambapo baadhi ya waumini waliokuwa karibu yao walihoji kulikoni kuwa kwenye ibada na vitu vyenye viashiria ya Freemason.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
“Wengine tulishangaa sana kwani baadhi ya vitu vilionekana kuwa na thamani kubwa, tukadhani labda wameleta zawadi kwa mtumishi wa Mungu (Gwajima),” kilisema chanzo hicho ambacho kinaabudu katika kanisa hilo.
MFUKO WANASWA NA WALINZI
Mtiririko wa tukio hilo unazidi kuwekwa wazi kwamba, haraka sana walinzi wa kanisa hilo walifika eneo lenye mfuko huo na kuunasa huku watu walioingia nao wakipotea au kujichanganya miongoni mwa waumini wengine.
WASIWASI WATANDA
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya waumini wa kanisa hilo walipozungumza na Uwazi baada ya ibada kumalizika walisema wanaamini watu hao walifika kanisani hapo kwa nia mbili, kujisalimisha au kuzijaribu nguvu za Gwajima ambaye ni maarufu kwa kuibua misukule.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiongoza ibada.
MFUKO WENYE VITU
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa, ndani ya mfuko wa watu hao kulikutwa saa ya rangi ya fedha, pete ya dhahabu, cheni 2 za fedha, bangili, fulana nyeupe na shati jeusi, vyote vikiwa na picha zenye alama mbalimbali za Freemason kama mafuvu, nyoka na bikari.
“Lakini mimi naamini wale watu nia yao hasa ilikuwa kumjaribu mtumishi wa Mungu ambaye ni kinara wa kuwarudisha watu waliokufa katika mazingira ya mazingara (misukule),” kilisema chanzo kimoja na kujitambulisha kwa jina moja la Isaya.
IMANI KWA GWAJIMA YAKAZIWA
“Mimi ninavyomjua Gwajima sidhani kama wangefanikiwa, ni vigumu sana. Kuna majambazi waliwahi kujaribu kumuua lakini waliambulia patupu, wakapigwa na upepo wa kisurisuri, sembuse Freemason? Ninachokijua mimi watamjaribu lakini hawataweza,” kilisema chanzo kingine.
UWAZI MZIGONI, WALINZI WAWA MBOGO
Wakati sakata hilo likiendelea, mmoja wa waandishi wa Uwazi alipata taarifa ambapo aliwahi tukio hilo na kujaribu kupiga picha lakini mlinzi mmoja (jina tunalo) alimkataza licha ya kufanya jitihada kubwa.
Mlinzi huyo alimnyang’anya kamera mwandishi wetu na kuishikilia kwa muda huku akitishia kufuta picha zote hata kama hazikuwa za tukio hilo.
GWAJIMA KIMYA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo nzima, Uwazi lilitumia siku tano kumsaka Mchungaji Gwajima ili kupata mtazamo wake juu ya tukio hilo ambalo huenda ni la kwanza kwenye kanisa hilo la kiroho jijini Dar es Salaam lakini bila mafanikio kutokana na kukwamishwa na wasaidizi wake.
Awali, ilikuwa Februari 25, mwaka huu ambapo hakupatikana kanisani kwake na hata kwa njia ya simu.
Baada ya kumkosa mtumishi huyo kwa kutopokea simu, Uwazi lilimtumia ujumbe wa simu (SMS) na kumuuliza kuhusu tukio hilo na ikiwezekana kukutana ambapo alijibu kwamba alikuwa kwenye kikao cha viongozi wa Kikristo, Kurasini jijini Dar, hivyo asingeweza kuonana na wanahabari.
Ijumaa ya Februari 28, mwaka huu, waandishi wa gazeti hili walitumia saa tano kumsubiri Gwajima kanisani kwake bila mafanikio.
MSIKILIZE MSEMAJI WAKE
Baadaye msemaji wa kanisa hilo, Mchungaji Yeconia Bihagaze alipoulizwa juu ya sakata hilo aliliambia gazeti hili kuwa, matukio kama hayo hutokea mara kwa mara licha ya kuchukua muda mrefu ikilinganishwa na hili la juzikati.
“Mambo ya Freemason kujisalimisha hapa mbona ni ya muda sana! Mimi naona kama yamepitwa na wakati, tukio hilo unalolisema mimi sijalisikia. Kanisa letu ni kubwa, mambo mengine ni madogomadogo hivyo siyo lazima yafike kwenye uongozi wa juu.
“Kwa nini msiandike misukule tunaowafufua hapa kila siku? Kwa nini msichukue matukio makubwa kwenye mtandao wa kanisa letu? Ninyi wanahabari wakati mwingine huwa mnatuvunjia heshima ndiyo maana huwa tunaamua kuwapotezea,” alisema Mchungaji Bihagaze. 

WEMA AMHARIBIA PASTOR MYAMBA

STAA wa filamu mwenye jina kubwa nchini, Wema Sepetu hivi karibuni alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.
Wema Sepetu.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo aliliambia gazeti hili kuwa, Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa haukuwa wa kweli.
Alisema kutokana na kutofika kwa staa huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi wageni wengine, wakiwemo waandishi wa habari.
Emanuel Myamba 'Pastor Muyamba'.
Mmoja wa watu wa karibu na Wema aliliambia gazeti hili kuwa muigizaji huyo hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi karibuni, kwani mara zote amekuwa akiwaeleza kila linapotokea jambo zito kama hilo.
Mtu huyo alisema katika ratiba ya siku hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja la starehe na halikuwa limebadilika.
juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo alichosema kimemsikitisha kwani walitoa mwaliko kwake kutokana na heshima aliyonayo.
“Nimemshangaa sana, lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu anajitambua na ni professional,” aliema Myamba.

BILIONEA ANASWA KWA UNGA DAR

BILIONEA maarufu jijini Dar es Salaam, Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) ambaye alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na Kikosi Maalum cha Polisi Tanzania kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya ‘unga’, amenaswa.
Bilionea Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’(44) aliyenaswa na polisi.
Vyanzo vililiambia gazeti hili kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Februari 23, mwaka huu, saa sita mchana akijianda kwenda nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mara baada ya Shkuba kukamatwa alisafirishwa usiku huohuo kwenda mkoani Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huu aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kusini.
Madawa ya kulevya.
Shkuba ambaye ni mkazi wa Mikocheni, Dar ni mfanyabiashara mwenye maduka ya kubadili fedha (bureau de change) jijini, ana makampuni ya ulinzi na nyumba Mikocheni pia anamiliki magari ya kifahari likiwemo aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150.
Vyanzo hivyo vilisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa na kikosi kazi tangu Januari 12, 2012 na inadaiwa kwamba alikimbilia nje ya nchi na kurudi kwa siri na ndipo jeshi hilo liliamua kumuwekea mtego.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa, tangu vita ya kuididimiza biashara ya unga ianze nchini, hakuna bilionea aliyewahi kukamatwa zaidi ya mtuhumiwa huyo.
Gari aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi ya milioni 150 ambalo ni mojawapo ya magari ya kifahari anayomiliki Shkuba.
Vyanzo vingine vya habari toka ndani ya jeshi hilo vinadai kwamba, Shkuba aliwahi kukamatwa mwaka 2006 kwa kuhusishwa na biashara hiyo haramu na kuwekewa ulinzi wa kifungo cha nje.
Habari zinadai kuwa, Januari 12, 2012, kikosi kazi cha kupambana na biashara hiyo kilipata taarifa ya kuwepo kwa madawa hayo aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Kikosi hicho kiliweka mtego maeneo ya Machinga Two mkoani humo na kufanikiwa kukamata unga huo uliokuwa umefichwa katika hoteli moja.
Binti wa Liyumba, Maureen Liyumba, siku alipokamatwa pamoja na wenzake wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 mkoani Lindi yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Watu wanne walikamatwa sanjari nao, akiwemo binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, Maureen Liyumba ambaye yuko mahabusu mpaka sasa na ameungana na Shkuba.
Vyanzo hivyo vilidai kwamba watu hao walikuwa wakiwasiliana na Shkuba ambaye watuhumiwa walimtaja na ndipo polisi walipoanza kumfuatilia.
Madawa ya kulevya aliyokamatwa nayo binti wa Liyumba na wenzake.
Siku moja nusura polisi wamkamate ambapo alikimbia na kulitelekeza gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T921 BPY ambalo bado linashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Lindi.
Inadaiwa kwamba polisi walipokwenda nyumbani kwake jijini Dar walimkosa na kila walipopiga simu zake zilikuwa hazipatikani hewani lakini baada ya kumkamata walimpeleka Lindi kwa helikopta.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi na Uwazi kuhusu madai hayo alithibitisha kukamatwa kwa Shkuba na kwamba tayari ameunganishwa na wenzake mkoani Lindi na wanaendelea kuwasaka mabilionea wengine ndani na nje ya nje ya nchi.

Maureen Liyumba pamoja na watuhumiwa wenzake.
“Ni kweli tulikuwa tukimsaka kwa muda mrefu Bwana Shkuba na tulijipanga vizuri sisi kikosi kazi hali iliyotufanya tumnase.
“Hii vita ya biashara haramu kwa sasa si kwa Tanzania tu bali ni vita ya dunia nzima, nawaomba wananchi wazidi kutupa ushirikiano na tutayafanyia kazi kwa siri maelezo yao,” alisema Kamanda Nzowa.

PICHA: HII NDIO BENDI INAYOTIKISA DUNIANI, HAPA BAIKOKO NI CHA MTOTO!





Hii ni Aibu hawa wanafanya matukio machafu kama haya ili mradi tuu kuvunja rekodi ya dunia Dunia hii inaenda wapi jamanii daah
Dunia inaongozwa na matukio machafu sana kwa sasa matukio haya mengi yanafanyika ili kupata pesa wengine wanadiliki hata kufanya mambo ya aibu katika jamii ilimradi wapate pesa ya kujikimu kimaisha












AIBU: PICHA ZA HEMED NA NAJMA DATAN WAKINYONYANA MATE HADHARANI ZAVUJA NA KUSAMBAA KWA KASI MITANDAONI!


Waigizaji wa filamu nchini ambao pia ni wanamuziki wa Bongofleva Hemedy Suleiman na Najma Datan wamezua maswali kwa watu wanaofuatilia habari za mastaa wa Tanzania baada ya picha zao wakiwa kimahaba zaidi kuanza kusambaa.

 Katika picha hizo zinazoonekana hapo juu  na chini wawili hao wanabusiana kimahaba kama wapenzi walioshibana. Haijajulikana kama picha hizo ni za video mpya ya muziki, filamu au ni wapenzi kweli.

Hata hivyo tayari inajulikana kuwa Hemedy kwasasa anatoka na Zuhura Gora ambaye ni model na muigizaji pia, huku Najma akiwa ameshawahi kuwa katika penzi na Mr.Blue, Najma pia hivi karibuni alijitosa Rasmi kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood na filamu ya Fan's Death akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Rammy Galis. 

USAGAJI WAMTESA JACKILIN WOLPER



Msanii Jacqueline Wolper, amesema anaumizwa sana na tetesi zinazozagaa kama moto wa kifuu kitaani kuwa anajihusisha na vitendo vya usagaji.

Akizungumza nasi  kuhusiana na skendo hiyo, mwanadada huyo alisema, akiwa kama mwanamke anayejitambua na kumtukuza vyema Mungu wake jambo hilo limekuwa likimuumiza.
 
“Roho inaniuma sana kuhusiana na hizo taarifa sijui niongee nini ili jamii inielewe kile nitachokizungumza, ni ngumu sana kufanya hicho kitu ambacho najua hakimpendezi Mungu kivyovyote vile,” alisema Wolper.

FACEBOOK, INSTAGRAM NA WHATSAPP KUSITISHA KUTOA HUDUMA NCHINI UGANDA BAADA YA RAIS WA NCHI HIYO YOWERI MUSEVENI KUPANGA SHERIA YA KUZUIA USHOGA


Ikiwi ni siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kusaini muswaada wa sheria ya kupinga ushoga nchini humo, kampuni ya Facebook imetangaza uwezekano wa kusitisha huduma zake nchini Uganda kama njia ya kupinga uamuzi huo ambao wamedai kuwa unakiuka haki za baadhi ya watu.
 
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inasema kuwa, Facebook ilianzishwa kusupport haki za binadamu kwa kuwapa nafasi watu wote ya kujielezea kwa uhuru, hivyo wanasikitishwa kujua kwamba Uganda kama nchi imesaini muswaada wa sheria ya kupinga ushoga.
 
Taarifa hiyo inaendelea kusema Facebook kwa sasa inatazama upya juu ya kujihusisha kwake kutoa huduma nchini Uganda, na kuongeza kuwa kusitisha kutoa huduma zake za Facebook, Instagram na Whatsapp nchini humo kwa muda watakaoona unafaa, ni moja ya hatua wanayofikiria kuchukua kama njia ya kuonesha kutoridhishwa kwao na uamuzi huo.
Isome taarifa hiyo:

STATEMENT FROM FACEBOOK ON ANTI-HOMOS6XU8LITY LAW
 
When we launched Facebook, we thought it as a platform to advance people’s rights and liberties of self expression in all form. We were equally shocked to learn that Uganda as a country had gone ahead to sign the Anti Homos9xu9lity bill into a law.

Facebook is currently reviewing its engagement to Uganda, as we seek to come up with a voice to express our dissatisfaction. And of course, suspending our operations in Uganda is one of the options we are considering. In the event that we suspend operations in Uganda, our platforms of Instagram, Facebook and Whatsapp will be off for a time we shall deem necessary.

We strongly condemn the act of the Ugandan Government to overstep the rights of a minority. All humans are created equal and deserve a right to freedom and happiness.
Signed
Sheryl Kara Sandberg
Chief Operations Officer (COO) At Facebook
 
Mmoja wa wamiliki wenza wa Facebook, Chris Hughes ni shoga na aliolewa na June 30, 2012 na mwanaume mwenzake, Sean Eldridge.
 ******
(Kwa  hisani ya  Bongo5

MAN CITY YATWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE


LONDON, England
KOCHA Manuel Pellegrini amefanikiwa kutwaa taji la kwanza akiwa bosi wa Manchester City baada ya jana kuifunga Sunderland katika fainali ya Kombe la Capital kwa mabao 3-1kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.
Kocha huyo raia wa Chile ambaye yupo katika adhabu ya kukosa mechi tatu za Ulaya baada ya kufungiwa na Shirisho la Soka la Ulaya (Uefa) kutokana na kumtolea lugha kali mwamuzi, Jonas Eriksson, alikuwa na furaha jana kutokana na ushindi huo.
Licha ya Sunderland kuanza kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 10 kupitia kwa Fabio Borini, ilijikuta ikizidiwa nguvu na kupata kipigo hicho kipindi cha pili.
Yaya Touré ndiye aliyefunga bao kali kwa shuti katika dakika ya 55, wapinzani wao hao walijikuta wakipagawa na kufungwa la pili dakika moja baadaye na Samir Nasri.

AL AHLY WASUSA VYAKULA, NI BAADA YA KIPIGO

Mohammed Mdose na Said Ally
KIPIGO cha bao 1-0 walichokipata Al Ahly dhidi ya Yanga, kimeonyesha kuwachanganya vilivyo Waarabu hao, kwani baada ya mchezo walionekana kutupatupa ovyo vyakula walivyokuwa navyo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Waarabu hao walikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, juzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa bao safi lililofungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Championi lilifanikiwa kupenya kwenye chumba walichokuwemo Al Ahly na kushuhudia matunda aina ya apple, ndizi na juisi vikiwa vimezagaa chini katika chumba hicho huku wachezaji hao wakiwa hawana muda navyo, kwani wengi wao walionekana kujadili kipigo hicho.
Championi lilijaribu kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kujua kwa kina chanzo cha mkasa huo, lakini walionekana kuwa na hasira na kugoma kuzungumza chochote.
Hali ilikuwa tofauti katika chumba cha timu ya Yanga ambamo wachezaji wake walikuwa wenye furaha muda wote huku wakipongezana.
Yanga na Al Ahly zinatarajiwa kurudiana mwishoni mwa wiki hii jijini Cairo.

March 02, 2014

“Mimi ni dalali wa madini”….Fid Q

Kati ya mamia ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu Tanzania, ni mwanamuziki mmoja pekee aliyehudhuria katika Tamasha la Sauti za Busara 2014, lililotajwa na Kituo cha Utangazaji cha CNN kuwa ni tamasha lenye nguvu barani Afrika.
Huyu siyo mwingine bali ni Fareed Kubanda (Fid Q), aliyekuwapo mjini Zanzibar kwa siku mbili kushuhudia tamasha hilo lililokuwa la siku nne, lililofanyika katika wiki ya pili ya Februari mwaka huu, Viwanja vya Ngome Kongwe visiwani humo.
Ikumbukwe kuwa Fid Q alianza shughuli za muziki miaka ya 1990. Alitoa wimbo wake wa kwanza mwaka 2000 ulioitwa; Huyu na Yule, alioimba na Mr Paul. Wimbo huu ulirekodiwa na Prodyuza maarufu nchini,  Master Jay katika Studio za MJ Records na kumpa heshima kubwa msanii huyo.
Starehe ilifanya mahojiano na  Fid Q ambaye pamoja na mambo mengine aliweka wazi sababu za yeye kuwapo katika tamasha hilo, kilichomvutia huku akiweka wazi kuhusu biashara ya madini aliyodaiwa kuanza kuifanya mwishoni mwa mwaka jana.
Swali: Nini kimekuvutia ukaamua kuhudhuria katika tamasha hili?
Fid Q: Mimi ni mtu ninayependa kujifunza zaidi, nimeona hili ni tamasha kubwa na zuri kwangu kujifunza. Kubwa zaidi ni kutaka kujua wenzetu wanafanyaje muziki. Huwezi kukaa tu na kwenda kupiga muziki staili moja kila siku; ili ujue, ni vyema ukajifunza kutoka kwa watu unaowaamini.
Swali: Kupitia wanamuziki wa muziki wa asili kutoka mataifa mbalimbali katika Sauti za Busara, unadhani unaweza kupata uzoefu wa kutosha?
Fid Q: Wasanii wote wa mataifa mbalimbali waliofanikiwa hasa Nigeria, wamekuwa wakichukua vionjo kutoka katika muziki wa asili, kisha wakileta katika muziki wa kizazi kipya, inapatikana ladha ya kipekee, ndiyo maana leo unawaona kina P Square wanatamba, walianza kujifunza na kutumia vionjo kutoka katika muziki wa asili.
Swali: Unadhani nini kinachowafanya wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutohudhuria tamasha hili?
Fid Q: Hawapo tayari kujifunza. Mimi nimewahi kutumbuiza katika tamasha hili, ninajua. Huku hakuna ubabaishaji, msanii unatakiwa uimbe kwa sauti yako jukwaani, walio wengi hili hawaliwezi. Idadi kubwa ya wasanii wamezoea kuimba kwa ‘playback’, (kuweka cd ya ala), ndiyo maana hata waandaaji wanashindwa kuwaalika, muziki tunaofanya sisi ni ule wa wenzetu, lakini tunashindwa kuuwakilisha ipasavyo, tumezoea kuimba kwa ‘playback’.
Swali: Unadhani kuna umuhimu gani kwa wasanii kuimba ‘live’ (kwa sauti zao wenyewe pasipo kutegemea CD)?
Fid Q: Ina faida zake. Kwanza inakutangaza na pia unaonekana wewe ni msanii halisi. Haya ndiyo wanayohitaji kuyaona watu wanaoujua muziki, watu wanaohudhuria matamasha ya kimataifa ni wengi, hawawezi kusikiliza kitu walichokisikia kwao, wanapenda kusikia kitu kipya kitakachowateka.

Kutana na Hafidh Masokola, Kijana wa Kitanzania Aliyegeuka kuwa Albino Ikiwa ni Athari ya Matumizi ya dawa Aina ya METAKELFIN.

Hafidh Masokola Damson ambaye kwa sasa anaishi Tabora mjini eneo la NationalHousing amebadilika maeneo yote ya viungo vya mwili wake isipokuwa meno pekee na kuwa albino hata kufikia hatua ya kujiunga na chama cha Maalbino Tanzaniatawi la Tabora.
Bw.Hafidh Masokola Damson ambaye alibadilika na kuwa Albino kutokana na matumizi ya dawa za Malaria baada ya kuzitumia mnamo mwaka 2010,Kwa maelezo yake mara baada ya kunywa dawa aina ya Metakelfin alianza kubabuka ngozi ya mwili wake huku magamba yakitoka mithiri ya nyoka katika mwili wake.
Hafidh Masokola kabla ya kubadilika kuwa mlemavu wa ngozi Albino.
Kwa uthibitisho wa habari hii waweza kumpigia kwa simu ya kiganjani 0767 298 348 au 0658 298 348.

TASWIRA ZA SALUM MKAMBALA AKIWA HOSPITALI YA TUMBI BAADA YA AJALI

Mtangazaji wa Channel 10, Salum Mkambala, akipelekwa Theatre katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Msanii wa kundi la Mizengwe, Hemed Maliyaga (wa kwanza kulia) akisaidiana na ndugu pamoja na mke wa Mkambala (wa tatu kushoto) kumpeleka mgonjwa Theatre.
...Mkambala akiingizwa Theatre.
HALI ya Mtangazaji wa Channel 10, Salumu Mkambala aliyepata ajali alfajiri ya leo kwa kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro inaendelea vizuri katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na mwandishi wetu hospitalini hapo, mdogo wa mtangazaji huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea Morogoro na alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri saa 10. 30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni kutokana na barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali iliyosababisha gari la kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.

BONANZA LA MICHEZO DAR LIVE HAKUNAGA

Mhe. Angela Kizigha na Mhe. Faustine Ndugulile wakifanya mazoezi na klabu mwenyeji wa bonanza hilo, Magenge 20.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Mh Angella Kizigha akiongea na wanajogging wa bonanza hilo.
Mhe. Angela Kizigha akipokea zawadi kutoka kwa klabu mwenyeji ya Magenge 20.
Mhe. Faustine Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni akipozi na Mgeni Rasmi, Angela Kizigha baada ya kupewa zawadi ya kikoi.
Timu ya Magenge 20 na Classic kabla ya mtanange kuanza.
Baadhi ya washiriki wa bonanza hilo wakiwa ndani ya Dar Live.
Wanabonanza wakiwa stejini ndani ya Dar Live.
BONANZA la michezo la kila mwezi linalofanyika katika Uwanja vya Burudani wa Dar Live Mbagala Zakhem limefanyika leo ambapo maelfu ya wanamichezo wamejitokeza kushiriki bonanza hilo la aina yake.
Wenyeji wa bonanza hilo walikuwa ni klabu ya Magenge 20 ya Mbagala Kiburugwa jijini Dar, ndiyo walikuwa wakizikaribisha timu zote zilizokuwa zimepewa mwaliko wa kushiriki bonanza hilo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa ni Mheshimiwa Angela Kizigha, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki aliyekuwa ameambatana na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na wanamichezo mbalimbali.
Licha mvua kubwa kunyesha lakini haikuweza kukata kiu ya wanamichezo waliokuwa wamejitokea kwani waliendelea kuserebuka ndani ya mvua bila kujali.
Hata hivyo burudani ya kufa mtu inatarajiwa kuangushwa jioni hii na bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Farasi’ chini ya Ally Choky ‘Mzee wa Ambulance’.
Vilabu  zaidi ya 180 vya mbio za pole ‘Jogging’ vimeshiriki ambapo michezo mbalimbali bado inaendelea kufanyika.
Washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali za michezo katika bonanza hilo la kufuru, aidha Tamasha hilo limedhaminiwa na PSPF, Mpango wa Damu Salama, Global TV Online, Kampuni ya A-One watengenezaji wa maji ya Maisha, Global Publishers Ltd, Dar Live pamoja na Benki ya Akiba Commercial (ACB).

WATU 28 WAUAWA CHINA

Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakiwa hospitali.
Miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo.
Baadhi ya mizigo iliyoachwa eneo la tukio.
Ulinzi ukiimarishwa eneo la tukio.
KUNDI la watu waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni mjini Kunming, China!
Mashahidi wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao waliovalia nguo nyeusi, waliwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Polisi walifanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya shambulio hilo.
Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo.