Pages

March 06, 2014

WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA BAADA YA HOSPITALI KUKUMBWA NA MAFURIKO

 Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita katikati ya Hospitali ya Palestina ambapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya hospitali hiyo.
 Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kuisha.
 Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali.
 Kushoto ni mgonjwa akiwa amelala juu ya benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
 Hii ndio hali halisi ya chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya Sinza Palestina.
 Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya hospital hiyo.
 Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate kuhudumiwa.
 Moja ya chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa.
 Hapa hata hapapitiki.
 Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa usafi.
 Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
 Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa kunyesha.
 Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa.
 Huu ndio mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya mtaro huo kuziba.
Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara, nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014  zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya meza na viti wakikwepa maji hayo wakati wengine wakikimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tu lakini yalikuwa ni machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
Baada ya mvua hiyo kuisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.

Akiongea kwa simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.

Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.

March 05, 2014

Kardinali Pengo aweka wazi msimamo wa Kanisa

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwaonesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, nakala ya gazeti la Mwanachi lililoandika habari kuhusu msimamo wa Kanisa juu ya suala la serikali tatu.

Dar es Salaam/Iringa.
Siku mbili baada ya Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoa waraka wa kulitaka Bunge Maalumu la Katiba kutopuuza mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, Askofu Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameibuka na kusema msimamo huo siyo wa Kanisa Katoliki nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kardinali Pengo pamoja na kukiri kuwa tume ilitoa maoni hayo, alikanusha kuwa taarifa zilizotolewa na moja ya magazeti kuwa msimamo wa Kanisa Katoliki ni serikali tatu.
“Maoni ya Tume hayawezi kuwa ni msimamo wa kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa misimamo yake na huwa inatolewa na Mwenyekiti wa TEC,” alisema.
Hata hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kutoka Jimbo la Iringa, alisema jana kuwa alikuwa na shughuli nyingi, hivyo asingeweza kuzungumzia suala hilo, labda wiki ijayo.
Akizungumza katika makazi yake mjini Iringa, Askofu Ngalalekumtwa alisema: “Mniache, nina shughuli nyingi…labda mnitafute wiki ijayo,” alisema.
Vilevile, Pengo ambaye alirejea msimamo wake binafsi wa kuunga mkono Muungano wa serikali mbili, alisema kwa namna Rasimu ya Katiba ilivyo, hakuna kigezo cha kulazimisha Kanisa Katoliki litoe msimamo.
Alisema Kanisa Katoliki lingeweza kutoa msimamo iwapo Rasimu ya Katiba ingekuwa na dosari zinazohusu imani au maadili.
“Kwa mfano, (Rasimu) ingekuwa inasema, hakuna Mungu lazima tungekuja juu kwa sababu inaingilia imani yetu,” alisema Kardinali Pengo na kufafanua:
“Vilevile tungeweza kusema inakwenda kinyume na maadili iwapo inaruhusu kuua wazee au inaunga mkono ndoa za jinsi moja.”
Tamko la Tume
Tamko la tume hiyo inayoongozwa na Askofu Mkuu wa Tabora, Paulo Ruzoka liliweka bayana kuwa muundo wa serikali mbili haukutatua matatizo ya msingi na badala yake ulilimbikiza kero zilizosababisha Zanzibar kujiundia katiba yake mwaka 2010 bila kushauriana na Tanzania Bara.
Tamko hilo la kurasa 15 lililosambazwa kwa baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Katiba, lilitolewa baada ya mkutano wa kitaifa wa Wajumbe wa Kamati za Majimbo za Haki na Amani za Kanisa hilo na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki Tanzania (CPT), uliofanyika jijini Dar es Salaam Februari 5 na 6 mwaka huu.

Msimamo binafsi
Kardinali Pengo alisema katika misimamo ya kisiasa ndani ya Kanisa Katoliki, waumini wanatofautiana bila kuzingatia ni kiongozi au muumini wa kawaida na hakuna sababu ya kulazimishwa kuwa na msimamo unaofanana.
Alisema yeye anaona serikali mbili zinaweza kusaidia zaidi katika usalama wa nchi na kujenga umoja hasa katika kuzuia watu wa nje wenye nia mbaya kupenya nchini ili kuanzisha chokochoko za uvunjifu wa amani.
Alisema ana wasiwasi mfumo wa Serikali tatu utatoa mwanya kwa maadui kupenya Zanzibar na hata kuingia Tanzania Bara.
Alitoa mfano wa nchi jirani ya Kenya, ambako matukio kadhaa makubwa ya kigaidi yametokea na kuonya kuwa kamwe asingependea kuona yanafanyika hapa nchini.
Kura ya siri
Akizungumzia mvutano wa mfumo wa upigani kura kwenye Bunge la Katiba, Pengo alisema: “Kura ya siri ndiyo njia pekee ya kutenda haki katika kupitisha vifungu kwenye Bunge linaloendelea mjini Dodoma.”

Lissu amkubali Sitta


 “Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake.” Tundu Lissu  

Dodoma.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya chama au ya kundi la watu wachache.
Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu ya  watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu  wakiingia katika uchaguzi, wataangushwa na Sitta.
“Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake,” alisema Lissu.Alisema katika kipindi ambacho aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.
Akizungumzia tetesi kuwa Mwanasheria Mkuu wa zamani,  Andrew Chenge ameonyesha nia  ya kugombea nafasi hiyo, alisema hayuko tayari kumuunga mkono.
Lissu alisema Chenge hataweza  kuliongoza Bunge hilo na kwamba kama atachaguliwa,  litavunjika likiwa mikononi mwake.
Kuhusu Samia Suluhu Hassan anayetajwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti , alisema hana shaka pia ingawa hajaonyesha makeke yake mbele ya vikao muhimu kama vya Bunge, lakini ni mzoefu wa muda mrefu serikalini na katika nafasi mbalimbali.

BUNGE LA KATIBA NGOMA INOGILE!

WAKATI msuguano  wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ukiendelea mjini Dodoma na kuzua majadiliano makali juu ya upigaji kura ya wazi au ya siri, ngoma inogile kwani inatabiriwa kuwa huenda bunge hilo lisifikishe  siku 90 za uhai wake na kuishia siku 70, baadhi wa wajumbe wameliambia Risasi Mchanganyiko.

Wakizungumza bila ya kutaka kutajwa majina yao, baadhi ya wajumbe wa bunge hilo wamesema kuwa hali siyo shwari kutokana na baadhi ya wanasiasa kutetea misimamo yao ili ishinde.
“Tunaonekana si wamoja ndani ya bunge hili na kila upande umekuja na dhamira yake ya kutafuta ushindi, hali hii inaweza kulifanya bunge kushindwa kumaliza siku 90 zilizopangwa kutafuta Katiba Mpya ya Tanzania,” alisema mjumbe mmoja kutoka Zanzibar kwa niaba ya wenzake.
Pia wanasiasa wanaotoka katika vyama vya upinzani wamekuwa wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutaka kuuteka mkutano huo.
“Asilimia kubwa ya wapinzani wanataka kura za  siri lakini CCM wanataka wajumbe wapige kura za wazi kwa maslahi yao ili kuweza kuwaadhibu wanachama wao wasiokubaliana na hoja za upande wao, kwa mtazamo huu hatutafika siku 90,” aliongeza mjumbe mwingine wa upinzani.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe  wa CCM wamewashutumu wenzao wa upinzani  kwa kuwaambia kuwa wana malengo  ya  kuvunja muungano wa Tanzania kwa ajili ya uroho wa madaraka.
“Haiwezekani tuje Dodoma kama Watanzania na tutoke  tukiwa si Watanzania, lengo letu ni kudumisha umoja na kuendeleza mazuri ya viongozi wetu waliotangulia,” alisema mbunge wa CCM anayetokea Mwanza.
Naye mwenyekiti wa  muda wa bunge hilo, Pandu Amir Kificho amekuwa katika wakati mgumu kwa kuwataka wajumbe kuacha  kuchangia rasimu ya katiba kabla ya muda wake.
“Naomba nieleweke, bado hatujaingia kuichambua rasimu ya katiba, hebu tujadili kanuni za kutuongoza kwanza,” alikaririwa mwenyekiti huyo akimwambia Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF) na kuwafanya wajumbe wengine kumshangilia.
Baadhi ya wadau wanaofuatilia bunge hilo wamesema hawatashangaa kuona wajumbe wakiondoka Dodoma kabla ya kutimia kwa siku 90.
“Hilo liko wazi, fedha za walipa kodi zinaweza kuliwa bure na Watanzania wasipate kile wanachotarajia,” alisema Othman Zinga anayefuatilia mkutano huo.

LAANA YA KANGA MOJA YAINGIA MPAKA KWA WACHEZA SHOW ZA MAJUKWAANI

Toka umeingia huu mtindo wa lile kundi la khanga moko siku hizi kamezuka kamtindo ka wacheza show za jukwaani nao kuvaa khanga na kuonesha sehemu kubwa za maongo yao ikiwemo kufuli walizo vaaa...Hii ni laana ya khanga moko inazidi kutafuna tasnia ya sanaaaaa ....
Umati mkubwa uliofulika katika ukumbi kwenye show moja ya mziki wakishangazwa na Show ya mwanadada huyo hapo juuu baada ya show hiyo kila mtu alisikika akimponda huyo dada kwa kile alichofanya hapo jukwaani

AIBU: KIGOGO ANASWA AKIONGOZANA NA KAHABA ALIYEVALIA NUSU UCHI





Kama kweli uko sawa na una akili timamu huwezi ongozana na mtu amevaa namna hii, kwanza ni aibu kwako kwani inaonyesha na wewe pia umekubaliana na mavazi hayo ya ajabu.

LINAH: SIPENDI KUTUMIA KONDOMU SABABU ZINAPUNGUZA LADHA YA MAPENZI

Esterlina Sanga ‘Linah’.
MSANII wa kike anayetesa kwenye Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ ametoa mpya baada ya kuibuka na kueleza wazi kuwa, awapo faragha hapendi kutumia kinga.
 
Linah alisema hayo wakati akizungumza na mwakilishi wa kona hii jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita, ambapo alisisitiza kuwa anachukia sana mipira ya kike na kiume wakati wa tendo kwa vile zinamkata stimu.

“Sema naogopa ukimwi na magonjwa mengine ndiyo maana nalazimika kutumia kwa ajili ya afya yangu lakini kiukweli kabisa, sipendi kabisa kinga,” alisema Linah.
Hivi karibuni, gazeti hili liliripoti habari ya staa huyo wa muziki kudungwa mimba na mdosi kabla ya siku chache baadaye kugundulika kuwa, kiumbe chake kilichoropoka.

WASTARA: HUYU NDIYE MSANII WA BONGO FLEVA NILIYEZAA NAYE KABLA YA SAJUKI

http://3.bp.blogspot.com/-65tYqlfukbk/UnoaxrvK4pI/AAAAAAAAB5o/7ZBljXBmxGE/s1600/WASTARA.jpg

RAY C AMUOMBA MPENZI WAKE WA ZAMANI LORD EYEZ ABADILIKE

Aliyekuwa mpenzi wa rapper Lord Eyez, mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C amezungumzia kuhusu sakata la wizi linalomkabili rapper huyo ambaye ni member wa group la Nako 2 Nako Soldiers.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Ray C amefunguka kama ifuatavyo:

USALITI 100%..MKE WA MTU AINGIZA MWANAUME CHUMBANI KWA MUMEWE MCHANA!

HUU ni usaliti 100%! Mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Mwanahamisi au mama Daudi, mkazi wa Pugu-Kajiungeni, Dar, amejikuta akipata aibu ya karne baada ya kudaiwa kuingiza mwanaume mwingine chumbani kisha kufumaniwa na mumewe.
MSAMAHA: Mwanahamisi ambaye ni mke wa mtu akiomba samahani baada ya kunaswa.
Tukio hilo la kufedhehesha lilijiri hivi karibuni, mchana kweupe nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao, mume wa Mwanahamisi aitwaye Mashaka au baba Daudi ana rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Paulo ambaye alidai kusumbuliwa na shemeji yake (mama Daudi) kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kuwa mama Daudi alikuwa akimtumia Paulo ujumbe wa mapenzi kupitia simu hadi wakati mwingine kufikia hatua ya kumbana na kumkumbatia pale anapokutana naye njiani.
Ikaelezwa kwamba Paulo alimwambia baba Daudi kuwa alikuwa ameshamtumia zaidi ya SMS 240 za kimapenzi.
Baada ya kuona kero zimezidi huku rafiki yake akimlalamikia kutomuelewa mke wake aliyezaa naye mtoto mmoja ambaye bado hata hajaacha kunyonya, Paulo aliamua kuvunja ukimya na kumuonesha ujumbe anaotumiwa na shemeji yake huyo ili wamkomeshe.
AIBU YA USALITI: Mke wa mtu pamoja na njemba aliyokuwa nayo wakiwa na aibu baada ya kunaswa live chumbani.
Ilisemekana kwamba baada ya kufanya tathmini ya SMS hizo, baba Daudi na Paulo waliweka mtego huku wakimshirikisha mke wa Paulo ambaye aliwahi kugombana na mama Daudi kwa kitendo cha kumtambia ovyo.
Ilielezwa kuwa baada ya mpango kukamilika huku Paulo akimwambia shemeji yake kuwa amemkubalia, mama Daudi alimuaga mumewe kuwa baba yake ni mgonjwa huko Yombo-Buza, Dar hivyo anakwenda kumuona na siku hiyo atarudi saa 12:00 jioni akijua kuwa kwa mwanya huo ataweza kwenda gesti maeneo ya Ukonga-Mombasa, Dar na Paulo kama walivyokubaliana.
Ilisemekana kuwa baada ya Paulo kuona gesti patakuwa na shida ya kumshikisha adabu mama Daudi, alimshawishi wakutane chumbani kwa mumewe (baba Daudi) ili iwe rahisi kumfumania.
Ilifahamika kwamba ili kusaliti chumbani kwa mumewe, alimpigia simu baba Daudi kujua alipokwenda.
Kwa kuwa baba Daudi alijua mchezo, alimwambia mkewe kuwa amekwenda kufuatilia kitambulisho cha kazi kisha atakwenda Kigogo, Dar kwenye mishemishe nyingine.
Ilidaiwa kuwa majibu hayo yalimfurahisha mama Daudi ambaye alimwalika Paulo chumbani kwa mumewe bila kujua aliwekewa mtego.
KIPONDO: Mke wa mtu akipokea kichapo baada ya kubambwa.
SAA 7:OO MCHANA KWEUPE
Mishale ya saa 7:00 mchana, Paulo aliondoka nyumbani kwake na kuwaacha wafumaniaji wakiwa tayari, alipofika kwa mama Daudi naye akainua simu kumpigia baba Daudi kumhakikishia Mwanahamisi kuwa mume wake harudi muda huo, akamwambia kuwa amekwenda mbali wataonana saa 12:00 jioni.
Ilidaiwa kuwa ili wafaidi mambo vizuri, mama Daudi alimuondoa mtoto wake na mdogo wake kwa kuwapa fedha ya kwenda kulipia kuangalia ‘tiivii’ kibandani ili abanjuke na Paulo kwa raha zake.
Nusu saa kabla ya tendo, Mwanahamisi alikuwa ameshasaula nguo zote mwilini ndipo Paulo alipomtaarifu baba Daudi kuwa mchezo tayari anaweza kufumania.
OFM, BABA DAUDI
Baba Daudi, huku akiambatana na makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers alitimba chumbani kwake na kumbamba mkewe ‘live’ kitandani kwake, tayari kusaliti ndoa.
Huku OFM ikishuhudia, mama Daudi alishtuka na kukimbilia khanga kisha akaanza kutoa lawama kwa Paulo kwa kumtia mtegoni.
Katika utetezi wake, mama Daudi alilia kwa uchungu na kusema kuwa ni shetani na tamaa ya fedha ndiyo iliyomponza kwani alijua angelamba mshiko kutoka kwa Paulo.
“Yaani naumia sana kwa mume wangu kunifumania tena na rafiki yake, naomba msamaha, ni shetani tu alinipitia,” alisema mama Daudi huku akimpigia magoti baba Daudi.
Pamoja na utetezi wake, mama Daudi alikula kichapo cha nguvu kutoka kwa mke wa Paulo ambaye aliunganishwa kwenye mtego.
Baada ya mtiti wa nguvu, mama wa Mwanahamisi aliitwa ambapo alipofika na kujionea aibu ya mwanaye, presha ilimpanda, akashindwa kuongea.
Hata hivyo, fumanizi hilo liliisha baada ya mmoja wa majirani kusuluhisha ugomvi huku akiwaongoza ibada ya toba kisha akawaomba wasameheane.
Mwanahamisi akamuangukia mumewe na kumuomba msamaha, maisha yakaendelea.

MASKINI JACK HALI MBAYA, AKWAA GONJWA LA HATARI MAHABUSU NCHINI CHINA!



Jacqueline Patrick ‘Jack’.
MODO mwenye mvuto Bongo Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka, safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo.
KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.
“Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi yake,” kilisema chanzo hicho.
MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.
“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.
Jack Patrick akiwa amefunikwa uso baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni nchini China.
WAKILI WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga.
KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum.
WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’
Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.
Habari zinasema kuwa hakuna cheni yoyote kutoka kwa watu ambao wanatafsiriwa kuwa ni waliomtuma kwani wanaosumbuka ni watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu zake.
Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es Salaam.
“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.  
SABABU ZA MOYO KUSHINDWA KUSUKUMA DAMU
Juzi, gazeti hili lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ambapo alisema:
“Moyo kushindwa kusukuma damu kwa mwendo wa kawaida husababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa, mgonjwa kushindwa kudumisha udhibiti wa maji mwilini, chakula au dawa.
“Sababu nyingine ni upungufu wa damu na utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za koromeo ambazo zinaleta maumivu ya ziada kwenye misuli ya moyo, utumiaji mwingi wa vimiminika au ulaji wa chumvi uliopitiliza na utumiaji wa dawa ambazo husababisha uwekaji wa maji mwilini kama vile Hiazolidinedione.”
KUHUSU KUKOSA HAMU YA KULA
Kwa mujibu wa daktari huyo, tatizo hilo humkumba mtu anapokuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na jambo zito linalomkabili, ambalo halina mlango wa kutokea.
TUKUMBUKE
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300.
Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili.

NELLY KIM KUTUMIA MAUTUNDU YA KANUMBA

Stori: Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu za Kibongo, Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’ amesema anajivunia sana kufanya sinema nyingi na marehemu Steven Kanumba na kwamba amejipanga kufuata nyayo zake ili aweze kufanikiwa kwa kutumia kipaji chake.
Marehemu Kanumba.
Akizungumza na Stori Mix, Nelly Kim alisema: “Nafurahi kufanya kazi na marehemu Kanumba. Nimecheza naye zaidi ya sinema 20 pale kwa Mtitu Game.
Nimejifunza kujiongoza na kuamini katika mambo makubwa, ndiyo maana sasa hivi nasimama na kampuni yangu ya Kasinge Production ambayo inatayarisha na kusambaza filamu.
Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’.
“Nimesharekodi filamu ya kwanza inayoitwa The Word of God ambayo nimecheza na Kajala, Ben, Kambi na wengineo.
Unajua wasanii hatujitambui, tunakubali kunyonywa wakati tunaweza kujitutumua na kusimamia kazi zetu wenyewe. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Kanumba ambayo nataka kuitumia ili kufaidika kwenye sanaa.”

March 04, 2014

KAHABA ANASWA AKIJIUZA NDANI YA GESTI

Zuena akiwa na mteja wake chumbani mara baada ya kunaswa na polisi. KABANG! Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar kwa kushirikiana na Oparesheni    Fichua
Maovu (OFM) ya GPL wamemnasa mrembo Zuena Mohammed anayedaiwa kukodi chumba cha gesti na kuingiza wa- naume kwa zamu usiku kucha

Zuena Mohammed akivaa nguo zake baada ya kunaswa na mteja chumbani.  
Tukio hilo lilijiri chumba namba 14 ndani ya Gesti ya Mori Lodge iliyopo Sinza jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikuwa amekodi chumba hicho na kuwapanga wanaume kwa foleni kwa ajili ya kutoa huduma haramu ya ng0no.

AFM Watonywa.
Awali, ‘makachero’ wa OFM walitonywa kuwepo kwa ishu hiyo na chanzo chake kilichodai kuk- erwa na tabia ya mrembo huyo ambaye amekuwa akitishia afya za wanaume wakiwemo vigogo wa serikali ambao ilidaiwa kuwa ni sehemu ya wateja wake.
Chanzo: Jamani OFM mpo ka- zini?


…akijifunika uso kwa aibu.

OFM: Tumejaa tele leta maneno.
Chanzo: Mimi naitwa (anataja jina) lakini naomba msinitaje. Kuna mrembo mmoja amekodi chumba gesti…yaani anapanga wanaume foleni anagawa dozi ya penzi.
OFM: Hatuwezi kukutaja tuna- heshimu vyanzo vyetu vya habari. Una uhakika na taarifa zako?
Chanzo: Nina uhakika asili- mia zote. Ninyi nendeni pale Mori Lodge maeneo ya Sinza, fanyeni kazi yenu mtapata mkanda kamili.


 
…akiwa na polisi (kulia).

OFM kazini
Baada ya kupenyezewa ‘tipu’ hiyo, OFM iliingia kazini na ‘kuliteka’ eneo la tukio kwa uchunguzi na kubaini undani wa ufuska huo wa kutisha.
Kabla ya yote ‘memba’ wa OFM alijifanya mmoja wa wanaume waliokuwa wakihitaji huduma ya mrembo huyo hivyo kujipatia data nyingi kabla ya kubadilisha uamuzi baada ya kupata ishu kamili.





HUDDAH MONROE NDANI YA SKENDO NZITO YA KUFANYA MAPENZI HADHARANI


 Mwanadada mwenye vituko vyakutosha huddah Monroe maarufu kama lady boss hivi karibuni huenda akatupwa mahakamani baada ya kuvunja sheria na kuweka mamba ya ndani hadharani ambapo ametupia picha kwenye mtandao huku akionekana yupo na njema wanafunja amri ya sita bila hata presha wa wasi, hakiki mdada huyu huenda anamatatizo na sio bure tu :Pichazi wakifanya live zitakujia sio muda endelea kutembelea site hii

KAULI YA WAZIRI WA ELIMU YAWACHEFUA WALIMU


Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekerwa na kauli ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa , kuwa serikali inaendelea kujadiliana na taasisi za fedha juu ya namna ya kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya  walimu yanayofikia Sh. bilioni 61.

CWT  imesema kauli hiyo ya serikali ni kutafuta visingizio baada ya  kushindwa kutekeleza ahadi yake kuwa ifikapo Februari, mwaka huu deni la walimu litakuwa limelipwa.

Rais wa CWT, Gration Mkoba,  alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema majadiliano ya mishahara ya walimu yalitokana na mgomo wa  2012 baada ya kukaa kwenye meza ya majadiliano na serikali ilikubali kulipa deni na kuandaa utaratibu wa kupandisha walimu madaraja.

“Inasikitisha kuona majadiliano yanahusisha waandishi wa habari bila ya kujua kuwa kwa kauli yake waziri tayari  walimu wameingia kwenye mgogoro na serikali, lakini  nawasihi walimu wasubiri tamko rasmi la mgogoro,” alisema.

Mkoba alisema tangu serikali ilipoahidi kutekeleza madai yao, hakuna hata dai moja  lililotekelezwa  lakini imewashangaza kuona ikijinadi kuwa inaendelea na majadiliano ya kulipa deni hilo wakati majadiliano hayana tija kwa mwalimu.

Alisema Novemba, mwaka jana mkutano mkuu wa CWT ulitoa siku 60 kwa serikali kukamilisha taratibu zote la kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu nchini.

Pia Januari mwaka huu kwenye kikao cha Baraza  la Taifa la CWT kiliazimia kuwa ifikapo mwishoni mwa Februari, mwaka huu, ikiwa serikali itashindwa kulipa malimbikizo hayo litakuwa tayari kuongoza mgomo.